Wataje basi na kuainisha maovu yao ili tulifanyie kazi lalamiko lakoUkiacha kulipwa Mshahara mzuri na marupurupu mengine , likiwemo V 8 labda na Mamlaka ya kiofisi , ukweli ni kwamba wengi wanaoteuliwa kwenye cheo hiki kwa sasa hawaakisi ukubwa wa cheo chenyewe .
Wateuliwa wengi ni wale waliosaliti walikotoka baada ya kuahidiwa vyeo hata kama tabia zao ni za "Kisela" ukiwemo ulevi na ukosefu wa adabu na maadili , jambo ambalo linawafanya wananchi kupigwa na bumbuwazi huku wakishindwa kuendelea kukiheshimu cheo hicho , kiukweli sisi tulio mtaani ndio tunaojua nani ni nani , sasa unapoteua mtu kuwa DC kwa vile tu aliwahi kuvaa fulana ya chama hata kama uadilifu wake ni sifuri inaletea ukakasi mno
Ukiacha Protocal ya kuheshimu Mamlaka ya Uteuzi , ukweli ni kwamba Wakuu wengi wa wilaya wanaoteuliwa hawaheshimiwi na wananchi kutokana na vituko vyao kabla ya teuzi , wengi tumeishi nao na tunawafahamu kuliko hata anayewateua na wala hatudanganyiki
NAKULILIA TANZANIA