TFF wekeni kigezo cha vyeti kwa walio na nafasi za usemaji na uhamasishaji ili kudhibiti ufinyu wa akili unaojitokeza

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,635
7,005
Jambo hili ni muhimu sana.Utakuta mtu anafanya personal attack kwa muwekezaji na biashara zake kisa alinyimwa mshahara anaoutaka.

Jambo hili ni ugaidi wa kibiashara na lisipoangaliwa vizuri litaleta shida sana baadae.

Kama wewe ni msemaji wa timu pinzani hakuna sababu ya kuleta personal attacks kwenye brands za watu badala ya kuleta utani na club.

Sijawahi kusikia bidhaa za GSM wala Azam zikishambuliwa tangu nimeanza kufuatilia mpira wa kibongo.Ila naona kuna mtu anafanya juu chini kuuangusha mbuyu.Huyu ni maskini kabisa aliyejawa na chuki na visasi.Kisa Alitaka alipwe pesa nyingi kuliko wachezaji kisa anatukana ovyo insta.

TFF naombeni mtengeneze kanuni ili watu hawa wakiajiriwa na club wawe na vyeti.
Vinginevyo wabaki kama mashabiki wengine wa kawaida
 
Kabsa maana vijana wasomi ni wengi sana hawa wengine wawe mashabiki tu
 
  • Thanks
Reactions: mmh
Na alivyo na nuksi yule jamaa akikishambulia kitu ujue iko kitu ndo kitatoboa. Kwa hiyo akitusema ndo anatupa mafanikio. Kila akipendacho hua kina negative, oneni alivyobusu goli lao jamaa mpaka leo hawaelewi.
 
Ayo mambo ya Haji timu nyingine zili lalamika kwa miaka Mingi Tff waliziba masikio na Simba walikua wakishangilia vitendo hivyo wakiwemo Vingozi wa Simba. MO, Barbara na wengineo walimuona Haji ni shujaa wao,Sasa kibao kimegeuka kinacho hitajika ni uvumilivu Kama walivyo vumilia wengine. Hatutegemei Tff Wala Serikali kuingilia kwakua waliyaacha Mambo yaende Kama yalivyo.
 
Hawawezj kuweka maana bosi kubwa tu ana degree ya mifugo.,akikazania kuhusu vigezo wanaweza kumchomoa hata yeye maana hana sifa zinazohitajika
 
Hivi ni kweli Haji anawapelekesha kwa kiasi kikubwa hivi!? Mbona sisi tuliishi nae hivyo hivyo na ilikiwa fresh tu? Halafu kuna kipindi alikuwa akikebei pia magodoro ya gsm mbona haukuwahi kemea hivi?
 
Kwani manara kafanya kipi cha hatari na ugeni ..ni utani tu. Kama amevunja sheria kwani mahakama hamzijui? Wanasheria mlioajiri wanakazi gani?
 
Na alivyo na nuksi yule jamaa akikishambulia kitu ujue iko kitu ndo kitatoboa. Kwa hiyo akitusema ndo anatupa mafanikio. Kila akipendacho hua kina negative, oneni alivyobusu goli lao jamaa mpaka leo hawaelewi.
Alivyowashambulia Yanga kipindi yupo Simba, je Yanga walitoboa kimafanikio?
 
Jambo hili ni muhimu sana.Utakuta mtu anafanya personal attack kwa muwekezaji na biashara zake kisa alinyimwa mshahara anaoutaka.

Jambo hili ni ugaidi wa kibiashara na lisipoangaliwa vizuri litaleta shida sana baadae.

Kama wewe ni msemaji wa timu pinzani hakuna sababu ya kuleta personal attacks kwenye brands za watu badala ya kuleta utani na club.

Sijawahi kusikia bidhaa za GSM wala Azam zikishambuliwa tangu nimeanza kufuatilia mpira wa kibongo.Ila naona kuna mtu anafanya juu chini kuuangusha mbuyu.Huyu ni maskini kabisa aliyejawa na chuki na visasi.Kisa Alitaka alipwe pesa nyingi kuliko wachezaji kisa anatukana ovyo insta.

TFF naombeni mtengeneze kanuni ili watu hawa wakiajiriwa na club wawe na vyeti.
Vinginevyo wabaki kama mashabiki wengine wa kawaida
Mkuu jamaa ameshatulia baada ya kuona hajibiwi ,ametukana sana hakuna anayemjibu akajishtukia Sasa hivi kapunguza ,baadaye atakuwa mpole ,isitoshe pale Yanga msemaji ni bumbuli ,anayesemea timu ni bumbuli ,yeye Yuko upande wa gsm cheo lenyewe hata halieleweki
 
Back
Top Bottom