Thamani ya kura yangu Tanzania na Zanzibar haipo tena ?

battawi

JF-Expert Member
Mar 29, 2014
2,672
2,540
Mimi kama mzanzibari niliyeshiriki chaguzi kadhaa hapa Zanzibar za kuchagua viongozi wa nchi.
Lakini mwaka 2015 umenivunja moyo kabisa baada ya kuona kura yangu ikipeperuka bila kujaliwa shida iliyonipata kwa kutumia muda wangu mwingi kujiandikisha,kuhakikiwa taarifa zanzzgu na mwisho kujipanga kwenye misururu mirefu ili kupiga kura.

nilikuwa na dhamira maalumu ya kupiga kura hii ambayo ni kuleta mabadiliko ya kiutawala na kuipa zanzibar GOOD BREXIT kama wengi wetu tunavyotaka zanzibar yetu iwe na mamlaka yake.Hii ni baada yakujuwa kuwa miaka mingi huko nyuma kura yangu haikuwa na maana yoyote ,hasa enzi zile za NDIYO na HAPANA. sikuwahipo kupiga kura hata kwa bahati mbaya zama zile.



Kubatilishwa kwa matokeo bila ya sababu za msingi kumenifanya nirudie kwenye Imani yangu ya ZAMANI ya kuto ithamini tena Kura nchi hii hasa Zanzibar.

Nahisi ni sawa na ILE ya NDIO NA HAPANA . yaani hakuna isipokuwa yeye, na ndiyo yeye tuu.

Sasa nataka nijifunze kutafuta njia nyingine isiyokuwa ya kura ili kupata demokrasia ya kweli Zanzibar na Tanzania. Kwani imekuwa kizungu mkuti kila uchao.



kubwa zaidi eti ''TUME YA UCHAGUZI IKO JUU YA SHERIA, HAKUNA MWENYE HAKI YA KUISHTAKI POPOTE PALE


Nashangaa wanao tuhamasisha kushiriki utumbo huu tena

MIMI NADHANI KURA BASI LABDA KATIBA IBADILISHWE AU PATOKEE LA KUTOKEA KUBADILISHA MFUMO WA NCHI.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom