Chingwanji
Member
- Oct 18, 2006
- 54
- 2
2008-03-15 08:54:40
Na Dunstan Bahai
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu, amesema thamani ya Shilingi imepanda kutokana na benki hiyo kujitahidi kudhibiti mfumuko wa bei.
Aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam ikiwa ni mara ya kwanza katika utaratibu aliyojiwekea wa kuzungumza na waandishi wa habari kila baada ya miezi mitatu kuhusu shughuli za benki hiyo na hali ya uchumi nchini.
Alisema dola moja awali ilikuwa ni Sh. 1,300 lakini sasa ni Sh. 1,160.
Hata hivyo, alisema kupanda kwa shilingi pia kumechangiwa na kukuwa kwa uchumi hasa kwa sekta mbalimbali kwa kuwa na mchango mkubwa katika pato la Taifa.
Alisema kilimo kimepitwa sana na sekta nyingine katika kuchangia pato la taifa.
Alisema katika mwaka uliopita wa fedha, pato la taifa kwa mauzo ya bidhaa nje ya nchi na huduma lilifikia dola bilioni 3.5 ambapo mazao ya kilimo thamani yake ilikuwa ni dola milioni 300 sawa na asilimia 10 tu ya pato la Taifa.
Kwa upande wa usafirishaji, sekta hiyo alisema iliingiza dola milioni 340, viwanda dola milioni 350 wakati sekta ya madini dola milioni 800.
Kuhusu matumizi ya dola ndani ya nchi, Profesa Ndulu alisisitiza kuwa sheria mpya za benki hiyo zinamkataza mtu au taasisi yoyote kumshurutisha Matanzania aliyeko ndani ya mipaka ya nchi kutumia dola.
Alisema atakayebainika, sheria iko wazi ya kumshtaki au kumchukulia hatua nyingine yoyote.
Kuhusu akaunti ya madeni ya nje (EPA) alisema BoT imekwisha unda kamati kuchunguza na kwamba upouwezekana hata akauti hiyo ikafutwa.
``Kuna shughuli nyingine zimeingia BoT kama mzigo kwani si kazi ya benki Kuu kuzifanya. Kazi kuu za BoT zimeainishwa bayana kama vile kusimamia uchumi wa nchi, kusimamia na kuangalia usalama wa benki na taasisi nyingine za kifedha, kudhibiti mfumuko wa bei, kuhakikisha malipo yako salama,`` alisema.
Alitoa mfano wa shughuli zilizokuwa zinafanywa na BoT ambazo si za msingi kama za ununuzi wa dhahabu uliokuwa ukifanywa na benki hiyo katikati ya miaka ya 1992 na 1994.
Kwa mujibu wa Gavana huyo, BoT iliingia kichwa kichwa kufanya biashara hiyo pasi kuijua ingawa hakutaja hasara labda iliyojitokeza hadi kusitisha kuendelea na biashara hiyo.
Alisema zipo shughuli nyingi zinazofanywa na benki hiyo ambazo si za msingi na hivyo kuna kazi ya kuzichunguza na zipo ambazo zitafutwa.
Kuhusu mikopo inayofanywa na benki za biashara na taasisi za kifedha, alisema BoT inajitahidi kupunguza riba kwa taasisi hizo ili nao washawishike kuwapunguzia riba wakopaji.
Kuhusu uvumi kuwa wapo waajiriwa wa BoT ambao hawana sifa, alisema kazi inafanywa ya kuwachunguza na ikibainika ni kweli, wataachana nao.
SOURCE: Nipashe