TFF yaomba radhi kwa makosa ya maandishi kuhusu Ngao ya Jamii, Simba yatakiwa kuirudisha

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
cebf9e90802fb28399057430ae5f7450.jpg
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF, linaomba radhi wanafamilia wote wa mpira wa miguu kutokana na makosa ya maandishi yaliyoonekana kwenye utambulisho wa Ngao ya Jamii iliyotolewa Jumatano Agosti 23, 2017.

Ngao hiyo ilitolewa mara baada ya mchezo uliokutanisha timu za Simba SC na Yanga FC za Dar es salaam kwenye Uwanja wa Taifa jijini. Katika mchezo huo, Simba ilishinda kwa mikwaju ya penalti 5-4 dhidi ya Yanga na kutwaa Ngao hiyo.

Watanzania hususani wanafamilia ya mpira wa miguu popote pale, TFF hatujapokea vizuri mwonekano wenye makosa kwenye Ngao hiyo ya Jamii kama ambavyo wadau hawajapokea vema suala hili.

Kutokana na makosa hayo, Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, tayari amechukua hatua za kinidhamu kwa watumishi waliohusika kadhalika kuwasiliana na uongozi wa Simba SC kuirejesha Ngao hiyo ili kufanyiwa marekebisho yatakayobaki kwenye Kumbukumbu sahihi.

Hatutegemei tukio kama hili kujirudia tena.
 
Huyo aliyemchukulia mwenzake hatua, naye anapaswa kuchukuliwa, ni uzwazwa wa hali ya juu kufanya kosa kama lile kwa taasisi kubwa kama TFF yenye waajiriwa wengi tena wenye elimu ya kutosha. Hata kwenye taaluma kuna makosa yakifanywa na Professor hayasameheki kamwe. Ila kiuungwana na kwa sababu michezo ni fair play, TUMEWASAMEHE tuliokwazika.
 
"Wanachukua hatua za kinidhamu kwa watumishi waliohusika" wao viongozi wa juu hawakuona tatizo hadi liibuliwe mitandaoni? Mabashite mengi nchi hii
 
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF, linaomba radhi wanafamilia wote wa mpira wa miguu kutokana na makosa ya maandishi yaliyoonekana kwenye utambulisho wa Ngao ya Jamii iliyotolewa Jumatano Agosti 23, 2017.

Ngao hiyo ilitolewa mara baada ya mchezo uliokutanisha timu za Simba SC na Yanga FC za Dar es salaam kwenye Uwanja wa Taifa jijini. Katika mchezo huo, Simba ilishinda kwa mikwaju ya penalti 5-4 dhidi ya Yanga na kutwaa Ngao hiyo.

Watanzania hususani wanafamilia ya mpira wa miguu popote pale, TFF hatujapokea vizuri mwonekano wenye makosa kwenye Ngao hiyo ya Jamii kama ambavyo wadau hawajapokea vema suala hili.

Kutokana na makosa hayo, Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, tayari amechukua hatua za kinidhamu kwa watumishi waliohusika kadhalika kuwasiliana na uongozi wa Simba SC kuirejesha Ngao hiyo ili kufanyiwa marekebisho yatakayobaki kwenye Kumbukumbu sahihi.

Hatutegemei tukio kama hili kujirudia tena.
Sio kweli na wao wana makosa waliikabidhi vipi bila kusoma? Ina maana ilitoka moja kwa moja kwa mtengenezaji na kuletwa uwanjani? Si ajabu mtengenezaji/mwandishi alifanya kwa makusudi ili kupima umakini wa viongozi na kwakweli amefanikiwa kuonesha kuwa viongozi wa TFF sio makini kabisa. Hii ni sawa na kupokea pesa na kuweka mfukoni bila kuhesabia na kukagua vizuri halafu baadaye unalalamika kuwa pesa ni pungufu au kuna fake ndani yake. Aibu yenu mmeumubuka dunia nzima. Hiyo ngao imepita kwenye mikono mingi kabla ya kuletwa uwanjani.
 
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF, linaomba radhi wanafamilia wote wa mpira wa miguu kutokana na makosa ya maandishi yaliyoonekana kwenye utambulisho wa Ngao ya Jamii iliyotolewa Jumatano Agosti 23, 2017.

Ngao hiyo ilitolewa mara baada ya mchezo uliokutanisha timu za Simba SC na Yanga FC za Dar es salaam kwenye Uwanja wa Taifa jijini. Katika mchezo huo, Simba ilishinda kwa mikwaju ya penalti 5-4 dhidi ya Yanga na kutwaa Ngao hiyo.

Watanzania hususani wanafamilia ya mpira wa miguu popote pale, TFF hatujapokea vizuri mwonekano wenye makosa kwenye Ngao hiyo ya Jamii kama ambavyo wadau hawajapokea vema suala hili.

Kutokana na makosa hayo, Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, tayari amechukua hatua za kinidhamu kwa watumishi waliohusika kadhalika kuwasiliana na uongozi wa Simba SC kuirejesha Ngao hiyo ili kufanyiwa marekebisho yatakayobaki kwenye Kumbukumbu sahihi.

Hatutegemei tukio kama hili kujirudia tena.

wakirekebisha watawakabidhi simba kwa mechi nyingine ya community sheild?
 
Back
Top Bottom