Thamani ya Dawa na Vifaa Tiba Vilivyo Expaya MSD ni Zaidi ya Tsh 20 Billion; CAG Hajaripoti

Stuxnet

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
4,778
2,000
Wakati wananchi wanalalamika ukosefu wa dawa kwenye hospitali na zahanati, yasemekana kwenye Bohari Kuu ya Madawa (MSD) kuna dawa zilizo expaya za thamani ya zaidi Tsh Bilion 20. Nimepitia ripoti ya CAG ya mwaka 2019/20 kwa haraka haraka sijaona hoja ya ukaguzi kuhusu dawa zilizo expaya.

Je timu ya CAG iliyotumwa MSD haikuliona hili?

Ushauri:
Hata kama CAG hakuliweka Wabunge waliopo kwenye Kamati ya Huduma za Jamii wanaweza kumuuliza Waziri wa Afya alitolee majibu kwa vile kiasi hicho ni kikubwa sana kuharibika wakati wananchi wanakosa hata dozi ya Panadol kwenye zahanati
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
5,692
2,000
Hiyo ripoti hukutakiwa kuipitia haraka haraka, unatakiwa uipitie kwa makini uje na habari complete hapa jf.

Hao MSD nao nasikia wanaidai serikali pesa zao hawalipwi, kama ni kweli hii taarifa yako basi na serikali itakuwa inachangia kuimaliza MSD kwa kulimbikiza madeni.
 
Huihui2

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
1,255
2,000
Wewe taarifa za madawa kuexpire umezipata wapi?
Kama hamuitaki mwaka huu basi mtakutana nayo mwaka kesho. Anyway kipindi cha Mwendazake taarifa zilikuwa zinafunikwa sana ndiyo maana wabunge akina Msukuma na Deo Sanga walidhani Magufuli anadhalilishwa
 
Stuxnet

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
4,778
2,000
Wewe taarifa za madawa kuexpire umezipata wapi?
Hapo ndipo tofauti ya ma great thinker wa JF na watu wa kawaida. Nina chanzo changu ndicho kimenijuza.

Uzuri ni kwamba MSD ni public parastatal na hizi siyo Siri. Ukienda kununua dawa kwenye maghala yao utaambiwa hakuna. Lakini unaziona zimejaa kwenye maghala ya Dar, Moshi na Tanga. Ukiwauliza wanakuambia zime expaya. Ndiyo nilivyopata taarifa hii
 
bnhai

JF-Expert Member
Jul 12, 2009
2,397

Kuwa great thinker ni kuleta ushahidi na sio majungu. Leta ushahidi.
 
Stuxnet

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
4,778
2,000
Kuhusu madeni kwenye ripoti ya CAG yako covered vizuri na Serikali imeahidi kuyalipa baada ya kuyahakiki. Nilichoshangaa ni kiasi kikubwa cha dawa ku expaya bila kutumika wakati wananchi wanakosa dawa kwenye vituo vya afya.
Hiyo ripoti hukutakiwa kuipitia haraka haraka, unatakiwa uipitie kwa makini uje na habari complete hapa jf.

Hao MSD nao nasikia wanaidai serikali pesa zao hawalipwi, kama ni kweli hii taarifa yako basi na serikali itakuwa inachangia kuimaliza MSD kwa kulimbikiza madeni.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom