TGNP<TAMWA<et al Asilimia 50/50 Bungeni bila Mgombea Binafsi ni Uwendawazimu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TGNP<TAMWA<et al Asilimia 50/50 Bungeni bila Mgombea Binafsi ni Uwendawazimu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Thomas David, Jun 29, 2010.

 1. T

  Thomas David Member

  #1
  Jun 29, 2010
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Let me be too hard on these friends of mine today (TGNP,TAMWA et al)

  Hata kama leo mtapewa 50% ya uwakilishi bungeni na huo upendeleo kwa asilimia kubwa lazima utoke CCM (iwe kwa viti maalum au kuteuliwa) sidhani kama utaleta mabadiliko yeyote.

  Kwanini?

  Hamtaweza kutetea maslahi ya taifa.Uhuru wenu (wanawake wenye nia-aspirants) ulishaporwa hata kabla ya kuingia bungeni.

  Bila shaka mnataka kuingia mjengoni kuganga njaa!

  Ni masikitiko makubwa, hata baada ya mahakama ya rufaa kukimbia wajibu wake wa kulinda haki za msingi za raia wa nchi hii (Kuacha hukumu ya mbuzi kwa chui au mbwa mwitu au fisi) na kusema jambo lile ni la kisiasa (mimi sijui la kisheria ni lipi-Mahakama ya rufaa inapaswa kutupa jibu) sijaona juhudi zozote kutoka kwenye civil society kulipigia hili kelele ukiachana na tamko la LHRC.

  CSO's mko wapi?

  TGNP,TAMWA kama hili la mgombea binafsi hamtalisemea na mnataka asilimia 50/50 basi mmepoteza mwelekeo na hakuna tofauti na waganga njaa wengine ambao tunawafahamu na matangazo kwenye televisheni yanayolipiwa na fedha za walipa kodi wa nchi za kigeni basi mwazichezea bure bila hata matokeo ya maana na ole wenu...

  Oneni aibu na fungueni vinywa vyenu na mpaze sauti zenu kupita fikra na mikakati ya mwovu ambaye kila kukicha anapanga kila hila kupora haki za mwananchi wa Tanzania ambaye bado yuko kizani  Macho yetu yapo kwenu na twapenda kuona wanawake waingie bungeni kwa kugombea kupitia mgombea binafsi na wawe na uhuru wa kusema na kutetea maslahi ya taifa bila aibu na hiana ya aina yeyote.


  Anne Kilango Malecela ni mpiganaji lakini uhuru wake ulishanyakuliwa ndio maana hata mwisho alinywea kabisa na heri asingethubutu kutuhadaa kama alivyofanya. Huzuni na masikitiko yetu na yawe juu yake milele.  Hivyo hatutaki akina Anne Kilango Malecela waingie bungeni kwani hakuna lolote ambalo watatuletea zaidi ya kelele ambazo mwisho wake twaufahamu sisi sote.


  Na basi mtoe vichwa vyenu nje ya wingu hilo nene na angalieni mbele nini kinatakikana kufanyika kuwakomboa wanawako ambao mnawapigania kiume.


  Kama TAMWA na TGNP wana malengo ya kutuletea akina Anne Kilango Malecela na basi washindwe na kulegea kabisa.

  Nawasilisha
   
 2. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wanawake wanapojidhalilisha kwa kutaka mambo ya upendeleo wanatia kichefuchefu kwa kweli. Wanawake wana tatizo gani hasa hata wasiweze kuwashinda wanaume ambao wengi wao ni mabwege tu kushinda wanawake? Ukitaka kuufahamu 'ubwege' wa wanaume angalia majumbani mwetu, kazi zote zinazohusu familia anaachiwa mwanamke na anazifanya kwa utimilifu wa hali ya juu kabisa. Asilimia 50 bungeni haitoshi kabisa bora wanawake ku-aspire kuwa na asilimia 75. Lakini wachujwe kikamilifu watu kama akina Sofia Simba wasipewe nafasi!
   
 3. m

  mob JF-Expert Member

  #3
  Jun 30, 2010
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,027
  Likes Received: 510
  Trophy Points: 280
  msiwe watu wa mapokeo kila siku.kaaeni chini na kufikira mnataka asilimia hamsini kwa hamsni ili mfanye nini?kusiwe na participation what we need is contributions ok mathalani tumekuwa watu wa mapokeo in such a way tumekuwa wapumbavu.wazungu walikuja na ishu kuwa ndoa za mitara hazifai tukakubali then sasa wanakuna na mambo ya ushoga tunakubali.kaeni chini na kutafakari .Kimsingi mimi nawajua sana hao TGNP hawana lolote zaidi ya kelele.tuwe na msimamo na sio kuburuzwa every day.
   
Loading...