THABEET HASHIM:- Breaking Newzzzzz!

Apr 27, 2006
12,621
1,241
Wakuu kama kawaida heshima kwa Tanzania, kijana wetu Thabeet Hashim, sasa hivi anaichezea UN-CONN(Universty Of Connecticut) inapambana na Memphis, angalia kwenye ESPN2 kwa wale wanaoweza,(Hashim ni Future NBA Candidate)

so far yeye ndiye anye-make a big different katika shule yake comeback, baada ya kuongozwa kwa 20-5, na sasa ni 60-60, wakuu tuangalie fahari ya nchi yetu, Tanzania kudos kwa wa-Tanzania walioko hapo uwanjani Madison Square Garden, na hasa member mmoja wa hii forum ambaye amekuwa akionyeshwa sana kwa kuirusha sana bendera yetu hapo uwanjani,Mungu Aibariki Tanzania.

Admin, mpira utaisha baada ya kama dakika 35 zinazofuata, unaweza kuifuta au kuihamisha.
 
malezi ya Hasheem ni kutokana na sera nzuri za ccm! teh teh teh

Kwi kwi kwi!!!!!

Lakini huko nyuma kabla ya vyama vingi, Taifa Stars wakishinda tulikuwa tunashangilia hivi:

CCM, CCM, CCM na kuendelea.

Mara yangu ya mwisho kushangilia michezo TZ, nafikiri ilikuwa ubingwa wa ngumi East Africa, tulikuwa tunahitaji point moja kushinda hayo mashindano. Ilikuwa ndio pambano la mwisho la
uzito wa juu, Mtanzania alikuwa anachukua kipigo. Ghafla mungu saidia, Mtanzania akarusha konde la nguvu na nafikiri alikuwa Mzambia yule, hakuamka tena. Nilishangilia siku hiyo, sijawahi kushangilia tena maishani.

Yaani ilipigwa CCM hiyo mpaka naingia nyumbani bado mimi nimo tu CCM, CCM, CCM!!!!

Naona kungelikuwa na picha ya tukio hilo, sasa ningejionea huruma kweli kweli kwa kuimba CCM ya mafisadi kiasi hicho.

Lakini wakati ule hatukuwa na kingine zaidi ya CCM.

Hongera Thabeet, tunakutakia mafanikio mema, mtaji wa mchezaji ni juhudi na mazoezi.
 
Mkuu Mtanzania

Kama unamzungumzia Koba Kimanga ilikuwa ni kwenye mashindano ya afrika mashariki pale diamond jubilee nami nilikuwa mmoja wa washangilaji siku ile, yaani ilikuwa starehe kweli.....
 
Mkuu Masatu,

Uko sahihi kabisa, nimehudhuria michezo mingi baadaye, lakini hakuna siku niliyowahi kufurahi kama siku hiyo. Ile ilikuwa furaha ya Uzalendo.

Nilikuwa nakaa Temeke, nafikiri tulitembea kwa mguu doka Diamond Jubilee tukiimba hiyo CCM yetu mpaka Temeke.

Jamani kale kauzalendo ka taifa letu kameishia wapi? Wakati ule hata ungeniambia toa kila kitu ulicho nacho ili kuisaidia timu ya taifa, ningeweza kufanya hivyo bila hata kunung'unika.
 
malezi ya Hasheem ni kutokana na sera nzuri za ccm! teh teh teh

Mkulu Nurujamii,

Umesema wewe, mimi simo kabisaaa kwenye hili, ingawa it sounds good, yaani kama ulivyosema kuwa Hasheem ni matunda ya sera za CCM!
 
Nampongeza Hashem kwa kipaji chake alichompa Mungu(sijui naye mtasema ni CCM?). Sera nzuri kabisa ya CCM yenye kuwawezesha wachache kujifanyia jitahada zao wenyewe kutoroka nchi yao kwenda kutafuta fursa nchi nyingine na wengi kubaki hapa nyumbani hohe hahe. Ni sera nzuri hiyo inayouza viwanja vya michezo na kufanya watoto wa siku hizi wakose hata pa kuchezea rede na chandimu sembuse mpira wa kikapu. Ni sera nzuri kwa kweli yenye kujenga mtindio wa ubongo na hatimaye kutufanya tuamini kila kitu ni CCM. Narudia tena, ni sera nzuri ya umalaya wa kisiasa. Na chama chenye sera hiyo si kingine bali ni Chama Cha Malaya.

Ipo siku watoto wetu watawauliza

Asha
 
Wakuu kama kawaida heshima kwa Tanzania, kijana wetu Thabeet Hashim, sasa hivi anaichezea UN-CONN(Universty Of Connecticut) inapambana na Memphis, angalia kwenye ESPN2 kwa wale wanaoweza,(Hashim ni Future NBA Candidate)

so far yeye ndiye anye-make a big different katika shule yake comeback, baada ya kuongozwa kwa 20-5, na sasa ni 60-60, wakuu tuangalie fahari ya nchi yetu, Tanzania kudos kwa wa-Tanzania walioko hapo uwanjani Madison Square Garden, na hasa member mmoja wa hii forum ambaye amekuwa akionyeshwa sana kwa kuirusha sana bendera yetu hapo uwanjani,Mungu Aibariki Tanzania.

Admin, mpira utaisha baada ya kama dakika 35 zinazofuata, unaweza kuifuta au kuihamisha.

FMES tupe update zake,amefikia wapi huko connecticut?
 
Alishamwagwa kutoka ligi ya NBA.
Sasa hivi anachezea ligi hafifu ya daraja la pili ya NBA.
Angekuwa ana nidhamu ya mchezo na kujituma angefika mbali maana hakuna mchezaji mwenye urefu kama yeye kwa sasa katika NBA.
 
Aiiseeeee amedondoka sana mpaka daraja la pili?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom