Thamani ya maisha huongezeka ukipita bonde la mauti

Elisha Chuma

JF-Expert Member
Jul 22, 2013
275
262
Mara nyingi mwanadamu akichomwa na mwiba ndio huona thamani ya kandambili (ndala) lakini kabla ya hapo zinaitwa malapa ya kuendea chooni.

Hali hii imeendelea kwa vitu vingi tunavyovohisi muda mwingine ni vidogo na havina thamani lakini tunavihitaji sana.

Asilimia kubwa yetu uhai na pumzi tunayovuta tunaichukulia kawaida, kulala na kuamka salama tunaona kawaida kwa vile ni kitu kinachojirudia kila siku na wengine hata wanapopata matatizo hukimbilia hata kuwaza kwanini wanaishi ama maisha kwao hayana thamani.

Wanasindikiza wanaoishi na maneno kadha wa kadha, lakini siku unayopewa sababu ya kuona maisha yako yanakatishwa na kitu kifulani aidha ugonjwa, ajali, maradhi n.k ndio uthamani wake huja.

Iko vivyo hivyo kwenye kila kitu unachokifanya kipe uthamani kabla hakijapotea elimu yako ni ya thamani sana usisubiri hadi ufe ndio tuone madaftari ya mipango yako mizuri.

Anza kufanyia kazi ukiwa hai. Afya yako ni ya thamani usisubiri hadi uwe hospitali ndio uanze kuuona uthamani wake.

Anza kuitunza afya yako. Familia yako ni ya thamani usisubiri hadi upate shida ama wanapofariki ndio uuone uthamani wao. Anza kuipenda, kuijali na kuilinda familia yako.

Wewe ni wa thamani usisubiri hadi ufanikiwe ndio uanze kujiona wa thamani. Anza kujipa hadhi ya ndoto yako na milango yako itafunguka.

Dhima ya huu ujumbe ni kwamba usipoteze uthamani kwa changamoto zako, usirudi nyuma, usipoteze nguvu yako uliyoanza nayo.

Songa mbele na uone uthamani wa hatua zako hata kama ni kidogo, kama unasita kuanza anza kupiga hatua leo ile hatua ndogo unayoinyanyua inatosha kukupa thamani ya kuishi.

Neno la faraja ukiwa umevunjika moyo linatosha kukuinua na kukupa furaha na tumaini kwanini isiwe na kwenye malengo na maisha yako kwa ujumla.

Anza leo, maisha ni haya haya wa kubadilika ni wewe.

Elisha Chuma

20191226_070719_0000.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom