TFF yamtangaza kocha wa Azam FC Ndiyaragije Etienne, kuwa kaimu kocha mkuu wa Taifa Stars

Ammy Ninje ana leseni A inayotambuliwa na FIFA ni Kocha wa level za akina Pep Guardiola..ila siasa ndo zinamaliza soka la Tanzania
Makocha wazawa hawana exposure na mechi za kimataifa kabisa tutaendelea kusugua bench sana we dont have the bright future
 
Leo tarehe 11 Julai Shirikisho la Soka nchini(Tanzania Football Fedaration-TFF) limetangaza Kocha wa Azam FC, Ndiyaragije Etienne, kuwa Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ‘Taifa Stars’.

Kocha huyo mpya ataiongoza timu hiyo katika mashindano ya CHAN, akisaidiwa na Kocha wa Coastal Union, Juma Mgunda.

View attachment 1151517
Bora wangempa yule Mwenyekiti wa Yanga ndio Mzawa.
 
TFF ya awamu ya wendawazimu kabisa. Sijui wanatumia kiungo gani kufikiri.
Kama ni suala la kumpa mzawa na ni wazo zuri, huyo Mrundi katokea wapi?
Mkuu . Labda amekua mzawa by default baada ya kupewa ukocha. Teheteheee
 
Gonjwa kuu la watanzania ni kutaka kuvuna pale ambapo hawaja wekeza!!!!!! Hivi tulitaka Amonike afanye miujiza gani? Hatuwekezi vya kutosha kwenye soka kwa muda mrefu lakini tunatarajia mafanikio. Hatuwekezi vya kutosha kwenye kukuza kiswahili lakini unasikia watu wakidai kitumiwe kufundisha masomo yote chuo kikuu. Mara ya kwanza kutinga AFCON tuna ambiwa ni miaka takribani 40 iliyopita, baada ya kuingia tena mara pili, tunategemea tuta angusha vigogo. Mpira, Riadha, na michezo mingine lazima tuwekeze toka chini na tuwe na mipango ya muda mrefu, vinginevyo maumivu yatakuwa yetu daima. Utamu unakuja tunapo weka siasa zetu ndani ya michezo hii.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom