TFF - Weka maslahi ya taifa mbele!!!

JuaKali

JF-Expert Member
Nov 14, 2007
776
118
Napenda kuwasuta kwa nguvu zote viongozi wa TFF kwa kukurupuka kutoa adhabu nzito bila kuzingatia maslahi ya taifa. Ningewaungeni mkono kama mgekuwa makini na kuwafungia viongozi wote wa Yanga kutojihusisha na michezo kwa muda wowote badala ya kuifungia club. Swali kubwa kwenu TFF kulikuwa na umuhimu gani kuifungia kushiriki mashindano yanayoandaliwa na chombo kingine CAF badala ya yale mnayoyaandaa? kwa nini kama mna uchungu msingeifungia kucheza ligi kuu as well? Mnaogopa kufirisika bila yanga kushiriki ligi kuu mtakosa pesa za kuhesabu usiku kucha huku mkitia ndani pesa kibao. YOUNG AFRICA WALIKOSEA LAKINI NYIE MMETIA FORA!
JIREKEBISHENI---MASLAHI YA TAIFA MBELE THEN UBINAFSI!!
 
Napenda kuwasuta kwa nguvu zote viongozi wa TFF kwa kukurupuka kutoa adhabu nzito bila kuzingatia maslahi ya taifa. Ningewaungeni mkono kama mgekuwa makini na kuwafungia viongozi wote wa Yanga kutojihusisha na michezo kwa muda wowote badala ya kuifungia club. Swali kubwa kwenu TFF kulikuwa na umuhimu gani kuifungia kushiriki mashindano yanayoandaliwa na chombo kingine CAF badala ya yale mnayoyaandaa? kwa nini kama mna uchungu msingeifungia kucheza ligi kuu as well? Mnaogopa kufirisika bila yanga kushiriki ligi kuu mtakosa pesa za kuhesabu usiku kucha huku mkitia ndani pesa kibao. YOUNG AFRICA WALIKOSEA LAKINI NYIE MMETIA FORA!
JIREKEBISHENI---MASLAHI YA TAIFA MBELE THEN UBINAFSI!!

Juakali,
Naomba ufafanuzi wa mambo yafuatayo:
1. Club ya soka ni nini/nani?
2. Viongozi wa timu wanafanya kazi ya nani?
3. Je haya maamuzi yaliyotolewa ni ya kisheria au ni blabla tu ?
4. Masilahi yapi ni ya Taifa?
 
Maamuzi yalitolewa kwa niaba ya klabu na viongozi wa Klabu!!
Ni sahihi kwa klabu kupewa adhabu kutokana na kutokuwa makini kwa waendeshaji!!

Ni jukumu la wenye klabu kuwachukulia hatua wale walioifikisha klabu hapo....

Nidhamu iwe mbele ama sivyo suala la utaifa halina maana.......
ama sivyo utafumbia macho MAMBO mengi kwa ajili ya UTAIFA..........
uNAONAJE..tusizungumzie UFISADI sababu ITATIA AIBU nchi yetu???
Siamaini kwa utaifa kwa watu wasio na nidhamu!!
 
masilahi ya taifa ni kutetea timu ambayo haina nidhamu?
Timu kwa maana ya kundi zima wakiwemo wiongozi, washauri, na wachezaji?

kumbuka mchelea mwana kulia ...........
matikeo ya kubembeleza wana wetu wa pekee ndio haya, toto zee kabisa lakini busara bado, wadogo zake watakuwa na mifano gani?
ingewezekana timu ya simba na yanga zikafutika katika uso wa nchi yetu, wataalamu wetu wa soka, wachezaji wetu makini, makocha wetu wazuri, ndio tungeona uwezo wao.
 
Haika nakubaliana na wewe kabisa.

Hawa Yanga na Simba wamedominate katika soka la Tanzania, na kwa kiasi kikubwa ndio wanalirudisha nyuma hili soka letu. Adhabu kwa Yanga ni fundisho kwa Simba kwamba nao wakifanya upuuzi kama huo hamna kubebana tena.
Kama ni amri yangu wale watoto wa copa cocacola wasiingie kabisa kwenye milolongo hii ya simba na yanga, ziundwe club zinazoendeshwa professionally ambapo zichukue watoto vipaji kama wale na sio walenge simba na yanga ambazo mpaka sasa wahusika kuua vipaji kutokana na majungu, fitna na husuda.
 
Mkuu JuaKali, hivi masilahi ya taifa katika soka ni yapi? Ni timu moja kudhalilisha taifa zima?

Maamuzi ya Yanga hayakujali kabisa masilahi ya taifa kisoka...

Uamuzi wa Yanga ulikua ni uamuzi uliofanywa na viongozi halali kwa niaba ya klabu....hili halikwepeki....Unaona jinsi nchi yetu inavyoshindwa kujinasua kutoka kwenye mikataba inayotulalia? Kwa sababu tu ilipitishwa na viongozi wetu waliowekwa kihalali? ale yalikua ni maamuzi halali ya Yanga, hivyo adhabu inapaswa kwenda kwa klabu.....

Pia kuna ile dhana kwamba mpira Tz ni Simba na Yanga tu...... hakika zikifa klabu hizi zitaibuka klabu nyingine...pengine bora zaidi. Haziwezi kufa na mashabiki wa soka.

Hata kama ni chungu, hiyo ndiyo dawa....sivyo siku nyingine ungesikia Yanga ama Simba wameamua kuondoa wachezaji wao wote timu za taifa.
 
Simba na Yanga ni vimeo vitupu.Tatizo la timu zingine ni kuwa na zenyewe viongozi na wachezaji ni washabiki wa timu hizo mbili.Hapo no soka ni utumbo kwa kwenda mbele.
 
Mkuu JuaKali, hivi masilahi ya taifa katika soka ni yapi? Ni timu moja kudhalilisha taifa zima?

Maamuzi ya Yanga hayakujali kabisa masilahi ya taifa kisoka...

Uamuzi wa Yanga ulikua ni uamuzi uliofanywa na viongozi halali kwa niaba ya klabu....hili halikwepeki....Unaona jinsi nchi yetu inavyoshindwa kujinasua kutoka kwenye mikataba inayotulalia? Kwa sababu tu ilipitishwa na viongozi wetu waliowekwa kihalali? ale yalikua ni maamuzi halali ya Yanga, hivyo adhabu inapaswa kwenda kwa klabu.....

Pia kuna ile dhana kwamba mpira Tz ni Simba na Yanga tu...... hakika zikifa klabu hizi zitaibuka klabu nyingine...pengine bora zaidi. Haziwezi kufa na mashabiki wa soka.

Hata kama ni chungu, hiyo ndiyo dawa....sivyo siku nyingine ungesikia Yanga ama Simba wameamua kuondoa wachezaji wao wote timu za taifa.

Unajua Simba ni wajanja sana.... Walikaa naYanga pamoja na TFF kwa makubaliano ya kupatiwa mil 50 kila timu hiyo ilkuwa ni kumpoteza yanga kwenye ramani ya soka.. Sasa sijui viongozi wa Yanga hawajui kusoma alama za nyakati. MASIKINI ONA MASHIBU YALIYOWAKUTA..?anyway
 
Ukitafakari kwa undani zaidi utaiona pande zote za wadau wamekosea hiki au kile kwa kukosa umakini na busara katika kuamua mambo yaani "Leadership during crisis"

1. YANGA - wana makosa ya kutopeleka timu uwanjani. Viongozi wa Yanga wanatakiwa watambue kuwa pamoja na mambo yote wanayoyafanya mteja wa mwisho wa bidhaa yao in Shabiki anayelipa kuona timu yao ambaye anatakiwa apewe haki yake. Hakuna sababu yeyote inayozidi kutopeleka timu hata kama kweli walikubaliana na TFF.

2. CECAFA - pamoja wao ndio wenye mashindano lakini hawakujipa muda wa kutoka kwenye hasira na kutulia kutoa maamuzi, ndio maana hata sura zao Musonyi na Magori wakati wakiongea na waandishi zilionekana ni kama vile viongozi wa mtaani. Mfano haikiuwa busara Katibu Mkuu wa CECAFA kusema "Viongozi wa Yanga ni wapumbavu kabisa, and Yanga is being led by very stupid leaders". Hata kama katibu huyu alikuwa amekasirika kiasi gani sio busara kutukana mbele ya waandishi hata kama adhabu waliyopewa Yanga ni ya kikatiba. Pili, walitakiwa wajipe muda wa kuwahoji viongozi wa Yanga, huenda CECAFA ingejitegua kwenye mtego wa TFF/CECAFA of having same leaders sitting on different shirts. Natural justice haikufuatwa na hiyo ndiyo CECAFA inayotaka mpira uendelee. Upuuzi huu ndio ulifanya Zambia na Malawi kugeuza kigoso kujiunga na COSAFA.

3. TFF - Hawa ndio hovyo kabisa, kwanza hawakustahili kuifungia Yanga kwa mashindano ambayo si yao, pili walitakiwa kuweka uwazi wa kile ambacho Yanga wanasimamia na wapenda soka wana haki ya kueleweshwa kwa nini madai ya Yanga ni upuuzi, pia hawakuwapa nafasi viongozi wa Yanga kujitetea. Tatu, kwa mazingira ya tatizo lenyewe TFF kutoa adhabu ni kuihukumu Yanga mara zaidi ya moja ambapo ni kinyume hata na sheria ya popote achilia mbali ya mpira wenyewe. TFF wanatakiwa wapewe semina ya "crisis management" (yaani kuamua kitu ndani ya mzongo).

NGOJA TUONE, MAANA YANGA WAMEKATA RUFAA NA SASA MUNKARI WA WOTE UMEPUNGUA NA TFF WANAJUA SIASA ZA MPIRA WAKI-HANDLE VIBAYA HII ISSUE YA YANGA HUENDA WASIRUDI MADARAKANI MAANA WAPIGA KURA NDIO HAO HAO YANGA NA SIMBA.
 
Naamini uamuzi wa TFF ulikuwa wa kukurupuka na hauna fundisho lolote kwa Yanga wala kwa Taifa. Wanajaribu tu kuonyesha kuwa wanaweza kuchukua maamuzi mazito ambayo mwisho wa siku yatabatilishwa. Au pengine tuseme ilikuwa ni njia ya kuibeba Simba ili ishiriki mashindano ya mwakani. Juzi nilimwona Musonye (fool I must say) akisema kuwa Yanga walikataa kuja uanjani baada ya kwenda kwa mganga na kuambiwa kuwa wangefungwa. Sijui kama TFF inakubaliana na maoni haya ya Secretary General wa CECAFA na kama ni hivyo, basi tatizo la Yanga haliwezi kuwa solved na kuwafungia kushiriki mashindano ya kimataifa mwakani. Mimi naamini tatizo la imani za kichawi katika mpira ni kubwa na linafanywa na klabu karibu zote. Yanga imefanya kosa ndiyo, lakini solution ni kuwafungia mashindano ya Kmataifa? Nakubaliana na CECAFA kuwafungia mashindano yake kwa sababu iliyasusia lakini kwanini wafungiwe mashindano ya CAF??? Hili halina faida yoyote kwa mpira wa Tanzania. ningeelewa kama adhabu kubwa ya fedha ingetolewa dhidi ya Yanga maana hii ingekuwa mwiba mkubwa kwa viongozi na wanchama wangeona sababu za kuwaondoa viongozi wapuuzi kama madega. Kwa maelezo hayo, mimi nakubaliana na wale wanaosema kuwa adhabu hii kwa Yanga was unnecessary. TFF ilitakiwa itafute njia ya kuwashauri CECAFA kupunguza adhabu toka miaka mitatu hadi mwaka mmoja au miwili badala ya kushindilia zaidi. Tukumbuke pia kuwa katika sheria za kawaida (rules of natural justice)huwezi kumwadhibu mtu mara mbili kwa kosa lilelile. Wanasheria wana kifungu cha utetezi kinachoitwa "autrefois convict" ie. nilishitakiwa kwa kosa hilihili na competent body na kutiwa hatiani. Vilevile kuna rule ya "hear the other side" (you dont condemn a person unheard). Yanga kama timu haikupewa nafasi ya kupresent utetezi wake. Eti TFF inadai utetezi upelekwe na viongozi baada ya adhabu kutolewa! kwa hiyo tusiongelee suala hili kwa ushabiki huku tukiacha chama cha mpira kinaendelea kudidimiza soka hapa nchini.
 
Tafadhari soma makala hii http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/8/4/makala3.php. kikubwa nilikuwa najaribu kuona upande wa pili wa shilling upo vipi badala ya kuiangalia upande mmoja.

Hakuna upande wa pili wa shilingi maana umefutika hauonyeshi chochote. Yanga wamekosa nidhamu na wanastahili adhabu zote walizopewa na TFF, CECAFA, CAF na hata FIFA wakiibuka na adhabu yao basi mimi nitaiunga mkono. Hizi timu mbili za Yanga na Simba zimechangia sana katika kudorora kwa mpira Tanzania. Hivyo adhabu kama waliyopewa Yanga itawafunua macho vilabu vingine na kuwaonyesha kwamba uhuni kamwe hautavumiliwa. Kufungiwa kwa Yanga hakutaathiri maslahi yoyote ya Tanzania
 
Hadi vilabu vya nje ya Dar vikipata nguvu na mashabiki ndo utaweza kusema kuwa mpira wa Tanzania unaweza kuendelea bila Yanga na Simba. Kwa sasa Tanzania ukiiondoa Simba au Yanga kwenye ligi kuu, itabidi watu wahamie kwenye ngumi, riadha au vinyoya kwani washabiki watakuwa kiduchu na viingilio inabidi viwe chini. Nakumbuka kipindi ambacho klabu za Pamba, Coastal, Pan na Majimaji zilipokuwa na nguvu, na Simba ikawa inashuka daraja, ilibidi mbinu zitumike na Yanga wakakubali kufungwa mechi ya mwisho (ilishatwaa ubingwa) maana kuanguka kwa simba wakati huo kulimaanisha kudorora kwa mpira. Kwahiyo leo hii ukiifungia Yanga na ikaamua kujitoa ligi kuu, TFF itavunjik! Mark my word! Hao jamaa wa TFF wapo pale kwa kutegemea mapato yanayotokana na washabiki wa Yanga na Simba!
 
Yaelekea ndugu zangu hili tatizo la viongozi wa Yanga kugomea mchezo kati yao na Simba na adhabu zilizotolewa na TFF na CECAFA tunaliangalia juu juu tu lakini ukilifatilia kwa undani utakuta kuwa ulikuwa uwamuzi mbaya sana ambao huenda ungekuwa na athari kubwa.

Jambo la kwanza nasikitika kwa viongozi wa yanga kuwa na fikra zilizodumaa katika kufikia uwamuzi wao wa kutopeleka timu uwanjani kwa madai ya kudai kwanza walipwe 50ml hata kama walikubaliana na wenzao wa Simba kama wanavyodai lakini wao kama watu wazima na wenye upeo wa kufikiri.
(i)Hivi kwa akili ya kawaida Yanga wana uhakika gani kuwa TFF na CECAFA walikuwa na hizo 50ml za kuwapa wao kabla ya mchezo?

(ii) Zawadi ya mshindi wa kwanza wa mashindano ya kagame anapata USD 30,000 ( takribani 34ml) ili kwa akili ya kawaida hata hiyo timu ambayo ingekuwa mshindi wa kwanza wangejisikia vizuri kweli kujua kuwa kuna timu iliyopewa pesa zaidi kuliko zawadi stahili?,

(iii) Kwa mfano mashindano haya yangefanyika nje ya Tanzania Yanga wangekuwa na nafasi ya kutaka wapewe 50ml?

(iv) Yanga hawaoni kuwa uamuzi wao kutopeleka timu yao uwanjani ingesababisha madhara kwa watu na mali endapo mashabiki waliolipa pesa zao wangeamua kufanya fujo kudai kurudishiwa pesa zao? Je Yanga wangekuwa tayari kutoa fidia kwa madhira hayo??

Kama kweli viongozi wanajua kuwa timu imesajiri wachezaji wazuri wa kitaifa na kimataifa kulikuwa na haja gani kugomea mchezo si bora timu ingecheza then wadai hizo 50ml angalau hata jamii ingewaelewa? Na hii ingeonyesha kuwa kweli viongozi wanathamini uwepo wa wachezaji wao ambao wanatafuta kung'ara kimataifa? Huoni kuwa hata wachezaji wa Yanga hawakutendewa haki kutocheza katika mchezo huo kwani ni kati ya michezo inayovutia macho ya watu wengi ndani na nje ya Tanzania na huenda ingekuwa na manufaa kwa wachezaji?

Kwa maoni yangu adhabu hiyo iliyotolewa inafaa sana na nina imani timu nyingine na viongozi wao wenye mawazo mgando wajifunze na kama wangetaka ushauri kutoka kwangu ningeshauri na timu ishushwe daraja. Hii tabia ya kuzilea Simba na Yanga ndio inayodumaza soka ya Tanzania. Na lazima watanzania tujifunze kukubali maamuzi magumu kama haya na sio kuleta ushabiki wa hovyo tu. Kama Yanga itakimbiwa na hao wachezaji haitakuwa jambo geni kwao kwani kuzaliwa kwa Pan Africa kulitokana na migogoro ndani ya Yanga lakini tulishuhudia Pan ikiwa timu nzuri iliyotokea katika historia ya soka Tanzania.

Na hii tabia ya kusema kuwa adhabu hiyo ni kubwa nini maana yake mmepima kwa kina athari ya kitendo cha yanga kutotokea uwanjani?? Tusiwe wajuzi wa kuzungumza mambo hata mahali ambapo viongozi wa klabu zetu wamefanya madudu kwa sababu ya ushabiki tu.

Hata Yanga ikifa leo nina imani soka Tanzania itadumu na kupanda chati...Mnakumbuka enzi za Pan Africa, Pamba ya Mwanza, Coastal Union ya Tanga, Maji Maji na timu nyingine nzuri soka ilikuwa ya ushindani na hata timu ya Taifa ilikuwa moto wa kuotea mbali?

Huko Simba na Yanga ndiko kwenye makaburi ya kuzikia vipaji vya wachezaji wetu na kama ningekuwa na uwezo hizi timu mbili ningezifuta katika ramani ya soka Tanzania nina imani tungekuwa na maendeleo.
 
Hadi vilabu vya nje ya Dar vikipata nguvu na mashabiki ndo utaweza kusema kuwa mpira wa Tanzania unaweza kuendelea bila Yanga na Simba. Kwa sasa Tanzania ukiiondoa Simba au Yanga kwenye ligi kuu, itabidi watu wahamie kwenye ngumi, riadha au vinyoya kwani washabiki watakuwa kiduchu na viingilio inabidi viwe chini. Nakumbuka kipindi ambacho klabu za Pamba, Coastal, Pan na Majimaji zilipokuwa na nguvu, na Simba ikawa inashuka daraja, ilibidi mbinu zitumike na Yanga wakakubali kufungwa mechi ya mwisho (ilishatwaa ubingwa) maana kuanguka kwa simba wakati huo kulimaanisha kudorora kwa mpira. Kwahiyo leo hii ukiifungia Yanga na ikaamua kujitoa ligi kuu, TFF itavunjik! Mark my word! Hao jamaa wa TFF wapo pale kwa kutegemea mapato yanayotokana na washabiki wa Yanga na Simba!

Kufungiwa kwa Yanga kamwe hakutasababisha TFF kufa!!! Hayo ni mawazo finyu, najua viongozi uchwara wa CCM na siri kali watafanya kila njia kuifungulia Yanga. FIFA ilishasimama kidete kuhakikisha vyama vya soka katika kila nchi haviingiliwi na sirikali katika maamuzi yake. Hivyo basi kama hao viongozi uchwara wanalijua hilo hawatafanya lolote.
 
Kufungiwa kwa Yanga kamwe hakutasababisha TFF kufa!!! Hayo ni mawazo finyu, najua viongozi uchwara wa CCM na siri kali watafanya kila njia kuifungulia Yanga. FIFA ilishasimama kidete kuhakikisha vyama vya soka katika kila nchi haviingiliwi na sirikali katika maamuzi yake. Hivyo basi kama hao viongozi uchwara wanalijua hilo hawatafanya lolote.

TFF inatakiwa kujustify hiyo adhabu siyo? wewe unadhani wanaweza kufanya hivyo? siyo suala la ushabiki hapa TFF wametokota, period!
 
TFF inatakiwa kujustify hiyo adhabu siyo? wewe unadhani wanaweza kufanya hivyo? siyo suala la ushabiki hapa TFF wametokota, period!

Yanga wanajiona wao ndiyo wao, hivyo wanaweza kuzidharau sheria za kandanda bila kuathiriwa na chochote, sasa TFF wameamua kufanya kweli. Na kama TFF wakiamua kuwa jeuri kama SIRI KALI itawaangilia ili wapunguze hiyo adhabu au kuifuta kabisa basi na wakalipeleka swala hilo FIFA na wao wakaamua kwamba serikali haina mamlaka ya kuingilia maamuzi ya chama cha soka, basi patakuwa patamu sana. FIFA inaweza kufungia Tanzania kutoshiriki mashindano yoyote duniani. Sasa sijui ni bora kufungiwa Yanga au Tanzania? Sisemi hapa kwa ushabiki bali kama mpenzi wa mpira ambaye anapenda kuona maendeleo ya kweli katika kandanda na kutokuwepo uhuni wowote. Timu yeyote ile ingefanya uhuni kama wa Yanga wa kugomea mechi kwa sababu zisizokuwa na kichwa wala miguu basi wangestahili adhabu kama waliyopewa Yanga.
 
Kutakuwa na utamu gani kwa TFF kama FIFA wataifungia Tanzania nzima?
 
Hapa watu wengi naona tunatoa maoni katika mtazamo wa ushabiki.
Washabiki wa simba wansherekea kupata tiketi ya kushiriki mashindano ya CAF.
Hivi mbona hatujiulizi ni sheria ipi iliyotumiwa na CECAFAkuwafungia Yanga?Ni kweli kuwa yanga haikutokea uwanjani, lakini hukumu inatolewa tu bila kuzingatian sheria?Hapa tunatakiwa tujue sheria za mashindano ya CECAFA zilikuwa zinasemaje kwa kosa kama hilo la yanga, sio kukomalia kusema tu yanga walistahili hiyo adhabu.Hata kwenye mahakama zetu unapotiwa hatiani unasomewa kifungu cha sheria kilichokutia hatiani na sheria uliyokiuka,sasa hapa naomba hawa wenzangu mnaosherekea yanga kufungiwa mnifahamishe kifungu cha sheria au kanuni iliyotumiwa kuwaadhibu yanga ili pengine nielewe mantiki ya maoni yenu.
Kitu kingine hapa ni ukweli kuwa kwa yeyote aliyefuatilia mashindano ya Kagame anafahamu kuwa mechi za yanga ndizo zilikuwa zinaingiza mapato makubwa kuliko mechi nyinginezo,kwa hiyo CECAFA na TFF walikasirika kiasi cha kutamani kuuwa mtu kutokana na yanga kutofika uwanjani kwa kuwa walishapiga mahesabu ya kugawana mamilioni. TFF walishatutangazia tokea mwanzo kuwa waliibembeleza serikali iwaruhusu kutumia uwanja mpya kwa ajili ya kupata mapato makubwa.
Jambo la mwisho ambalo kwa mtazamo wangu inabidi tuliangalie, ni je adhabu waliyopewa yanga inasaidia kuinua kiwango cha soka la Tanzania?Hapa ni dhahiri kuwa soka letu litaendelea kusuasua!Kila siku TFF hao hao wanahangaika kuitafutia timu ya taifa mechi za kirafiki za kimataifa ili kuwapatia wachezaji exposure, sasa hii adhabu kwa yanga itasaidiaje kuinua kiwango cha soka letu?Ikumbukwe kuwa yanga ina wachezaji wa timu ya taifa takribani tisa.
Mapato ndio yanaiua yanga, wazee wa TFF walishajua mil.500 hazikosekani.
Suala la kutokea vurugu halipo na halijawahi kutokea, mara ngapi mechi zinaahirishwa uwanja wa taifa kutikana na sababu mbalimbali kwa mfano mechi ya stars na angola iliyoahirishwa kufuatia shamba la bibi kujaa maji, mbona hatukurudishiwa viingilio vyetu? na hakuna vurugu yeyote iliyotokea?
Na wale wanaosema Tenga ni yanga, wasisahau kuwa huyo huyo Tenga ndiye aliwaongoza wachezaji wenzake akiwa nahodha, kuondoka yanga na kwenda morogoro kisha kurudi kuanzisha pan africa!Kwahiyo tenga ni mpenzi wa pan africa aliyoiasisi yeye mwenyewe.
 
Maamuzi ya TFF yalikuwa sahii nayaunga mkojno 100%.Unajua watanzania tumezidi na tabia ya kuangalia mambo kwa upeo mdogo,hili tukio la Yanga kutukubali kupeleka timu uwanjani kwa sababu ninazoweza kusema za "kitoto" madhara yake ni bahati mbaya hayakuonekana siku hiyo ila "impact" yake mbeleni ni kubwa mtaiona siku si nyingi.Moja ya harakaharaka ninoyoweza kusema kwa sasa ni kwamba kama kulikuwa na mtu mwenye kulenga kuwekeza katika Timu za kibongo kutokana na sera nzuri za michezo za serikali hivi karibuni kama kuwekaza katika vijana na viwanja vizuri, atasita kufanya hivyo kwani anopgopa yasije yakamkuta ya Yanga.na kwa ufupi niwaambie kuwa kama hilo jambo walilolifanya Yanga lingetokea katika nchi kama Argentina,Colombia,Uturuki au Uingereza ,nakwambia damu ambazo zingemwagika hapo uwanjani zisingekuwa za kawaida na tungeishiwa kufungiwa miaka mingi na FIFA.Basi tu kutokana na ukarimu wa wa Tanzania au niseme mechi yenyewe haikuwa na umuhimu sana pengine kutokana na aibu iliyolotwa na timu hizo mbili ktk mashindano hayo mwaka huu ndio maana watu walikuwa wapole. Na hii ndio linawafanya watu waanzekuona kuwa haukuwepo umuhimu wa adhabu.
Ukisema uwafungie viongozi wa Yanga nakwambia next year simba watafanya hivyo wakijua timu itaendelea kupeat.
asanteni
 
Back
Top Bottom