TFF yamtangaza kocha wa Azam FC Ndiyaragije Etienne, kuwa kaimu kocha mkuu wa Taifa Stars

Display Name

JF-Expert Member
Feb 11, 2014
423
451
Leo tarehe 11 Julai Shirikisho la Soka nchini(Tanzania Football Fedaration-TFF) limetangaza Kocha wa Azam FC, Ndiyaragije Etienne, kuwa Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ‘Taifa Stars’.

Kocha huyo mpya ataiongoza timu hiyo katika mashindano ya CHAN, akisaidiwa na Kocha wa Coastal Union, Juma Mgunda.

E8F954B6-F910-4428-B236-3D29F99906CA.jpeg
 
Kikao cha Kamati ya dharura cha Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF), ambacho kimekutana leo Julai 11, 2019 kimemtangaza kocha mkuu wa Azam FC Ndayiragije Etienne kuwa Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Tanzania Taifa Stars.

Kocha Etienne, amependekeza benchi lake la ufundi kusaidiwa na kocha wa Coastal Union Juma Mgunda pamoja na kocha Msaidizi wa Polisi Tanzania Suleiman Matola, ambapo Meneja wa kikosi hicho atakuwa Nadir Haroub Cannavaro.

Uteuzi huo umezingatia program maalumu ya kuendeleza makocha wazawa.



IMG_20190711_211448_374.jpeg
 
Sasa kuendeleza wazawa uyo wa azam ni mzawa sasa?

Kwanza ni wa muda au ndio kapewa mazima?
 
Hii tii efu efu ya si si emu, bado haijaacha tu kutuletea wadau wa michezo masapraizi ya kila aina! Hongera nyingi ziwafikie wateule wote. Mwisho wa siku matokeo tutayaona uwanjani.
 
Kukuza vipaji vya wazawa. Ettiene( kifaransa lakini Ni Steven kiingereza St kiswahili).
Huyu ni mzaliwa wa Burundi. Mrundi.
 
Makocha wazawa hawana exposure na mechi za kimataifa kabisa tutaendelea kusugua bench sana we dont have the bright future
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom