THAMANI ya shilingi ya Tanzania imeshuka kwa asilimia 50 kuanzia mwaka 2002 hadi Juni

Ntemi Kazwile

JF-Expert Member
May 14, 2010
2,182
307
Thursday, 15 July 2010 08:27
Fredy Azzah (Mwananchi 15 July 2010)

Ripoti iliyotolewa na Kitengo cha Takwimu cha Taifa mwishoni mwa wiki imefafanua kuwa fedha hiyo, imeshuka kwa sababu bidhaa ambayo ilikuwa ikinunuliwa kwa Sh 50 mwaka 2002, hivi sasa inanunuliwa kwa Sh 100.


Taarifa hiyo, ilifafanua kuwa, bei za bidhaa zimeongezeka kutoka Sh168.1 Juni 2009
hadi Sh 180.2 Juni mwaka huu 2010.


“Thamani ya Sh100 katika manunuzi ya Juni 2002 inaonyesha kwamba imeshuka hadi kuwa sawa Sh57.31 Juni 2010,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.


Taarifa hiyo pia ilisema, mfumuko wa bei za bidhaa ambazo siyo za vyakula umepanda kwa asilimia 0.6 kufikia Juni 2010.


Taarifa hiyo, ilifafanunua kuwa bidhaa hizo ni
mavazi ya watoto, mafuta ya taa, mkaa, samani, pamoja na mafuta ya dizeli na petroli.


Baadhi ya bidhaa hizo, zimekuwa zikinunuliwa kwa dola huku thamani ya shilingi ikiendelea kushuka, hivyo mlaji kulazimika kununua kwa bei ya juu kufidia gharama ya dola.




Pia taarifa hiyo ilionyesha kuwa, mfumuko wa bei kwa bidhaa za vyakula, uliopimwa kwa kigezo cha mwaka wa fedha ulioisha Juni 2010, umepungua hadi asilimia 7.2 ikilinganishwa na asilimia 7.9, Mei 2010.


Kutokana na takwimu hizo, Serikali imefikia malengo yake ya kushusha mfumuko wa bei hadi kufikia chini ya asilimia 10 kufikia mwishoni mwa Juni 2010.


Malengo hayo, yalikuwa yameainishwa katika hotuba ya bajeti ya Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustapha Mkulo aliyoitoa Bungeni alipokuwa akiwasilisha bajeti ya mwaka 2009/10.


Taarifa hiyo, ilieleza kushuka kwa mfumuko wa bei, kwa bidhaa za vyakula umepungua hadi asilimia 7.1 kwa mwaka wa fedha ulioisha Juni 2010 kulinganisha na asilimia 8.1, Mei mwaka huu.


Ilisema mfumuko wa bei za bidhaa zisizo za vyakula umepungua hadi asilimia
7.5 katika mwaka wa fedha ulioisha, ikilinganishwa na asilimia 7.7, Mei mwaka huu.


“Kupungua kwa mfumuko wa bei kumechangiwa hasa na kupungua kwa bei za bidhaa za vyakula kwa asilimia 2.0,” ilieleza taarifa hiyo.


Taarifa hiyo, ilizitaja baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kupungua kwa bei kuwa ni nafaka, ndizi za kupikwa, baadhi ya matunda na njegere.
 
Back
Top Bottom