TGIF; kila la heri maharusi wa kesho...! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TGIF; kila la heri maharusi wa kesho...!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mbu, May 22, 2009.

 1. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...hivi, kwanini wanakamati wanakuwa wanoko sana

  Bwana harusi anataka mchango kidogo angalau alipie kodi ya chumba kwa miezi sita, wao wanashikilia hiyo ni shauri yake,... eti wanataka fungu lililobakia litumike kuvunjia kamati!

  Halafu utakuta pengine wala huyo bw Harusi hakutaka makuu ya sherehe kubwa, msafara wa magari, tarumbeta wala rusha roho! Personally, nimeshuhudia kwa Bw. mdogo mmoja, ndugu zake walimlazimisha afanye bonge la harusi japo jamaa ndio hivyo tena, (KCC).

  Mbaya zaidi ni pale walipomlazimisha dogo akope 3* his salary, eti akiwa kama mhusika lazima achangie donge nono! ...Kwani lazima sherehe mpaka mtaani washikishwe adabu jamani?

  Haipendezi badala ya maharusi kufurahia fungate, unamuona bwana harusi kawa mdooogo kwa madeni.

  Wanakamati, msiwape adhabu waoaji!
   
 2. M

  Mtu wa Kawaida JF-Expert Member

  #2
  May 23, 2009
  Joined: May 2, 2008
  Messages: 217
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Hili ni tatizo la watanzania kutaka makuu. Mie nadhani umefika wakati tukafikiria mara mbili mbili tunapoamua kuwa na mwenza katika sehemu iliyobaki ya maisha yako. Tubaliane na hali zetu halisi na sio kuburuzwa na jamii inayotuzunguka.Tusifanye mambo kwa kuiga. Kama wanadoa wakijikusanya kwa uwezo wao pasipo shinikizo sidhani kama kuna watu/wanakamati watakuwa na wasemaji wakuu katika nguvu ya hao wanandoa.
  Vile vile wanandoa wanatakiwa pia wasiwape nafasi wanakamati mamlaka makubwa katika maamuzi yao ya shughuli nzima ya harusi.
   
 3. Kaniki1974

  Kaniki1974 JF-Expert Member

  #3
  May 23, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 352
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Eti una kuta mtu wa KCC ana simu ya laki tatu jamani! Too much money, isn't it? Consumption pattern yetu waTZ kiboko!
   
 4. Outlier

  Outlier JF-Expert Member

  #4
  May 23, 2009
  Joined: Dec 28, 2008
  Messages: 325
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kama usipotaka makuu hautachangisha watu. Na hata kama ukichangisha, uamuzi wa matarumbeta, sijui msururu wa magari ni juu yako unless uwe **** kichizi. Utalazimishwaje kufanya kitu usichotaka?
  Pesa zikishachangwa hazikuhusu na zinahusu sherehe na yanayofuata kwa hiyo sahihi kamati kuamua.
  Na hili la kulazimishwa kukopa? Utakuwa na akili au matope (ukikubali).

  Huko KCC ndio wapi? Na simu ya laki tatu; mi naona sio ajabu, ni masuala ya priorities tu! Kama wewe una-care kujenga nyumba au kununua gari, mwenzako raha yake kuwa na simu ya "ghali" - so, what's up? MUB!
   
 5. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #5
  May 23, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  Mkuu Outlier
  Kima Cha Chini (KCC), siyo eneo bali kiashirio kuwa mtu uwezo wako wa chini ila unataka mambo makubwa kwa kujionesha.

  @Mbu
  Kamati zingine hao wanakamati ni wakali maana wanabana matumizi ili waondoke na cha juu. Usishangae kuona mtu anapenda kuwa kamati lukuli mara ya ndugu, rafiki, jirani n.k. kumbe ana lake kichwani.
  Tatizo na hapo mjini watu wanataka harusi za kukata na shoka, si unajua ile' can you see me now'!! Halafu mwezi baada ya ndoa hofu za madeni juu wakati mtu unawezafanya wedding ndogo ya kukufurahisha wewe+ndugu wa karibu..
   
 6. Outlier

  Outlier JF-Expert Member

  #6
  May 23, 2009
  Joined: Dec 28, 2008
  Messages: 325
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Asante kunifahamisha; hii imeanzishwa lini, kwa kweli leo mmeniuza! lol

  Ni possibility lakini very unlikely. lol
   
 7. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #7
  May 23, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  Mwenyewe nilivyoiona hapa, nimekumbuka chuoni maana tulikuwa tunatumia sana..Sijui Mbu na Kaniki wameitoa wapi?!!..l  Kuhusu hili, you could be right siyo kila mtu anafanya hili maana katika vitu vingi kuna 'exceptional'.
   
 8. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #8
  May 23, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  hivi simu ya sh. laki tatu ni ya bei ghali???

  hao maharusi wenyewe wanaentertain mambo ya kamati, michango etc. as long as wana haki ya kuamua juu ya sherehe wanayotaka, wakiamua kuipa haki hiyo kwa kikundi cha strangers and scavengers wanaojiita kamati shauri yao.

  sioni sababu ya kumhurumia dogo ''aliyelazimishwa'' kukopa.
   
 9. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #9
  May 23, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Maisha mafupi wajameni kuleni maisha..kwa nini kuishi kwa kujibanabana? kula kitu roho inataka..!
   
 10. Kapinga

  Kapinga JF-Expert Member

  #10
  May 23, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 728
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ushangaa hiyo...nilienda kumtembelea msela mmoja kwao house girl anasimu nne (tigo, voda, zain and zantel) ndo bongo hiyo!!

  katika mambo ya harusi ndo nimechoka...mtu harusi mlioni 30! alafu bibi harusi kwenye account ana laki 7 na bwana harusi laki nane (na madeni juu)

  wangefanya harusi ya mil 15 na mil 15 agawane na mkewe wangekuwa wapi?

  tuwe makini jamani! kwa maisha ya sasa financial stability ni muhimu kuliko sherehe hizi za kiasara..watu hao hao uliwachangisha ukiwa na shida utapewa ratiba mpaka uchoke!
   
 11. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #11
  May 23, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Life is about having good time mkuu. If hao jamaa wapo comfortable na hiyo ishu mi sioni hatari wala nini naona shega tu. Ukizilea hizi shida utakufa kwa mawazo siku si zako.
   
 12. Kapinga

  Kapinga JF-Expert Member

  #12
  May 23, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 728
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  I hope unatania mkuu!!
   
 13. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #13
  May 23, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Sitanii mkuu.

  Maybe sipo sahihi sana lakini katu sitoishi kimaskini na kukaribisha misery ktk maisha yangu. Kama nna pesa lazima nifanye kitu roho inataka ili mradi tu vinalika. Ktk maisha ya binadamu ni vyema ku-make space for good time. Vitu kama sherehe sio vya kubanabana kwa sababu ni kama special case they don't happen many times.

  Matatizo yapo na yataendelea kuwepo whether unakula happy au hauli.
   
 14. Kapinga

  Kapinga JF-Expert Member

  #14
  May 23, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 728
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  I guess we all have different goals in life...mine is financial stability...si sawa na vijana wengi bongo wanapush range 4.6 wakati hawajajenga nyumba...ndo mambo ya kitu roho inapenda..mwisho wake sio mzuri.

  Ukiangalia thread utaona jamaa analalamika hizi kamati na expenses za harusi..tuwe tunatoa ushauri wa ukweli jamani...im not against weddings but they should be within your means..sio harusi movenpick unaishi uswazi. Tuanze kuona mbali.
   
 15. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #15
  May 23, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  kuna haruc nilihudhuria last wik, ilikuwa ni ya hali ya juu kupitiliza, baada ya haruc kamati ilibakiwa na kama 3ml hivi,wanakamati waliitana kesho yake na baadhi ya watu wa karibu wa maharuc nikiwepo na mie ili waweze kujipongeza kwa kufanya kitu "balaa" mjini.....tulikunywa/kula na zilizobakia kamati waligawana pasu-pasu......
   
 16. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #16
  May 23, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...duh, mbona umemaka sana bro... halafu hapo uliposema pesa zikichangishwa hazikuhusu na ni sahihi kamati kuamua si ndio kulazimishana kwenyewe huko?
   
 17. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #17
  May 23, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...hiyo kauli kwamba harusi haijirudii ndio inayowafanya wanakamati kuwabana mbavu kina KCC! ...inatia huruma kwakweli! Ukiweka wanakamati wenye ubavu mdogo, michango nayo itasua sua hivyo hivyo..., ukiwapa kamati wenye nacho shughuli inakuwa siyo yako tena,...balaaa!
   
 18. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #18
  May 23, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...mnaona sasa, kwanini hizo 3m wasipewe walengwa ambao ndio hao maharusi? wanakamati waliogawana pesa wamevurunda sana!
   
 19. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #19
  May 25, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0


  liisemekana kwamba bila wao wacngeweza kufanya haruc kama ile so ni lazima wajipongeze kwa kazi nzito...
   
 20. M

  Mama Joe JF-Expert Member

  #20
  May 25, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,507
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Mtu mwenye akili na utashi utaweka priority mbele, hat kwa hela ndogo na marafiki wa kweli waweza kuwa na tafrija nzuri tu yenye kumbukumbu ya kudumu.
  Sio mtu unajua uwezo wako mdogo bado unataka watu 1000, ukumbi movenpick etc ndo kamati inaundwa ikutengenezee hiyo ndoto! - utalazimishwa kutoa at least kiasi cha kuanzia usifiri yote unachangiwa!
  In life you need not suffer for the sake of FUTURE but there need to be a limit on your expenses while you are young and healthy and yearning something! Sio unasubiri retiring time 55 or 60 years ndo unaanza kuamka kutafuta site na watoto uliolea kifahari wamekulundikia vijukuu kibao maana nao pamoja na elimu hawajazoea maumivu hivyo wanakurudishia watoto ili waweze kuponda raha kwenye 2 rooms walizopanga maana wameona priority ni Rav 4 na benz "mama mwenye nyumba hataki family" Unajua watu wa namna hii wanaishia wapi???? wanarudi kijijini kwao kabisa na kulima hawezi yaani ni mzigo na aibu!
  Take care, be happy today but remember there is sunset, and next day.
   
Loading...