Thadei Ole Mushi: Mwigulu Nchemba anatufundisha jambo hapa

Alex Fredrick

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
680
1,338
MWIGULU ANATUFUNDISHA JAMBO HAPA.

Na Thadei Ole Mushi

Mimi si muumini wa iyena iyena lakini katika hili acha niseme kidogo.

Mojawapo ya picha ya Bunge iliyo trend Sana Jana ni ya Mwigulu Nchemba akiwa na Wabunge wawili mmoja ni Senetor Festo Tuntemeke Sanga Mbunge wa Makete na Mwingine ni Reuben Kwigila Mbunge wa Handeni mjini.

Hoja kubwa kwenye ile picha ni namna ambavyo Mwigulu Nchemba anavyosaidia vijana wanaomzunguka kutimiza ndoto zao..

Ni ukweli usiopingika kuwa Mojawapo ya Sifa kubwa aliyonayo Mwigulu Nchemba ni kusaidia wale wanaomzunguka kufikia malengo yao. Aidha kwa ushauri au hata msaada kifedha. Ni tabia ambayo Viongozi wengi waliofanikiwa hawana.

Kama kila kijana akiyefanikiwa akiwa na moyo huu alionao Mwigulu basi vijana wengi sana watafikia ndoto zao. Ukiachana na hii picha ya Hawa wabunge wawili List ya vijana ambayo Mwigulu kawavusha kwenye Mambo mbalimbali ni kubwa Sana.

Mwigulu hatumii vijana wanaomzunguka Kama punda au Daraja la kuvuka yeye. Bali Yeye ndiye amekuwa Daraja la kuwavusha wengine. Picha mbili za chini ni watoto ambao Mwigulu anawasomesha katika shule mbalimbali nchini. Hawa anajitolea fedha zake kuwasomesha.

Hili ni la kupongeza na funzo hili litumike kutufundisha sisi wengine namna ya kuvusha wanaotuzunguka. Katika nafasi zetu tuna watu wa kushika mkono na kuwasaidia kutimiza ndoto zao. Tupunguze ubinafsi na tujifunze Jambo hili jema toka kwa Savimbi wa Iramba Singida.

Hongera Sana Mwigulu.

Ole Mushi.
0712702602.
FB_IMG_1605072636539.jpeg
FB_IMG_1605072632498.jpeg
FB_IMG_1605072627450.jpeg
 
Kumchukia MWIGULU ni sawa na kujichukia......
binafsi nlikuwa namchukia tena sana ila kuna mambo nimejayajua .......inashangaza na kwa sasa mimi ni shabiki wa kufa wa huyu mwanasiasa
 
Mwigulu ni mtu sana,ni zaidi ya watu wanavyomuona Bungeni....binafsi yangu natamani siku moja awe rais
 
Mbio za urais 2025 zimeshaanza.

Kigwangalla naye atawaleta wa kwake akina mwanaFA.

January naye ataweta akina Freddie nk nk!
 
Kila nkiona post ya mwigulu nakumbuka zile chapa za barabarani za "Mwigulu raisi"
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom