TFF yaigeuzia kibao Vodacom; Yataka vielelezo sakata la jezi Yanga

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Messages
15,870
Points
1,225

nngu007

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2010
15,870 1,225
[h=3][/h]

*Yataka vielelezo sakata la jezi Yanga

Na Zahoro Mlanzi

SAKATA la Klabu ya Yanga kutovaa jezi zenye nembo nyekundu, limezidi kuchukua sura mpya ambapo Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), sasa limeigeukia
Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom na kuitaka iwasilishe vielelezo vinavyoonesha kukubaliana na Yanga.

Yanga tangu kuanza kwa Ligi Kuu Bara, Januari 20 mwaka huu haijavaa jezi zilizotolewa na Vodacom, ambazo kifuani zina nembo ya kampuni hiyo ambayo ndiyo mdhamini mkuu wa ligi hiyo.
Kutokana hilo, Yanga katika michezo yake miwili dhidi ya JKT Ruvu na Moro United, wachezaji wake hawakuvaa jezi hizo za Vodacom, badala yake walivaa zenye nembo ya Kilimanjaro Lager ambao ni wadhamini wao.

Akizungumza Dar es Salaam jana kuhusu sakati hilo, Ofisa Habari wa shirikisho hilo Boniface Wambura, juzi alisema waliiandikia barua Yanga kuhusu msimamo wa TFF kuhusu ulazima wa kuvaa jezi hizo kama kanuni inavyoeleza.

"Pamoja na Yanga kuiandikia barua hiyo, lakini pia tumewaandikia Vodacom tukitaka watueleze makubaliano waliyofikia kati yao na klabu hiyo kwa maandishi ndipo tutakapojua la kufanya," alisema Wambura.
Alisema Yanga ilijieleza juu ya hilo na kutoa sababu ambazo hazina msingi kwani Ligi Kuu Bara inaongozwa na kanuni, hivyo haina budi kuzifuata, kwa kuwa Yanga ikikubaliwa, timu nyingine zinaweza kuomba rangi wanazotaka.

Wambura alisema kama yapo makubaliano mengine yaliyofikiwa tofauti na kanuni zinavyoelekeza, Vodacom ndiyo wanaotakiwa waoneshe ni makubaliano ya aina gani waliyofikia.
Wiki iliyopita viongozi wa Yanga, walithibitisha kwamba timu hiyo ilishakubaliana na Vodacom kwamba watavaa jezi zenye nembo nyeusi.

Baada ya taarifa hizo, TFF ilisema kinachotakiwa ni Yanga kukubali hali iliyopo na ikizingatiwa kwamba mkataba wa Vodacom unamalizika msimu huu.
Alisema ni bora kuendelea na msimamo kama kanuni inavyoagiza kuliko kutoka nje ya kanuni kwani kunaweza kuleta matatizo makubwa.
 

Forum statistics

Threads 1,389,976
Members 528,065
Posts 34,040,174
Top