Thadei Ole Mushi: Tukimaliza royal tour tujikite kutatua matatizo yetu ya ndani kwenye utalii

Alex Fredrick

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
680
1,338
TUKIMALIZA ROYAL TOUR TUJIKITE KUTATUA MATATIZO YETU YA NDANI KWENYE UTALII.

Na Thadei Ole Mushi.

Kutangaza Utalii wa nchi yetu ni jambo moja, lakini kupata faida kutokana na matangazo hayo ni jambo jingine. Kutangaza tu bila kushughulika na matatizo ya ndani tutabaki pale pale tulipo. Mama Samia ana nia ya dhati kabisa ya kuutangaza utalii wetu, lakini tusisahau kuwa Matangazo bila strategy za ndani tutakuwa hatujafanya kitu. Nchi zinazoongoza kwa utalii Africa hazijatangaza kwa kiwango cha Tanzania inavyofanya.

Kwa nini tunapitwa pamoja na kwamba tunatangaza kwa wingi?

Mwaka 2020 katibu wa wizara ya Utalii kipindi hicho Dkt. Aloyce K. Nzuki aliwahi kusema kuwa watalii wanaokuja kutalii Tanzania asilimia 80 ni wageni wapya kabisa ambao hawakuwahi kufika Tanzania na asilimia 20 tu ndio huwa wanarudi kuja kutalii Tena. Alikuwa amewaita waandishi wa Habari pale Ngorongoro wajadili kwa nn watalii hawarudi.Tafsiri yake kwa Lugha Rahisi ni kuwa watu hutamani kuja Tanzania kutalii lakini wakishakuja hukinai na hawatamani tena kurudi, nilishauri mambo kadhaa ambayo nilitamani Waziri wa Utalii Kipindi kile Dr Ndumbaru angedili nayo ili watalii wavutike kuja zaidi Tanzania lakini bado naona matatizo yale yapo pale pale...

Shida yetu kubwa haipo kwenye matangazo bali ipo kwenye mambo yafuatayo:-

1. Gharama.

Ukichukua nchi kumi Africa zenye Bei nafuu kwa utalii Tanzania haitoonekana.

Nimepitia mtandao wa Bigworld Small Pocket wametaja mataifa ambayo gharama za utalii Ni ndogo kuliko nchi nyingine.

Nchi inayoongoza kwa kuwa na gharama ndogo ni Morroco. Mtandao huo unasema ukiwa Morroco na mfukoni ukiwa na USD 30-40 sawa na shilingi 69,570 hadi 92,762 unaweza kugharamia chakula, malazi, Usafiri na viingilio vya sehemu mbambali zenye vivutio vya utalii hizi Ni gharama za siku moja pale Morocco.

Mtandao huo unataja nchi ya Pili yenye gharama sawa na Morroco kuwa Ni Tunisia na ya tatu ni Misri. Nikatamani kuangalia kwa Tanzania nikakuta kuwa mtalii aliyejibana Sana kwa siku anatumia 170,000 hapo hajakutana na waongoza watalii ambao wameshamsokota na kumuomba simu au chochote akiwa naye kwenye matembezi. kwa hiyo fedha ya kutumia siku moja kwa mtalii Tanzania unaweza kuitumia Pale Morocco kwa siku tatu.

Imekuwa ni kawaida kwa Tanzania mtu akishaitwa mtalii kumbambikia Bei za ajabu ajabu kwenye mahitaji yake chumba Cha elfu 40 atauziwa Laki, chakula Cha 5,000 atauziwa 15,000.

Ukikutana na mtalii huko mtaani kawa mwekundu na anatembea Kama kichaa kwa sababu ya Mambo haya ya nn kurudi Tena Tanzania?

2. Mabalozi.

Mwaka 2020 binafsi sikuona sababu ya Katibu wanWizara ya utalii kuwaita waandishi, badala yake katibu angeshugulika na mabalozi wetu kwenye maeneo mbalimbali Duniani. Hawa wanaweza kuwa na impact kubwa kuliko waandishi wanaoandika habari za ajabu ajabu ambazo hazina tafiti. Waandishi wetu asilimia kubwa hawana uwezo Tena wa kutafiti na kutengeneza agenda badala Yake wamebakia kuwa maripota wa matukio.

Nafikiri tufungue madawati ya utalii kwenye Balozi zetu na tuwape kazi na kila mwaka Dawati hilo watajaza dokezo la wameweza kuleta watalii wangapi.

3. Mipango na Sera.

Je Tanzania tuna Mpango wowote (Document) inayoonyesha kwa miaka 5 ijayo Ramani ya utalii inatuelekeza kwenda wapi?

Hawa Morocco mwaka 2001 walianzisha project ya kukuza utalii inaitwa "Plan Azur" katika plan hiyo walilenga kujenga Resorts Hotel za kisasa kabisa lakini walizoziuza kwa Bei nafuu Sana.

2010 Wakaja na plan ingine inayoitwa "Vision 2020" . Sisi tukaanzisha ya kwetu ya "Mpaka Kileleni" iliyotaka kumuua Steve Nyerere kule Mlimani ambayo haina tofauti sana na hii ya waandishi wa habari kujadili utalii huko Ngorongoro.

Tuna mipango ya muda mrefu yenye kuakisi ushindani wa Biashara hii ya utalii?

4. Je Watalii waliokwisha kutalii hapa kwetu Tanzania tunawapa discount yoyote wakitaka kurudi?

5. Je tunawahudumiaje Watalii wetu kuanzia wanapotua Hadi wanaondoka? Wanaondoka wakiwa na furaha au wanaondoka wakiwa na proposal kibao za kuombwa hela? Wahudumu wetu wanawahudumiaje huko mbugani na mahotelini?

Mambo Ni mengi Ila tujiulize kwa haya je Kuna mtalii atakayetamani kurudi?

Mwaka 2019 Morocco walipata Watalii Milioni 12.93, wakafuatiwa na S.Africa Milioni 10.23 na kwenye kumi Bora Tanzania hatupo. Sisi tuliingiza Watalii Milioni 1.5 kwa ratio hiyo itabidi tukae miaka kumi kupata Watalii wa Morocco wa mwaka Mmoja.

Ole Mushi
0712702602
 
Pale arusha makamupuni ya utalii yakuomuona mtalii yanafikiria kumuibia na kuwa omba omba kuanzia ngono Hadi nguo
Mtalii anasumbuliwa hadi kero

Haya ile safari ya kutoka arusha kwenda karatu haina mvuto kabisa sawa na kule mikumi
Njiani ni jangwa hakuna miti

Hata kama ni mimi nisingerudi
 
Lkn bwan mushi ikumbukwe kuwa Morocco ipo karibu San na mataifa ya ulaya na vilevile south Africa wazungu walikuepo hapo enzi na enzi siyo ajabu kbsa kukuta idadi kubwa ya wagen ktk nch hzo

Mfno tu Morocco imeungana kbsa na Spain kat ya kilomita tatu had nne unaingia ulaya Kama Italy Spain ureno

Kimsingi tuongeze juhudi na elimu ya hospitality ya Hali ya juu Sana na kupunguza garama zile fee itazamwe upiya bila kujali Kenya wanafanyaje itafiaka mahali influx kubwa ya wagen wametapaka Hadi huko burugi mbug yetu ya michongo
 
Pale arusha makamupuni ya utalii yakuomuona mtalii yanafikiria kumuibia na kuwa omba omba kuanzia ngono Hadi nguo
Mtalii anasumbuliwa hadi kero

Haya ile safari ya kutoka arusha kwenda karatu haina mvuto kabisa sawa na kule mikumi
Njiani ni jangwa hakuna miti

Hata kama ni mimi nisingerudi
Pale Arusha makamupuni ya utalii yakuomuona mtalii yanafikiria kumuibia na kuwa omba omba kuanzia ngono Hadi nguo
Mtalii anasumbuliwa hadi kero



Mijamaa ya Arachuga imepinda. Kusuka kama dada zetu ni wao, kuoa viajuza wao, kuomba ngono kwa watalii wao, kuomba nguo wao, khaaaaa!!

Bwasheee Ole Mushi wasamehe hawa ndugu zetu!!!



Wanadhani ngono ndio utalii waliyoifuata Tanzania kumbe vivutio tulivyonavyo.
 
poor communication skills,
yaani mtu anaenda na mgeni safari hadi anarudi hakuna maelezo yoyote mgeni anapewa..poor service.

hygienic is very poor for some of the mountain guides and safari.mgeni anapewa chakula kabla ya kula anaanza kumeza vidonge vya kuzuia kuharisha!

mountain guide anavaa ovyo ili mgeni siku akiondoka amwachie gears and other materials..shame

Rais alitoa kibunda ili watu waende training..hapo kidogo naona mambo yanaeza kwenda vizuri huko mbeleni.
 
Tour Operator akikata leseni, example June, ikifika Dec ime expiree

Hata akikata October, ikifika Dec ime expiree
 
Back
Top Bottom