Thamani ya dola dhidi ya TZS

sem2708

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,204
4,211
wanaJF,nimekuwa nikiangalia inflation rate kwa maana ya thamani ya TShs vs US$,kwa takriban mwezi sasa,imekuwa ikipanda kwa kasi ya ajabu
mathalan leo nimepitia bureau exchange kadhaa maeneo ya posta na kukuta duka moja la pesa WANANUNUA DOLAa moja ya marekani kwa i Tshs 1680...
i was shocked. hivi tunaelekea wapi? serikali yetu inaliona hilo? na je inachukua hatua gani?
kwa hali hii tunahitaji tamko toka kwa gavana atuambie mikakati ya kuthibiti mfumuko huu wa bei na ya kuwa kuna mikakati gani ya kuthibiti hali hii
 
Angalia subject heading ya topic haijakaa sawa. Wapi tunaelekea: "Tunaelekea kuzimu, hatuna serikali hivyo hakuna hatua yoyote itakayochukuliwa" bali mimi na wewe na yule ndiyo tuchukue hatua. Matatizo haya na mengine kama ya Richmond/Dowans, Wizi wa fedha za EPA, ugumu wa maisha, kupanda bei ya bidhaa na kadha wa kadha tuyatolee tamko. Tutumie haki yetu kwa kufanya maandamano ya amani tuyatolee tamko. Gavana hawezi kutuambia chochote kwa sababu yeye ni sehemu ya tatizo.
 
Punguza jazba mtoa mada, nadhani unamaanisha TZS against USD.
Kwa wanao export ndio wanapiga hela na export ya bidhaa inaongozeka.
Wacongo wanasema, 'unakwenda na makuta(pesa) kadogo kudaresalama na unauuza(unanunua) vitu mingi'.
Ila tunauumia ktk kuagiza bidhaa kama mafuta ndio noma
 
kwa ujumla hali si njema...,mie nimepita mchana bureau de change nyingi zilikuwa zinauza dola moja mpaka sh.1,700/= -1,705/= hii hali haiashirii bali ishakuwa mbaya!
 
kwani Tanzania tuna viongozi wa kuona vitu kama hivi?eti thamani ya Tsh inashuka? Viongozi wetu wa chama tawala si ndo WAFANYA BIASHARA WAKUBWA? Wao ndio kwanza wanachacharika ku import vitu wapige hela zaidi...hii nchi iko kama haina wenyewe!
 
Kwani thamani ya dola na inflation kwa mujibu wa mtoa mada ni sawa? Hapa analinganisha inflation na flactuation ya dollar au? I stand to be corrected
 
Back
Top Bottom