kitokololoo
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 704
- 813
Ninaandika huu uzi japokuwa wengi hawatakubariana na hichi nachosema.
Mimi nimezaliwa mpaka najitegemea sijawahi uona upendo wa mama yangu
My story: Baba yangu na mama yangu walitengana nikiwa na miaka miwili mama aliondoka na kwenda kuolewa na mwanaume mwingine toka hapo baba yangu alikuwa ndiyo mama yangu ndiyo baba yangu.
Baba alihakikisha nakula,navaa,nasoma miaka ikapita nami Mwenyezi Mungu akanijaharia nikamaliza chuo na kupata kazi na kujitegemea.
Mpaka naandika uzi huu wazazi wangu wote wameshafariki Mwenyezi Mungu awapumzishe kwa amani
Kipindi cha msiba wa marehem baba yangu nililia sana kwa uchungu sana maana nilikuwa peke yangu mama yangu kanitenga kaka ambao tumechangia baba tu walikuwa botswana migodini huko hivyo walichelewa kufika msibani niliumia sana kumzika baba yangu peke yangu bila mama yangu kuja msibani.
Baada ya msiba nilisikia ndugu zangu wakisema huyu mtoto kalia sana kwa sababu mama yake alimwacha mdogo sana pia wakati mama yake anaondoka alitamka maneno makali sana kwamba mama yangu alitamka kwamba mimi naondoka namwacha mtoto wenu akifa mtajua nyinyi akipona mtajua nyinyi hayo ni maneno ya mama yangu mbele ya baba yangu na ndugu zangu.
Sababu kubwa ya mama kuondoka nyumbani ni kuwa hali ilikuwa ngumu ya kiuchum nyumbani lakini hata kama ndiyo hivyo mama yangu hakunionea huruma mimi na kuniacha nikiwa na umri mdogo kiasi kile mpaka aniache na baba yangu kweli?
Baadae baba alipata kazi shirika la reli maisha na akawa pia pale nyumbani anafuga kuku nakumbuka na ng'ombe na kulima pia kaka zangu walikuwa wanamsaidia sana kidogo maisha yakabadirika nyumbani lakini baba yangu hakuamua kuoa tena mpaka anapofariki.
Huwa naumia ile kauli aliyotamka mama yangu kwamba kama ndugu zangu wakiniacha nife sawa nikikuwa sawa lakini bado nampenda kama mtu aliyenizaa.
Lakini kwangu thamani ya baba ni kubwa kuliko ya mama katika maisha yangu sijawahi pata upendo wa mama zaidi ya wema wa kunizaa.
Japo ntakosolewa kwa nilichokiandika ila hayo ndiyo maisha yangu na ndiyo nionavyo mimi.
Mwenyezi Mungu awape pumziko la milele wazazi wangu na wazazi wa wengine waliofariki Amen..