Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,567
- 217,920
Ukiacha kulipwa Mshahara mzuri na marupurupu mengine, likiwemo V 8 labda na Mamlaka ya kiofisi , ukweli ni kwamba wengi wanaoteuliwa kwenye cheo hiki kwa sasa hawaakisi ukubwa wa cheo chenyewe.
Wateuliwa wengi ni wale waliosaliti walikotoka baada ya kuahidiwa vyeo hata kama tabia zao ni za "Kisela" ukiwemo ulevi na ukosefu wa adabu na maadili , jambo ambalo linawafanya wananchi kupigwa na bumbuwazi huku wakishindwa kuendelea kukiheshimu cheo hicho , kiukweli sisi tulio mtaani ndio tunaojua nani ni nani , sasa unapoteua mtu kuwa DC kwa vile tu aliwahi kuvaa fulana ya chama hata kama uadilifu wake ni sifuri inaletea ukakasi mno.
Ukiacha Protocal ya kuheshimu Mamlaka ya Uteuzi, ukweli ni kwamba Wakuu wengi wa wilaya wanaoteuliwa hawaheshimiwi na wananchi kutokana na vituko vyao kabla ya teuzi, wengi tumeishi nao na tunawafahamu kuliko hata anayewateua na wala hatudanganyiki.
NAKULILIA TANZANIA