TFF wasikitishwa na kauli ya Bashe kuhusu mechi ya Simba na Yanga

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) limetoa wito kwa viongozi wote nchini kuacha kutoa kauli zinaweza kuchochea vurugu katika mpira wa miguu.

Kauli hiyo imekuja baada ya TFF kusikitishwa na kauli ya Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ambaye alisema waamuzi wa mechi ya Simba na Yanga iliyochezwa Julai 3 walidhibitiwa.

Bashe alisema waamuzi wangekuwa hawajadhibitiwa wangetoa adhabu ya penati dhidi ya Yanga. Kauli hiyo imeonekana kuchochea vurugu badala ya amani kutoka kwa kiongozi huyo.

Kwani kaongea kama waziri au shabiki? Mkanyeni mzee wa kigoma kwanza mwenye watu "wakubwa"polisi!
 
TFF inaingilia uhuru wa watu kutoa maoni yao. Ata Raisi angetoa maoni yake hayawezi kubadili matokeo au kuleta chuki. Mpira ni mchezo kama drafti au kombolelea au bao, siyo kitu serious ki hivyo.
 
Back
Top Bottom