TGIF: Amri 10 za Serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TGIF: Amri 10 za Serikali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Apr 17, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Apr 17, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Nilikuwa shambani nalima jioni ya Alhamisi karibu na kisiwa cha Belle Isle nje ya Jiji la Detroit. Mara nikasikia sauti iliyoniita na kusema ‘Mwanakijiji!' nikaitika ‘Naam!". Ikaniambia "Sogea hapa". Basi pole pole nikaelekea iliko sauti hiyo. Nilipokaribia ikaniamuru nisimame na nisiendelee mbele zaidi. Nikaona upande wa kushoto kwangu kichaka kikiwaka moto; kichaka kile kilikuwa kinateketea taratibu na matawi yake kugeuka makaa na majivu. Chini ya Kichaka kile pameandikwa Tanzania. Nikaogopa na kutetemeka. Sauti ile ikaniamuru "Usiogope! Vaa Viatu vyako, maana hapo unaposimama pana ufisadi".

  Basi nikafanya hima kuvaa viatu vyangu na kukusanya matambara yangu ya shambani nikisubiri agizo jingine. Sauti ile ikaniambia "Tazama nakupa amri zangu, amri ambazo utawapelekea wana wa Tanzania ili wazishike na kuzifuata." Mara sauti kama ya ngurumo ya radi ikasikika na mwanga mkali kutoka angani ukaangaza na kunipofusha macho yangu. Nilipoyafungua nilijikuta nimevaa miwani myeusi ya jua na mbele yangu kuna laptop iliyoshikwa na mikono ya mtu asiyeonekana.

  Nikaona na tazama, maandishi makubwa ya mtindo wa "Old German" yakatokea na sauti ikasema: " Zishike moyoni na uwapelekee Watanzania amri hizi!". Hizi ndiyo amri 10 za serikali ya Tanzania

  Amri ya Kwanza: Mimi ndiyo serikali yenu ya Chama Cha Mapinduzi, hakuna serikali nyingine.

  Amri ya Pili: Usilitaje bure jina la serikali yako ya Chama cha Mapinduzi, hasa kama wewe ni mpinzani au hauna chama. Kuitaja taja serikali kwa kila tatizo kutakuletea matatizo kwani serikali hii humfuatilia mtu na familia yake hadi kizazi cha nne cha Wanaopandikiza mbegu za chuki. Kama huamini waulize kina Kambona.

  Amri ya Tatu: Ishike na kuikumbuka siku ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi, ukiisahau Chama kitakukumbusha kila ifikapo Februari.

  Amri ya Nne: Waheshimu viongozi wa Chama cha Mapinduzi na serikali yake pamoja na watoto wa watoto wao ili upate mafanikio katika biashara zako na siku zako za kunufaika na ufisadi ziongezeke.

  Amri ya Tano: Usinikosoe

  Amri ya Sita: Usiibe mali za CCM

  Amri ya Saba: Usiseme nasema Uongo.

  Amri ya Nane: Usizitamani sera ambazo si zako wala mali zozote za CCM.

  Amri ya Tisa: Usiwashuhudie watu juu ya udhaifu wa viongozi wao na kuwafumbua macho juu yangu.

  Amri ya Kumi: Usisimame kutetea mali za nchi yako na wala usiwe na kimbelembele cha kujifanya wewe ni mwanaharakati wa mabadiliko. Nitakumaliza.


  Ndipo miguu yangu ikanyong'onyea kwa hofu. Ndipo sauti ile ikaniagiza kupeleka ujumbe wa Unabii wake kwa njia ya makala. "Ninakutuma uwaandikie maneno nitakayokupa kwani wakati umefika wananchi wasikie NENO kutoka kwa serikali yao!" Akanipa maneno ambayo nimeyaweka moyoni hadi wiki ijayo kwenye mojawapo ya makala zangu. Yatakuwa ni maneno ambayo yatawatikisa watawala na yatawashtua watawaliwa.

  Kuna wazee niliowaacha kilabuni wakati naenda shamba; waliponiona narudi huku uso unatabasamu wakaambiana "huyu naye amesikia sauti". Wakasema "Amen Amen" huku wakiendelea kupokezana kombe la mbege. Kwa mbali wimbo wa "umkombhoti" wa Yvonne Chakachaka ukisikika kwa mbali.
   
 2. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #2
  Apr 17, 2009
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Tunasubiri kwa hamu mkubwa. Lakini nina mawazo nayo ni kubuni njia ambayo kwa kutumia vipaji vyenu, andishi lenu linawafikia watu wengi. Nipo kwenye mchakato once ikikamililka nitajua nini cha kufanya. Ninaongea naelimisha na saa nyingi natumi andishi lenu kutolea mifano halisi. wengi wanaelewa.

  Kule vijijini bado access ya Tanzania Daima bado ni tatizo. Mwanahalisi inafika lakini kuna wilaya moja tena nzuri sana lakini kwa bahati mbaya haipati hii fursa.
   
 3. MyTanzania

  MyTanzania Senior Member

  #3
  Apr 17, 2009
  Joined: Sep 9, 2008
  Messages: 107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Twangoja bwana Musa,tumesubiri sana miaka 400 (over 40 years of independence)
   
 4. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #4
  Apr 17, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,896
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Kweli huyo ndo Mwanakijiji... So nice. Creativity nzuri sana. Nimeipenda kweli.
   
 5. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #5
  Apr 17, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Mkuu Mwanakijiji,

  Mie nimeshakata tamaa sana na Viongozi waliopo hivi sasa na kinachoniuzi sana ni tabia y akwamba flani hawezi kuguswa kwa kuwa ni UWT au ni mtu wa karibu wa mkulu.

  Yaanii nchi inendeshwa kwa kufuata matakwa ya watu wachache.Kuna harufu ya Ubaguzi!
   
 6. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #6
  Apr 17, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Tunaweza kuamua, hata mtu mmojammoja, kama hawataki kubadilika, basi tubadilike sisi-hatimaye na wao watalazimika kubadilika kwa sababu wanachokifanya kwa kiasi fulani wanategemea msaada wetu
   
 7. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #7
  Apr 17, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mungu alipoona wanadamu hawaachi matendo yao maovu alimtuma mwanae wa pekee, akamwaga damu ikamkomboa mwanadamu. Baada ya tanzania kuliwa na mafisadi wachache na sie kupiga kelele nyingi bila mafanikio ya dhati, Damu ya ukombozi wa kiuchumi lazima imwagwe kwa ukombozi wa wengi.
   
 8. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #8
  Apr 17, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Kidumu chama cha mafisadiiiiiiiiiiiiiiiiiii!!!!!!!!!!!!!kidumuuuuuuuuuuuuuuuu!!!!!!!mileleeeeeeeeeeeeeeee!!!!! Wanaoonagere wafe....wafeeeeee!!!!!!!!!!!!!
  Zidumu fikara za mafisadiiiii........
  Ole wao.....
   
Loading...