TGNP yamshauri rais Magufuli kuangalia swala jinsia katika uteuzi wake wa viongozi

KaselengeJr

Member
Jul 6, 2016
22
9
Mwishowe TGNP wafunguka na kumshauri Rais JPM,kuzingatia jinsia kama inavyoelekezwa/shauriwa kwenye mikataba mbalimbali ya kikanda na kimataifa pindi afanyapo uteuzi wa viongozi mbalimbali.

Kwa kusisitiza hilo TGNP walifika mbali zaidi kwa kuchambua idadi ya kina mama walioteuliwa katika ngazi mbali mbali za uongozi ikiwemo zile za Mawaziri,Manaibu mawaziri,Makatibu wakuu na manaibu makatibu wakuu.Wakuu wa mikoa,wilaya na wakurugenzi halikadhalika akina mama walioteuliwa ni wa chache mno kuliko wale wa serikali ya awamu ya NNE chini ya Rais Kikwete.

Hawakuishia hapo skins mama hao wa TGNP waliendelea kusema kwa utaratibu huo itakuwa ni vigumu kufikia malengo ya kimelenia ya umoja wa Kimataifa paka kufikia mwaka 2025 kuwa uwakilishi wa 50% kwa 50% kati ya me na ke za uwakilishi kwa ngazi za juu za serikali.

Kisha wakasema Mh.Rais asihofu kuwateua akina mama kwani wapo wanaofaa kwa ujuzi na kuongoza na kwenda na kasi anayotaka Mh.

My Take: 1 nikuwapongeza TGNP kwa kutoa yao ya moyoni kwa kumshauri rais angalie (women impowerment & gender balance) nafasi na umuhimu ya kuwashirikisha wanawake katika uongozi.

02:Lakini pia nikufungua njia kwa makundi mengine ya kijamii yanayo hisi kwa njia moja au nyingine nao wamegwasa kama wana mtandao huo wa TGNP waweze kusema na kupaza sauti zao kueleza kilio chao kwa Mh.JPM,kwani Rais wetu na serikali yake ni serikali ya watu na na nisikivu

03: Kupitia ushauri huo Rais JPM asikie kilio hicho cha TGNP kama kina mantiki au kimebeba chembechembe za ukweli na kinatija afanyie kazi.
04: Kama hivyo ndivyo yanayosemwa na TGNP IPO haja ya Mh.JPM,kipenzi wetu kuangalia upya staili ya UTEUZI wake ili ibebe SURA ya kitaifa Kwa kuingiza / kuhusisha makundi yote makubwa na muhimu katika jamii kwa uwiano sahihi wa uwakilishi( ikiwemo makundi ya akina mama,vijana,wazee, na uwakilishi kwa IMANI ZAO).

Kufanya hivyo kutapunguza Malalamiko kutoka makundi husika,kutaleta upendo na kujenga/ kuimarisha zaidi mshikamano wa kitaifa,kutoa fursa sawa wa kuchangia Mawazo kutoka makundi hayo kwa serikali yao na mwisho kutoa fursa za ajira kwa makundi yote ya kijamii yanayounda nchi.

Mwisho,manunguniko kama hayo kama yana ukweli huweza kulibomoa Taifa.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Mimi tokea Mwenyezi Mungu alivyonyofoa sehemu yetu ya mbavuni na kuwaumba akina " Hawa " wala sishangai wakiwa wanakosa nafasi sehemu mbalimbali kwani hata Mwenyezi Mungu alitambua kuwa wao daima watakuwa ni Wasaidizi wetu tu hadi dunia iyeyuke na hata kama tukiamua kuwateua basi tutafanya hivyo kama sehemu ya kuwafurahisha ila daima Wanaume tutabaki kuwa Watawala na Viongozi wao watake wasitake au wanune wawezavyo.

Hawa TGNP kabla ya kuanza kumlaumu Mheshimiwa kwa kupunguza teuzi zao waanze kwanza kumuuliza Mwenyezi Mungu ilikuwaje akaanza kwanza kumuumba Mwanaume halafu wao alifanya kuwafikiria tu baadae ndipo akawaumba?

Vitu vingine hata havihitaji kuwa na PhD kuvijua sana bali unatakiwa tu utumie " common sense " na bahati nzuri ninachokiwasilisha hapa kipo supported hata katika different divinity literature hivyo basi ukininunia Mimi kwa hiki nilichokiandika hapa jua moja kwa moja kuwa umeshatenda dhambi.

Halafu nitoe RAI tu kuwa muwe mnajitahidi kuvisoma mara kwa mara hivyo Vitabu vya DINI na siyo tu kuviweka majumbani mwenu kama " mapambo ". Maarifa yote haya yanapatikana humo.

Jipangeni upya HAPA KAZI TU!
 
Sipingi equal treatment kati ya mwanamke na mwanaume ila ninapinga kwa raisi kutumia Gender kama credential ya mtu kupata kazi fulani!
Nahizana ya kusema 50/50 ni yaajabu kwasababu huwezi chagua mtu kisa mwanamke afu uwache mwanaue mwenye uwezo na sifa wakufanya kazi!!
Nazaidi, inaenda tofauti na principle ya usawa ambayo wanajaribu kutetea.
Iweje mwanaume awe na credentials nyingi na nzuri zidi ya mwanamke afu eti kisa mwanamke tu achaguliwe. Hiyo sio unequal treatment ambayo hiyo taasisi inajaribu kupigania.
 
Ni kweli usemavyo kuwa Mungu alimuumba Adam( mume) kuwa kiongozi na mkutoa Hawa ubavuni mwa Adam kuwa msaidizi wake,baada ya kugundua upweke wa Adam.

Na hicho ndicho wanachokisema TGNP,ya kwamba miongoni mwa viongozi wateule wa Mh.JPM,na wanawake pia wawemo ili kufanya kazi ya usaidizi kama alivyofanya hawa katika kutoa maamuzi mbalimbali ya kiongozi katika Serikali take,kama alivyo yeye na makamu wake na hawana maana ya kupoka madaraka yote toka kwa wanaume Bali kufanya mseto baina ya jinsia hizo mbili.

Hoja nyingine ni kwamba Tanzania sio kisiwa au parokia ambapo inaweza kwenda kwa utaratibu wake/ sheria zake zenyewe kama nilivyosema kwenye maandiko ya awali,kwa kiasi Fulani IPO haja/ na imekuwa ikifanya hivyo ikibidi kwa kusaini mikataba mbalimbali ya kikanda na kimataifa ikiwemo ile kutambua haki ya kupewa usawa katika nafasi za uongozi kwa akina mama ambapo Mara ya mwisho maamuzi hayo yalipitishwa na kika o kilichofanyika BEIJING. Na Yale malengo ya melenia ambayo nimekwisha ya Taja.

Tumeona nchi ya Rwanda kwa Mh.Kageme sasa akionekana kuwa rafiki wa karibu wa rais wetu JPM,ndio nchi pekee katika Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla kufikia malengo ya kimelia kwa kuteua akina mama katika ngazi za juu kwa 50%/50%.

Na kama hoja ni Elimu na Uwezo wa kuongoza ili kwenda na kasi ya Mh.TGNP wanasema wapo vizuri/ tayari kumsaidia rais kumpatia /kumuonesha akina mama hao.

Mwisho,ila sio kwa umuhimu sasa dunia inashuhudia mabadiliko makali katika nafasi za kiutawala na uongozi kwa kushikwa na akina mama huku wa kivunja rekodi ya uongozi uliotukuka,akiwemo akina Angel Michael(Ujerumani),Helen Sarifu Jonson(Liberia),Nchi za Afrika ya kati,nanyinginezo nyingi

Sio tu kwenye sekta ya siasa Bali hata kwenye taasi za dini tumeshuhudia viongozi wanawake katika makanisa ya Anglican paka kufikia kiwango cha ukasisi,haya ni mabadiliko makubwa yanayoonesha wanawake wanaweza,kama alivyo kuwa mama wa Yesu Kristo,Mariam

Bado historia ya dunia inatufanya turudi nyuma paka kwenye enzi za dola za kifalme ili tuweze kujifunza na kujua umuhimu wa wanawake katika nafasi za uongozi.Wapo wafalme wengi wa like waliweza kuongoza vizuri na kuzifikisha jamii zao katika ustawi mkubwa.

Tusirudi kanani,kama kweli yanayolalamikiwa na TGNP ni sahihi ni swala kuyafanyia kazi maoni yao,dunia inahitaji mabadiliko na ndio maana ikatoka kwenye zama za UJINGA,ujinga uliowafanya wanaume kuhodhi kila kitu paka haki ya kupiga kura( enzi ya dola ya rumi,ulaya kabla ya migomo ya wafanyakazi na nchi za kiarabu)

Hapa Kazi Tu haina tafsiri ya kuwatenga,kuwabagua au kutowashirikisha watu katika kutekeleza majukumu yao na kupewa fursa ya kutoa mchango katika serikali.Umeitafsiri Vibaya na Wala rais wetu Hakumanisha hivyo.

TUJENGE HOJA ZA KULIJENGA TAIFA LETU,NA TUJENGE UTAMADUNI WA KUSHAURIANA KUREKEBISHA TOFAUTI ZETU ZILIZOPO KATIKA JAMII KWA UWAZI KAMA WALIVYO FANYA TGNP BADALA YA KUBEBA MAMBI KATIKA VIFUA VYETU AMBAVYO MWISHOWE VINAWEZA KULETA ATHARI KWA TAIFA.
 
Sipingi equal treatment kati ya mwanamke na mwanaume ila ninapinga kwa raisi kutumia Gender kama credential ya mtu kupata kazi fulani!
Nahizana ya kusema 50/50 ni yaajabu kwasababu huwezi chagua mtu kisa mwanamke afu uwache mwanaue mwenye uwezo na sifa wakufanya kazi!!
Nazaidi, inaenda tofauti na principle ya usawa ambayo wanajaribu kutetea.
Iweje mwanaume awe na credentials nyingi na nzuri zidi ya mwanamke afu eti kisa mwanamke tu achaguliwe. Hiyo sio unequal treatment ambayo hiyo taasisi inajaribu kupigania.
Wanachokidai TGNP ni kwamba wapo akina mama wangefaa au wanafaa kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi kutoka kapu la uteule wa Mh.Raid.

Sifa zote wanazo wamesoma na kupata elimu/ujuzi na uzoefu wa Kutosha.
 
Mimi tokea Mwenyezi Mungu alivyonyofoa sehemu yetu ya mbavuni na kuwaumba akina " Hawa " wala sishangai wakiwa wanakosa nafasi sehemu mbalimbali kwani hata Mwenyezi Mungu alitambua kuwa wao daima watakuwa ni Wasaidizi wetu tu hadi dunia iyeyuke na hata kama tukiamua kuwateua basi tutafanya hivyo kama sehemu ya kuwafurahisha ila daima Wanaume tutabaki kuwa Watawala na Viongozi wao watake wasitake au wanune wawezavyo.

Hawa TGNP kabla ya kuanza kumlaumu Mheshimiwa kwa kupunguza teuzi zao waanze kwanza kumuuliza Mwenyezi Mungu ilikuwaje akaanza kwanza kumuumba Mwanaume halafu wao alifanya kuwafikiria tu baadae ndipo akawaumba?

Vitu vingine hata havihitaji kuwa na PhD kuvijua sana bali unatakiwa tu utumie " common sense " na bahati nzuri ninachokiwasilisha hapa kipo supported hata katika different divinity literature hivyo basi ukininunia Mimi kwa hiki nilichokiandika hapa jua moja kwa moja kuwa umeshatenda dhambi.

Halafu nitoe RAI tu kuwa muwe mnajitahidi kuvisoma mara kwa mara hivyo Vitabu vya DINI na siyo tu kuviweka majumbani mwenu kama " mapambo ". Maarifa yote haya yanapatikana humo.

Jipangeni upya HAPA KAZI TU!
Kweli wewe ndiye Ng'ombe Mayai na Mungu kawalaani kwa kuwanyima akili na maarifa..
 
Kama reference ya haki sawa ni uongozi wa jk, basi haina haja ya kuendelea kugawa madaraka kwa wanawake maana sote tulishuhudia utendaji wa serikali kudorola, ni bora wawe wacha sana ambao rais anaona wanafaa kufanya naye kazi na ikaenda mbele, haya mambo ya kuremba mwandiko yatatukost, tunataka watu imara si kwa kigezo cha kuwa mwanamke wala mwanaume
 
Wanachokidai TGNP ni kwamba wapo akina mama wangefaa au wanafaa kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi kutoka kapu la uteule wa Mh.Raid.

Sifa zote wanazo wamesoma na kupata elimu/ujuzi na uzoefu wa Kutosha.
Bado ana muda mrefu TGNP wampe muda, wameanza TGNP watakuja wa kusini, watakuja wenye dini kisha wasio na dini tutafika kweli?
 
Mwishowe TGNP wafunguka na kumshauri Rais JPM,kuzingatia jinsia kama inavyoelekezwa/shauriwa kwenye mikataba mbalimbali ya kikanda na kimataifa pindi afanyapo uteuzi wa viongozi mbalimbali.

Kwa kusisitiza hilo TGNP walifika mbali zaidi kwa kuchambua idadi ya kina mama walioteuliwa katika ngazi mbali mbali za uongozi ikiwemo zile za Mawaziri,Manaibu mawaziri,Makatibu wakuu na manaibu makatibu wakuu.Wakuu wa mikoa,wilaya na wakurugenzi halikadhalika akina mama walioteuliwa ni wa chache mno kuliko wale wa serikali ya awamu ya NNE chini ya Rais Kikwete.

Hawakuishia hapo skins mama hao wa TGNP waliendelea kusema kwa utaratibu huo itakuwa ni vigumu kufikia malengo ya kimelenia ya umoja wa Kimataifa paka kufikia mwaka 2025 kuwa uwakilishi wa 50% kwa 50% kati ya me na ke za uwakilishi kwa ngazi za juu za serikali.

Kisha wakasema Mh.Rais asihofu kuwateua akina mama kwani wapo wanaofaa kwa ujuzi na kuongoza na kwenda na kasi anayotaka Mh.

My Take: 1 nikuwapongeza TGNP kwa kutoa yao ya moyoni kwa kumshauri rais angalie (women impowerment & gender balance) nafasi na umuhimu ya kuwashirikisha wanawake katika uongozi.

02:Lakini pia nikufungua njia kwa makundi mengine ya kijamii yanayo hisi kwa njia moja au nyingine nao wamegwasa kama wana mtandao huo wa TGNP waweze kusema na kupaza sauti zao kueleza kilio chao kwa Mh.JPM,kwani Rais wetu na serikali yake ni serikali ya watu na na nisikivu

03: Kupitia ushauri huo Rais JPM asikie kilio hicho cha TGNP kama kina mantiki au kimebeba chembechembe za ukweli na kinatija afanyie kazi.
04: Kama hivyo ndivyo yanayosemwa na TGNP IPO haja ya Mh.JPM,kipenzi wetu kuangalia upya staili ya UTEUZI wake ili ibebe SURA ya kitaifa Kwa kuingiza / kuhusisha makundi yote makubwa na muhimu katika jamii kwa uwiano sahihi wa uwakilishi( ikiwemo makundi ya akina mama,vijana,wazee, na uwakilishi kwa IMANI ZAO).

Kufanya hivyo kutapunguza Malalamiko kutoka makundi husika,kutaleta upendo na kujenga/ kuimarisha zaidi mshikamano wa kitaifa,kutoa fursa sawa wa kuchangia Mawazo kutoka makundi hayo kwa serikali yao na mwisho kutoa fursa za ajira kwa makundi yote ya kijamii yanayounda nchi.

Mwisho,manunguniko kama hayo kama yana ukweli huweza kulibomoa Taifa.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Wakati wa kubebanabebana umepitwa na wakati kama ikionekana wanaochapa kazi au wenye sifa ni wanaume wapewe pasipo kutoa upendeleo
 
Kama reference ya haki sawa ni uongozi wa jk, basi haina haja ya kuendelea kugawa madaraka kwa wanawake maana sote tulishuhudia utendaji wa serikali kudorola, ni bora wawe wacha sana ambao rais anaona wanafaa kufanya naye kazi na ikaenda mbele, haya mambo ya kuremba mwandiko yatatukost, tunataka watu imara si kwa kigezo cha kuwa mwanamke wala mwanaume
Hatumanishi kuusifia utawala wa JK na kuuponda ule JPM katika swala hili Bali TGNP wametumia kama nukta mrejeo katika kujenga hoja zao lakini pia kuweka sawa hoja kwa mtazamo wa kisheria na mikataba ya kimataifa.

Hapo swala la uteuzi wa akina mama ni ajenda/hoja nyigine na uwajibikaji ni ishu nyingine usichanganyi mambo.Jenga hoja Je kinachosemwa na TGNP ni sahihi au sio sahihi?
 
Wanachokisema ni sahihi mkuu lakini kipi bora, tuweke wanawake ili kutimiza adhima za kisheria na mikataba ya kimataifa ilihali utendaji wao hauridhishi japo sio wote, hebu toa maoni yako wewe ukizingatia kuwa tunahitaji watendaji wenye uwezo wa kutenda kwa mda husika
 
Samia Suluhu aliwahadaa wanawake kuwa atalisimamia hili LA ku-balance gender kwenye teuzi zote kutoka Ikulu.
 
Wanachokisema ni sahihi mkuu lakini kipi bora, tuweke wanawake ili kutimiza adhima za kisheria na mikataba ya kimataifa ilihali utendaji wao hauridhishi japo sio wote, hebu toa maoni yako wewe ukizingatia kuwa tunahitaji watendaji wenye uwezo wa kutenda kwa mda husika
Hapo umenena ofkoz hachaguliwi kiongozi kwa sababu ya jinsia yake pekee ,ila sifa stahiki ikiwemo elimu/ujuzi,uchapakazi,na rekodi yake katika Utumishi wa umma na jamii kwa ujumla,

Wapo wanawake/wanaume wanaofaa na pia wasiofaa kwa upande wangu mm Rais afanyie kazi maoni yao huku akiendelea kutafiti/ kuibua majembe mengine kama akina Kairuki afanye nao kazi awamu/uteuzi ujao.
 
Hatuwezi ku-maintain equity kama wahusika hawana sifa za kujaza nafasi husika. Binafsi Niko against gender equality hasa kwa kumbeba mtu kwa sababu tu eti ni mwanamke. Nchi inahitaji zaidi ya gender ballance kufikia malengo ya kukuza uchumi
 
Hapo umenena ofkoz hachaguliwi kiongozi kwa sababu ya jinsia yake pekee ,ila sifa stahiki ikiwemo elimu/ujuzi,uchapakazi,na rekodi yake katika Utumishi wa umma na jamii kwa ujumla,

Wapo wanawake/wanaume wanaofaa na pia wasiofaa kwa upande wangu mm Rais afanyie kazi maoni yao huku akiendelea kutafiti/ kuibua majembe mengine kama akina Kairuki afanye nao kazi awamu/uteuzi ujao.
Yeah itakaa poa sana
 
Back
Top Bottom