TGIF: The man we called "Yeke Yeke"

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,987
Karibu sehemu nyingi enzi ile za miaka ya themanini kulikuwa na jirani, rafiki, mtu fulani ambaye alibatizwa jina la "yeke yeke". So far, nawakumbuka wawili. Mmoja wao alikuwa anavaa kikoti cha rangi ya kijani kibichi na wimbo wa "yeke yeke" was like Gods gift to humanity! Na mwingine alikuwa ni mtumishi wa nyumbani ambaye kichwa chake kilikuwa kikitingishika kama hakina ubongo kila akisikia wimbo wa "yeke yeke".

Baada ya muda majina yao ya asili wengi tulishayasahau na tuliwajua kwa jina hilo la "yeke Yeke".

Unamkumbuka mtu yeyote aliyepewa jina la "yeke yeke" and the story behind it au aliyepewa jina fulani la ajabu kutokana na kitu fulani katika maisha na stori gani unakumbuka juu yake?
 
Nakumbuka baada ya ile njaa ya mwaka '85 kule Ethiopia watu wenye miili myembamba walianza kuitwa "Ethiopia". Kuna mchezaji mmoja wa mpira alikuwa anachezea timu ya Wica pale Mwenge kwa wachonga vinyago....huyu jamaa walimbatiza jina la "Ethiopia" kwa sababu alikuwa mwembamba halafu mwenye chenga na mbio kichizi. Akikutoka ilikuwa humkamati.....halafu ukija kustuka....goli.....
 
Dada yangu mmoja yeye alijiita mwenyewe "Vai" (Vailet) Masantula. Ila kama ni kubatizwa majina basi Waalimu huwa wanayapata sana hasa kule secondary. Nawakumbuka waalimu kama "mama Nyungu ya Mawe" na mama wa Kihaya alikuwa Nyungu kweli, Bunsen Burner??, nk
 
Namkumbuka mtu jamaa mmoja alibatizwa madenge maana ukimuona kwanza kabla ya vituko utasema waliochora katuni ya madenge walichukua picha yake, subiri sasa aanze vituko the madenge haoni ndani, wakati huo sani ilikuwa inatoka mara moja kila baada ya miezi mitatu na inasubiriwa kama nini ili kuangalia ,madenge ametoa kisa gani, the jamaa anafanana na madenge na anavituko kama madenge, ilibidi akubali jina hilo.
 
Kama kumbukumbu zangu ni nzuri, Minziro, yaani Fred Felix alipewa jina hilo kutokana kijiji cha minziro kutajwatajwa sana mwanzoni vita ya kagera
 
kuna mtoto mitaani kwetu anaitwa "kiroba" kwajaili ya ufupi hata umri wake haujulikani ... ila sauti yake imeshaanza ku break ... jina halisi hatulijui kabisa
 
Babu umenikumbusha mbali weye.....!
Mimi nakumbuka nilipachikwa jina la ...JOJO... kutokana na zile chewing gum za miaka ya 80 kiasi kwamba hata VISHADA vikipepe sana kutokana na upepe tulisema vinakwenda JOJO.
Lakini mimi ilikua kutokana na wembamba wangu wenzanu walizani nigepeperushwa na upepe
 
kuna kaka mmoja hapa anaitwa timberland kwaajili nguo zake, hata jina lake simjui, hadi mkewe anaitwa mama timberland.
Hebu fikiria, majirani wote hatumjui jina lake, manake hadi kadi inaandikwa jina hilo au baba nanihii..
 
Lakini naamini haya majina mengi yanaendana na tabia zenyewe. Nakumbuka Nyerere aliitwa "Mchonga" na "Haambiliki" ... halafu kama kuna waliitwa zaidi kutokana na majina ya vikatuni kama hao kina "Lodi Lofa", Pimbi n.k
 
Usimsahau "ndumila" au ndumi la kuwili.
 
mwnkjj mchokozi weye huachi.....?, miye memory zangu fupi zinanirudisha katika tukio moja miezi kadhaa nyuma, ambapo mweshimiwa waziri mstaafu mmoja alipobandikwa jina la vijisenti kutokana na kauli yake, is this irrelevant?
 
Mntangazaji Abdallah Mlawa alijulikana Kenya kama Mr. KIJARUBA, he heeeheheeeee Akinamama pale nawaona ..... heheheeeeeee
 
...Unamkumbuka center back wa Simba miaka ya 80 Athuman Maulid??? Alipachikwa jina la Big Man na mtangazaji mmoja wa KBC Kenya wakati wa Challenge Cup...Jamaa alikuwa bonge la Mtu........
 
Karibu sehemu nyingi enzi ile za miaka ya themanini kulikuwa na jirani, rafiki, mtu fulani ambaye alibatizwa jina la ...

Unamkumbuka mtu yeyote aliyepewa jina and the story behind it au aliyepewa jina fulani la ajabu kutokana na kitu fulani katika maisha na stori gani unakumbuka juu yake?

...miaka hiyo late 70's na 80's namkumbukia mgonjwa mmoja wa akili maeneo ya dengu beach (Ocean Road-Dsm), alikuwa anajulikana kwa jina la 'MAPISTO' kutokana na ishara ya vidole kila ukimwita jina hilo.

Huenda keshafariki maskini yule mzee (RIP), miaka ile wagonjwa wa akili walikuwa wachache mno mitaani, na inasimuliwa kuwa "MAPISTO" enzi zake alikuwa msomi na mwenye familia nzuri tu!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom