Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,391
- 39,484
1. Ukiulizwa wimbo wa mapenzi unaoupenda sana unasema "Mv. Mapenzi meli ya wapendanao"
2. Ukiambiwa uchague wimbo wa kusindikiza salamu kwa yule umpendaye unasema "Karolina" yeah.. ule wa "siku ulipoondoka ewe Karolina"..
3. Ukiambiwa ni mwanasoka gani wa Tanzania ambaye ni nyota wa zama zote.. bila kusita unasema "Gibson Sembuli"...
4. Ukiulizwa na chombo gani cha kielektroniki ambacho unatumia kusikiliza muziki kila uendako na kinatumia betri kwa haraka unasema "Radio ya National Bendi 4"!
5. Ni mcheza filamu gani unayemhusudu sana kupita wote. Unafikiri mara moja na kusema "Amita Bachichani".. na anayefuatia unasema "Govinda"
6. Ukiulizwa filamu ya mapenzi ambayo unaikumbuka sana unasema "Disco Dancer" hasa pale pa gitaa la umeme!
7. Ukiulizwa kuhusu mwanamuziki mahiri kabisa kutokea katika Tanzania ambaye amefariki kijana bila kuchelewa unamkumbuka "Nico Zengekala"
8. Ukiulizwa ukumbi ambao ulikuwa unapenda kujimwaga kila weekend huchelewi kusema ule wa pale Ubungo (nasikia uligeuzwa Kanisa)
9. Ukiulizwa ni bendi gani unaipenda unasema "Juwata Jazz - Baba ya Muziki"
10 Ukiulizwa ni kikatuni gani ambacho unakumbuka hadi leo kwa tabasamu... unasema ile sherehe aliyoandaa Kipepe Bush na kuwawekea TV za Bush kina Lodi Lofa..