Thank God for giving us Magufuli aka jiwe aka chuma.

Surya

JF-Expert Member
Jun 7, 2015
8,363
12,537
Nasikitika sana kuona member wanao unga mkono uzi ulio pewa jina sawa na uzi huu usemavo apo juu, na kumpa like.

Nanukuu kauli.. "Cartoon pic"
"Mtoto- baba ukitaka upande chati kisiasa unafanyaje?
Baba- tafuta tatizo alafu litatue."
Ndicho kilichofanyika katika kikokotoo na viongozi wa ccm na serikali,
Baada ya wananchi kulalamika kuhusu mafao yao na kuona kero nyingi kutokea, wakaona kutatua maana maji yaliwafika shingoni.

Niseme jambo la kweli,
Wananchi walio wengi wamekua wakilidhishwa na baadhi ya mambo ambayo hufanywa na serikali ya sasa na kusahau nchi yetu iko wapi kiuchumi na inakwenda wapi?
Je tunanufaika sawa kulingana na mali zetu za nchi pamoja na jasho letu wananchi kama kodi tunazo toa??
Kiongozi wa nchi hufanya mengi na kujionesha kwa mengi kuwa anafanya hili kutuliza mihoyo ya wachache wetu ambao ni wafupi wa fikra.

Niseme tena maendeleo hayana chama.
Tunahitaji kiongozi ambae atasimamia haki na kufatwa kwa katiba ya nchi.

Rais anahitaji kuwa mtu mwenye ulewa mkubwa kuhusu jinsi ya kuipandisha nchi kiuchumi,

Nashaangaa kuona kiongozi ambae sio mjasilia mali hata kidogo anakupa sera ya hapa kazi tu, na huku hakuna sera ya yoyote ya nchi inayo husu kuongeza ajira katika nchi.

Elimu ambayo ndio nguzo ya kila mwananchi sela zimeishia kidato cha nne elimu bure, baada ya hapo unataka mwananchi huyu akafanye nn?

Tatizo naona ni kuwa mtu analidhika na machache ambayo kiongozi ambae yupo kayafanya, na kusahau mangapi tunataka katika nchi yetu.
Mfano: ni kama mashabiki wa Arsenal walivokua na kocha wao Wenger muda mwingi waliona ngoja tuone ataendelea kutupa lipi!, mwishowe hakuna step kubwa ambayo walivuka,

lakin timu zingine kama Manchester united ni dakika sifur tu wanakutupilia mbali na kwenda kutafuta maendeleo kwengine. Kwani wanajua hawastahili kupata kidogo.

Naomba wananchi wenzangu kuweni kama vilabu ambavyo hutimua makocha na kuleta kocha mwengine kama vile walichokifanya Man u au Liverpool.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom