TGIF: Aliyeandika habari hii anahitaji kufungwa!

Mi siamini serikali haiko serious na elimu na walimu wetu kiasi hiki.

  • Kwa nn kununua vitabu na kujenga nyumba za walimu mpaka pesa a BAE.
Tujiulize kwenye bajeti ya sasa ni kiasi gani kimetengwa kujenga nyumba na walimu na kununua vitabu . Yaaani mpaka pesa iliyokuwa misallocated na wala rushwa imekamatwa ndo wanakuja na sababu tamu.

Hapo ndio utashangaa na liserekali hili lisilo na msimamo !
 
Mkuu MM,

Haya masuala ya rada, kagoda, meremeta,deepgreen, IPTL, EPA, Kiwira, Downs (hatimaye Symbion), ukwapuaji wa nyumba za watanzania, safari za nje za raisi, mawaziri kukaa mahotelini kwa gharama kubwa, shule za kata, siasa za udini, kumkashifu BABA WA TAIFA, nk nk kwa ukweli wa Mungu yanaumiza sana. Kwa nini yote haya ? kwa nini angalau hayapungui kama hayawezi kwisha? tatizo hasa ni nini ? Ni CCM, ni watanzania, ni akili zetu finyu au ni kweli kama wengine wanasema tumelogwa ? Au ni mchanganyiko wa mengi ?

Tufanyeje kujinasua na maafa haya ?

Mimi bado naanimi tukipata katiba ya watu italeta mabadiliko na kutuelekeza tunakotaka.

Vile vile katiba ya watu itatuwezesha kuchukua hatua muafaka kwa wahalifu wooote na uhalifu woote huu.

Sijakata tamaa!
Ewe mwenyekheri Julius Nyerere utuombee kwa Baba aliyejuu, muweza wa yote atuokoe na waovu hawa.
 
Yaani baada ya kuandika kote wiki hii nzima bado kuna watu wanaamua kuwapotosha Watanzania kwa makusudi. Ninaamini imeandikwa na mtu wa Ikulu au Mambo ya Nje.
.
Mzee Mwanakijiji, kwanza pole kwa juhudi zako kuandika sana kuhusu issue hii. Za kutoka jikoni zimethibitisha muafaka umeishafikiwa, fedha zitarudishwa nchini kupitia UK AID kama misaada ya serikali ya Uingereza kwa Tanzania. Fedha hizi ambazo zilipangwa kurudishwa nchini kupitia Shirika lisilo la Kiserikali la Save The Children Fund, sasa zitarejeshwa nchini kupitia Shirika la DFID ambalo litazirejesha serikalini kugharimia miradi ya kiserikali ya maendeleo itakayokubaliwa na pande zote mbili na sio kutumbukizwa kwenye Busket Funding ya General Budget Support.

Mpango huo umewezekana baada ya kazi kubwa ya lobbying kwenye corridors za Wenstiminster ambayo pia umeridhiwa na wahiusika wakuu wakisuppotiwa na Mama Balozi wa UK nchini.

Game nzima itahitimishwa hivi karibuni kwa ile Lobby group kurudi tena UK kukamilisha mambo ili fedha zirudi.

Kitu kimoja naomba kuwahakikishia wanajamvi, fedha hizo zikirudi kupitia UK Aid kwa DFID, zitatumika kwa maendeleo kuikweli kweli, na hazitatumika kulipia vitafunio na kulipana posho.

Kwa bahati nzuri, Waingereza nawaelewa vizuri, wanautaratibu unaitwa 'scrach my back and I'll scratch yours' ukiona wameridhia fedha hizi zirudishwe kama msaada kupitia DFID, ambayo ni sawa na kuzirudisha serikalini, lazima wana lao jambo kama lilile lile lililopigiwa kelele sana na Barones Linda Chalker kabla hiyo 'obsolate' radar haijanunuliwa, kwani ilikubaliwa inunuliwe ili kuokoa ajira za Waingereza pale BAE, hivyo kuweka maslahi ya Waingereza mbele.

Hatua hii ya kuridhia kurejeshwa serikalini kwa mlango wa nyuma, lazima ina maslahi fulani kwa Uingereza, hivyo kinachofanyika ni Tanzania kupewa peremende ilambe kwanza ndipo kazi ifuatie. You just keep watching what next baada ya kurudishiwa kinachodaiwa ni chenji yetu, tutapigwa gundi ya mdomo kisawasawa and we can't say on anything to them!.

Pasco.
 
Ivi viongozi wetu wamerogwa na nani jamani wanatia huruma.malipo ni duniani kila siku ni selikari ndo yenye matatizo,lnabinafsishwa maliasili,madini bado sisi wananchi.kwa iyo mkukuta ni kama series(filamu)ilikuwa moja,sasa 2po pili na ya tatu mwakani...

Ndomanake hiyo ndo serikali ya magambazi inadai chenji hata haya aioni,
 
Asante sana hata mimi inanikera kuita hizo pesa kutoka BAE eti chenji wakati kama si SFO kufuatilia tungekua tumeshaibiwa yani ni kitu kibaya kufanya watu wazima wajinga,pia tusisahau fedha za EPA bil.60 zilizorudishwa na wale wezi raisi aliowaambia wazirejeshe hivi kwanini wasitajwe na kuchukuliwa hatua kwanini tunakaa kimya tu wakati watu wengine wanafanya makosa na kufugwa jela,hawa waliozirudisha hizo hela wamekua nani hadi wasikamatwe?nina hasira sana..
 
ukifuatilia mengi nchi hii utakuwa kichaa BORA MALECELA JR ANAONGELEA MAREKANI.
 
.
Mzee Mwanakijiji, kwanza pole kwa juhudi zako kuandika sana kuhusu issue hii. Za kutoka jikoni zimethibitisha muafaka umeishafikiwa, fedha zitarudishwa nchini kupitia UK AID kama misaada ya serikali ya Uingereza kwa Tanzania. Fedha hizi ambazo zilipangwa kurudishwa nchini kupitia Shirika lisilo la Kiserikali la Save The Children Fund, sasa zitarejeshwa nchini kupitia Shirika la DFID ambalo litazirejesha serikalini kugharimia miradi ya kiserikali ya maendeleo itakayokubaliwa na pande zote mbili na sio kutumbukizwa kwenye Busket Funding ya General Budget Support.

Mpango huo umewezekana baada ya kazi kubwa ya lobbying kwenye corridors za Wenstiminster ambayo pia umeridhiwa na wahiusika wakuu wakisuppotiwa na Mama Balozi wa UK nchini.

Game nzima itahitimishwa hivi karibuni kwa ile Lobby group kurudi tena UK kukamilisha mambo ili fedha zirudi.

Kitu kimoja naomba kuwahakikishia wanajamvi, fedha hizo zikirudi kupitia UK Aid kwa DFID, zitatumika kwa maendeleo kuikweli kweli, na hazitatumika kulipia vitafunio na kulipana posho.

Kwa bahati nzuri, Waingereza nawaelewa vizuri, wanautaratibu unaitwa 'scrach my back and I'll scratch yours' ukiona wameridhia fedha hizi zirudishwe kama msaada kupitia DFID, ambayo ni sawa na kuzirudisha serikalini, lazima wana lao jambo kama lilile lile lililopigiwa kelele sana na Barones Linda Chalker kabla hiyo 'obsolate' radar haijanunuliwa, kwani ilikubaliwa inunuliwe ili kuokoa ajira za Waingereza pale BAE, hivyo kuweka maslahi ya Waingereza mbele.

Hatua hii ya kuridhia kurejeshwa serikalini kwa mlango wa nyuma, lazima ina maslahi fulani kwa Uingereza, hivyo kinachofanyika ni Tanzania kupewa peremende ilambe kwanza ndipo kazi ifuatie. You just keep watching what next baada ya kurudishiwa kinachodaiwa ni chenji yetu, tutapigwa gundi ya mdomo kisawasawa and we can't say on anything to them!.

Pasco.
Pasco unachekesha kama si kujifariji toka lini UK AID ikawa idara ya serikali ya Tanzania au kuipangia serikali nini cha kufanya tuseme ille nipango ya kununua madawati na kujenga nyumba za walimu haipo tena.
 
Tatizo waandishi wenu wananunulika kwa bei nafuu sana, kibaya zaidi wanasahau hata nafasi ya heshima ya taaluma zao.

Mwandishi ananunuliwa kwa bahasha ndani kuna buku 5 ikizidi buku 10 dah njaa mbaya jamani.
 
sasa kama watu wameamua kuzidai basi wajenge hoja inayoendana na ukweli vinginevyo wanaonekana wanalazimisha na kutumia ujanja kuhalalisha kushindwa kwao. Hoja yao inatakiwa iwe very simple:

Kweli kulitokea uzembe, na wananchi wetu ndio waliodhurika, na tumetambua hilo ndio maana kesi x,y,z za wahusika zimefunguliwa na mashtaka mazito ya a, b, c, d yako juu yao. Kutokana na kutambua hili fedha hizi ambazo ni za hisani toka BAES kwa ajili ya watu wetu zitatusaidia, na tuko tayari kukaa na BAES na SFO kuona jinsi gani fedha hizi zitaingizwa nchini kuwanufaisha watu wetu. Hata kama hazitoletwa serikalini, sisi kama Serikali tungependa kujua utaratibu utakaohakikisha kuwa kweli fedha hizo zote zimeingia nchini kuwanufaisha watu wetu. Hivyo tunataka utaratibu huru, wa wazi na ambao utahusisha chombo huru cha tatu kusimamia mipango yote ambayo itafadhiliwa na fedha hizi. Uwakilishi wa serikali, asasi za kijamii, taasisi za kidini na vyama vya upinzani utahitajika na mfumo wa kuwahakikikishia Watanzania kuwa fedha hizi zinatumika vipi utawekwa na kila Mtanzania atakuwa na haki ya kujua matumizi ya fedha hizi. Wawakilishi wote wa kutoka Tanzania watalipwa na serikali nje ya fedha hizi. Miradi yote itakayofadhiliwa itakuwa na alama ya kuonesha ni fedha hizi ndio zimetumika, na Kila mwisho wa robo tatu Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu atatoa taarifa moja kwa moja umma juu ya matumizi ya fedha hizo. Tuko tayari hata fedha hizo zitolewe kwa kiwango fulani hadi itakapokamilika. Fedha ambazo zitakuwa hazijatolewa tutataka ziwekwe kwenye escrow account ili zipate faida."
 
Hivi ndivyo inavyotakiwa lakini kina Membe wanajitahidi kuficha uchafu uvunguni wakidhani watu hawaoni wangefanikiwa miaka ile ya '47 mawasiliano yalipokuwa ya simu za kukoroga line hadi uombe posta, wanajifanya masikini jeuri eti kama ni kupangiwa wako tayari kuzikosa wakati kesho yake wanatembeza bakuri kwa hao hao wanaowafanyia jeuri.
 
Kwenye msafara wa wanadai chenji huko Uiengereza, yumo communication officer wa Foreign Affairs - Assah Mwambene. Je huyu dogo anajuwa nini kuhusu hii article? Hivi Kikwete si yuko Guinea? kakutana lini na huyu waziri wa maendeleo wa Uingereza na wapi?
 
Labda wamo kwenye promosheni bana.....you never know
Tatizo waandishi wenu wananunulika kwa bei nafuu sana, kibaya zaidi wanasahau hata nafasi ya heshima ya taaluma zao.
 
Mengi naye achukue hatua amfukuze huyo mwandishi na muhariri wa NIPASHE
la sivyo watu kumchukulie kama na yeye ni SPEAKER ya serikali
 
Vithlani alihongwa heka na BAE ili awaconvince viongozi wa tz wanunue radar kwa bei ya juu, mahakama ikaamuru BAE wailipe tz kama charity paundi mil 29. Hii cyo chenji bali ni tozo ambayo BAe imeamriwa na mahakama ilipe kwa watz na cyo serikali ya tz ndio maana BAE wanataka wachannel hii ela thru charitable organizations. Membe kama ana uchungu na hii hela akawabane Chenge, Dr idriss, Vithlani na mkapa ili warudishe hongo waliopewa.
 
Yaani baada ya kuandika kote wiki hii nzima bado kuna watu wanaamua kuwapotosha Watanzania kwa makusudi. Ninaamini imeandikwa na mtu wa Ikulu au Mambo ya Nje.

JK, Waziri Uingereza wajadili chenji ya rada

Na Mwandishi maalum
2nd July 2011

JK%2846%29.jpg

Rais Jakaya Kikwete

Rais Jakaya Kikwete na Waziri wa Misaada ya Kimataifa ya Maendeleo wa Uingereza, Andrew Mitchel, wamekutana na kuzungumzia kuhusu fedha ambazo Serikali ya Tanzania inadai ilipwe na kampuni ya kuuza silaha ya nchi hiyo ya British Aerospace (BAE).

Katika mazungumzo hayo viongozi hao wawili wamekubaliana kuendelea na jitihada za kuishawishi BAE kuilipa Tanzania fedha hizo ambazo ni chenji iliyotokana na kuuziwa radi kwa sababu ni haki yake.

Tanzania inadai kulipwa fedha zake kiasi cha paundi za Uingereza milioni 29.5 zinazotokana na Tanzania kutozwa kiasi kikubwa zaidi kuliko kile kilichotakiwa kulipwa wakati inanunua rada kutoka BAE.

Ununuzi wa rada hiyo ulisababisha matatizo makubwa yakiwemo madai ya rushwa na hatimaye kampuni hiyo ya BAE ilifikishwa mahakamani kwa madai hayo ya kutoa rushwa katika ununuzi wa rada hiyo.

Hatimaye mahakama iliamua kuwa BAE haikutoa rushwa isipokuwa ilifanya makosa katika vitabu vyake vya mahesabu, lakini kampuni ikaamuliwa pia kulipa kiasi cha Paundi milioni 29.5 kuirudishia Tanzania ambayo ni fedha yake kihalali kwa sababu ilidhulumiwa fedha zake.

Hata hivyo, kampuni hiyo pamoja na kuamuliwa kuilipa Tanzania moja kwa moja, iliamua kutoa fedha hizo kwa taasisi isiyokuwa ya kiserikali ambayo ingeleta fedha hizo Tanzania kwa njia ya kutoa huduma.

Tanzania imepiga hatua hiyo na majuzi ilitoa taarifa kali bungeni kupinga hatua hiyo ya BEA, Serikali inataka kuziingiza fedha hizo katika kuboresha elimu ikiwa ni pamoja na kununua vitabu kwa ajili ya wanafunzi na kujenga madarasa na nyumba za walimu.

CHANZO: NIPASHE

Katika kauli amabazo nikizisikia napata kichefuchefu ni hii kauli ati tunadai chenji yetu.............Ni aibu kwa waziri au raisi unatoka mbele ya watanzania wenye akili timamu na kutuambia tunadai chenji...........huu ni ulimbukeni na kuwakosea adabu watanzania na taifa lao...Nadhani hii sio chenji ni wanarudisha pesa ya watanzania walioiba kwa kushirikiana na viongozi wachache waliokosa weledi katika taifa hili...Navyojua mie chenji ni pesa unayorudishiwa baada ya kununua kitu ambacho kipo pungufu ya pesa ulitumia mfano...pipi inauzwa shs 50 na wewe ukatoa 100..unapaswa urudishiwe shs 50 iliyozidi........sasa hii chenji inayozungumzwa ni takribani miaka zaidi ya 5 na tena ni baada ya kelele za watanzania wachache wanaoitakia mema nchi yao..............TUACHE KUFICHA UCHAFU,MANENO HALISI NI KUWA WANATURUDISHIA HELA WALIOIBA NA AKINA CHENGE NA SIO CHENJI...............Chenji sio neno muafaka kulitumia kwa sasa...
 
Siku zote wanajua kwamba sisi ni wasahaulifu ndio maana kunakupindisha ukweli lakini JF hawasahau kitu,ukweli umwagwa bwelele
 
Wanachakachua hadi habari! hii ni hatari ikulu inaweza kuchakachua kila jambo sas wanadai mahakama imeamua tulipwe na Bae wanaamua kuitoa kama hisani hivi wafikiri mahakama za huko ni sawa na hapa
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom