TFF yagawa noti kwa wahariri wa michezo‍, hii vita haitaisha bure

Trump2

JF-Expert Member
May 28, 2017
1,553
2,608
DAR ES SALAAM

Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), jana liligawa mamilioni ya Shilingi kwa wahariri wa michezo wa vyombo mbalimbali vya habari za michezo waliohudhuria mkutano uliotishwa na Rais wa shirikisho hilo, Wallace Karia.

Taarifa za kuwepo kwa mgawo huo wa fedha zimetolewa na baadhi ya wahariri waliohudhuria mkutano huo, uliofanyika jana asubuhi katika Hoteli ya Sea Scape jijini Dar es Salaam.

Imeelezwa kuwa zaidi wa wahariri 30 walihudhuria mkutano huo na kila mhariri aligawiwa Shilingi laki moja (100,000) na kwamba mgao huo uliwafikia pia wapiga picha waliokuwepo. Imedaiwa kuwa zaidi ya Shilingi milioni nne ziligawiwa kwa wahariri na wapiga picha

Taarifa zimeeleza kuwa fedha hizo ziligawiwa na Ofisa mmoja wa TFF wa kitengo cha uhasibu kwa utaratibu wa wahariri na wapiga picha kuorodhesha majina yao, lakini haikufahamika mara moja lengo la mgawo huo.

Haya yamebainika wakati Rais wa TFF, Karia akieleza shirikisho hilo liko katika mpango wa kubana matumizi na kupambana na ufisadi huku akifananisha mwenendo wa utendaji na ule wa Rais Dk. John Magufuli katika kupambana na matumizi yasiyo ya lazima na kupambana na ufisadi.

Katika mkutano wake wa jana, pamoja na mambo mengine, alisema ndani ya miezi saba, TFF imetumia Shilingi 3,752,001,171.00 hukusehemu kubwa ya matumizi hayo ikielekezwa kwenye usimamizi wa ligi mbalimbali na kuandaa timu za taifa ambako zimetumika Sh. 2,409,150,732 ambazo nisawa na asilimia 64 ya matumizi yote.

Asilimia 36 ya fedha zilizobaki ilitumika kulipia madeni ya TFF, mishahara ya wafanyakazi, kusaidia mikoa katika maeneo ya miundo mbinu, kuwajengea uwezo wafanyakazi na kuendesha mafunzo mbalimbali.

Aidha Rais Karia alieleza kuwa shirikisho limepunguza mishahara kwa wafanyakazi kutoka Sh. Milioni 85, mpaka Shilingi milioni 50 baada ya kupunguza idadi ya wafanyakazi kutoka 44 mpaka 21 waliobaki sasa huku kukiwa na wale wa kujitolea.

Haijafahamika kiasi hicho kilichogawiwa jana kwa wahariri kilitolewa katika fungu gani
 
Mshaanza tayari, hakuna press yoyote ya kiongozi mkubwa ambayo haina bahasha.
Mi nipo kwenye sekta ya habari lila zaidi ya nusu ya press nilizohudhuria nimetoka na bahasha tena yenye nembo ya taasisi husika (TFF walikosea tu kutokutuwekea kwenye bahasha; wakatupa mikononi).
 
Waliingia kwa fitina lakini naamini haitawaacha, ukipanda fitina tegemea kuvuna matunda yake yakiwa mengi na yamesitawi kwa wingi pia.

TFF hii ni full vitimbwi daily
 
DAR ES SALAAM

Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), jana liligawa mamilioni ya Shilingi kwa wahariri wa michezo wa vyombo mbalimbali vya habari za michezo waliohudhuria mkutano uliotishwa na Rais wa shirikisho hilo, Wallace Karia.

Taarifa za kuwepo kwa mgawo huo wa fedha zimetolewa na baadhi ya wahariri waliohudhuria mkutano huo, uliofanyika jana asubuhi katika Hoteli ya Sea Scape jijini Dar es Salaam.

Imeelezwa kuwa zaidi wa wahariri 30 walihudhuria mkutano huo na kila mhariri aligawiwa Shilingi laki moja (100,000) na kwamba mgao huo uliwafikia pia wapiga picha waliokuwepo. Imedaiwa kuwa zaidi ya Shilingi milioni nne ziligawiwa kwa wahariri na wapiga picha

Taarifa zimeeleza kuwa fedha hizo ziligawiwa na Ofisa mmoja wa TFF wa kitengo cha uhasibu kwa utaratibu wa wahariri na wapiga picha kuorodhesha majina yao, lakini haikufahamika mara moja lengo la mgawo huo.

Haya yamebainika wakati Rais wa TFF, Karia akieleza shirikisho hilo liko katika mpango wa kubana matumizi na kupambana na ufisadi huku akifananisha mwenendo wa utendaji na ule wa Rais Dk. John Magufuli katika kupambana na matumizi yasiyo ya lazima na kupambana na ufisadi.

Katika mkutano wake wa jana, pamoja na mambo mengine, alisema ndani ya miezi saba, TFF imetumia Shilingi bilioni3,752,001,171.00 hukusehemu kubwa ya matumizi hayo ikielekezwa kwenye usimamizi wa ligi mbalimbali na kuandaa timu za taifa ambako zimetumika Sh. bilioni2,409,150,732 ambazo nisawa na asilimia 64 ya matumizi yote.

Asilimia 36 ya fedha zilizobaki ilitumika kulipia madeni ya TFF, mishahara ya wafanyakazi, kusaidia mikoa katika maeneo ya miundo mbinu, kuwajengea uwezo wafanyakazi na kuendesha mafunzo mbalimbali.

Aidha Rais Karia alieleza kuwa shirikisho limepunguza mishahara kwa wafanyakazi kutoka Sh. Milioni 85, mpaka Shilingi milioni 50 baada ya kupunguza idadi ya wafanyakazi kutoka 44 mpaka 21 waliobaki sasa huku kukiwa na wale wa kujitolea.

Haijafahamika kiasi hicho kilichogawiwa jana kwa wahariri kilitolewa katika fungu gani

Muwe mnaeleza bahasha zote mnazopata kwenye press conference zoter zikiwemo zile za vyama vya siasa...mueleze kila kitu...Waaandishi wengi hawana mishahara au wanachelewa kulipwa kwa hiyo wanategemea bahasha kutoka kwa sources au watoa habari mbalimbali...Hivi siku hizi NSSF haiwaaliki tena waandishi wa habari na hasa wahariri na kuwalipia gharama za hoteli, posho ndani ya bahasha to the tune of tsh 500,000/- or more?
 
wafanyakazi 21 wanalipwa mshahara wa mill 50. ikiwa na maana ya kwamba on average kila mfanyakazi analipwa mshahara wa mill 2.4.
HAHAHAAAAAAAAA WE MCHOKOZI MAANA NIMETOKWA NA MACHOZI KWAKUCHEKA

NDIOMAANA WAMELAMBA BAAHASHA AKILIZAO ZIKAWA NA RANGI ZA KHAKI WAKASAHAU KUULIZA MASWALIYAAMAANA KAMA HAYA
 
500
Muwe mnaeleza bahasha zote mnazopata kwenye press conference zoter zikiwemo zile za vyama vya siasa...mueleze kila kitu...Waaandishi wengi hawana mishahara au wanachelewa kulipwa kwa hiyo wanategemea bahasha kutoka kwa sources au watoa habari mbalimbali...Hivi siku hizi NSSF haiwaaliki tena waandishi wa habari na hasa wahariri na kuwalipia gharama za hoteli, posho ndani ya bahasha to the tune of tsh 500,000/- or more?
"000 HIBAHASHA YA KUBAHASHIWA SIOHIVHIVI
 
Brown envelop kwa wanahabari ni kitu kisichosahihi lakini kimekua mazoea.
Hapo wanabana matumizi wametoa 100,000 maana yake wangekua hawabani matumizi wangetoa zaidi
 
Karia ndo rais wa TFF anayefaa,hizi ni fitina za yanga
 
Mnagawa pesa kwa wahariri huku mna madeni kibao ya wachezaji ambao wanawadai

mfano:Wachezaji wa timu ya beache soccer na kocha wao wanawadai pesa zao mpaka leo hamjawalipa hii dhuluma haitawaacha salama TFF
 
wafanyakazi 21 wanalipwa mshahara wa mill 50. ikiwa na maana ya kwamba on average kila mfanyakazi analipwa mshahara wa mill 2.4.
huu ni ulafi tu, kutokana na ukosefu wa ajira, wangejilipa 1.3 fedha hizo zingeajiri hadi watumishi 40.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom