TFF wametumia kigezo gani kuongeza muda wa usajili hadi Aug 15! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TFF wametumia kigezo gani kuongeza muda wa usajili hadi Aug 15!

Discussion in 'Sports' started by adakiss23, Aug 10, 2012.

 1. adakiss23

  adakiss23 JF-Expert Member

  #1
  Aug 10, 2012
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 3,346
  Likes Received: 655
  Trophy Points: 280
  Leo TFF wameongeza muda wa usajili hadi 15th Aug ambalo lilitakiwa lifungwe leo 10th Aug saa 6usiku. Wametumia vigezo gani kuongeza muda huo? Je hawana kalenda ya matukio? Au kwa kuwa Yanga hawajakamilisha usajili wa mchezaji wa 5 wa kigeni? Simba washakamilisha usajili wa kigeni cz kuna Twite Mudde Okwi Kanu na Sunzu. Azam washafunga usajili siku nyingi cz wana Blackberry Shikanda Balou n pacha wake Tcheche. Yanga bado m1 na bado mambo hayajaeleweka cz wanahitaji beki na Bin Kleb alikuwa Rwanda Rage akamuwahi akamsajili Twite akatoka akaenda kampala kakosa ikabidi arudi Kigali kurekebisha mambo. Sasa mpaka leo mchana mambo hayasomeki itakuwaje?? Ndo ikatumwa memo kwa prezdaa Tenga arefushe muda 'gumashi' lifanyike. Kwa mtindo huu ligi inaashiria kutakuwa na magumashi ya kutosha. TFF mpaka sasa hawajatoa ratiba ya ligi Kwanini? Wanasubiri nn? Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki soka letu!

  Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
   
 2. B

  Baba Kiki JF-Expert Member

  #2
  Aug 11, 2012
  Joined: May 31, 2012
  Messages: 1,366
  Likes Received: 487
  Trophy Points: 180

  Kwa kweli kutokana na TFF kushindwa kutoa maelezo ya kina yenye kuridhisha akili dadisi, una haki ya kujenga mashaka. Lakini kama wapo wenye taarifa za kutosha kwa nini muda wa usajili urefushwe, ni vizuri wakatujulisha na ikiwezekana watutajie nani walikuwa hawajakamilisha usajili na kwa nini.
   
 3. m

  matambo JF-Expert Member

  #3
  Aug 11, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 728
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  nasikia yanga wamemsajili mbuyu twite wa Simba, labda hili ndilo walilokuwa wanataka
   
 4. Bwana Mapesa

  Bwana Mapesa JF-Expert Member

  #4
  Aug 11, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,924
  Likes Received: 660
  Trophy Points: 280
  we waache watuone si wajinga opareshen SANGARA itaamishiwa TFF kwa mda wasituone maboya..watatoa roho za watu..kuna watu wanauchiz na haya mambo ya simba na yanga..wasiangalie hizo pesa chafu zinazomwagwa wanaweza kukosa pakwenda kuzitumia.
   
 5. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #5
  Aug 11, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Wenye taarifa za kutosha tupo,kwanza jiulize mwenyewe mpaka TFF wanatoa taarifa za kusogeza mbele mwisho wa usajili hiyo jana tarehe 10(siku ambayo ndo ilikuwa ndo iwe mwisho) team yenu ilishawasilisha hayo majina TFF? je ni team ngapi ambazo zilikuwa zimeshawasilisha?,ukijijijibu maswali haya ndo utaelewa kwanini TFF wamesogeza mbele kufungwa kwa pazia hili.
  Tuacheni ushabiki wa kishamba,team kama ilishakamilisha zoezi la usajili kwa kuweka kila kitu chake sawa itawezaje kuathirika kwa kusogezwa mbele,na kwanini walalamike mbona Azam ambao walishakamilisha kila kitu long time wapo kimya.
  Tafakarini na kuchukua hatua wapenzi na wanachama wa Simba,hao Viongozi wenu wameshawageuza "MABOYA"
   
 6. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #6
  Aug 11, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mimi naona huko Msimbazi hakuna watu wenye u'chizi na mema ya Club yao otherwise hapo kwenye red palitakiwa pahamishiwe kwa Rage,Kaburu na Msema ovyo wenu Kamwaga kwanza kabla ya TFF.

  Tafakarini na kuchukua hatua wapenzi na Mashabiki wa Simba, hao viongozi wenu washawaona "MABOYA"
   
 7. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #7
  Aug 11, 2012
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  YM anagawa hela hadi TFF
   
 8. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #8
  Aug 11, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Simba ni moja kati ya Club nzuri sana kuongoza kwasababu wengi(naomba nieleweke vizuri,wengi) wa Wanchama wao ni "MABOYA" wasiokuwa na uwezo wa kuona tatizo liko wapi.
  "adakiss23" with confidence unatuambia kuwa Simba ilishakamilisha usajili wa wachezaji wao wa kigeni ukimjumuisha na Twite just kwasababu Mh Rage aliwatamkia pale kwenye mkutano wenu mkuu kuwa alishakamilisha zoezi hilo tena kwa tambo nyingi tu namaneno ya kashfa tele kwa Mjumbe wetu wa Usajili Bin Kleb,wanachama wa Simba wakalipuka kwa nderemo hoihoi na vifijo wakasahau kabisa tabia ya uongouongo aliyo nayo Mwenyekiti wao,wakawatangazia pia kuwa angekuwepo uwanjani siku ya Simba day,matokeo yake hakuwepo,sasa nikikuuliza una vithibitisho gani kuwa usajili wa Twite Simba ulishakamilika, huna...na kama ulishakamilika mapovu ya nini sasa?
  Pia naomba nikujulishe kuwa kwa Yanga siyo lazima itimize wachezaji wote wa 5 wa kigeni,Yanga ya sasa hv ni tofauti kabisa na Yanga ile ya kuanzia mwaka jana kurudi nyuma,Yanga hii haisajili ilimradi imesajili tu kwa hawa wa nje inataka kuhakikisha ikisajili imesajili kweli majembe siyo sampuli za kina Mwape na Asamoah.
   
 9. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #9
  Aug 11, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,991
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  TFF ni kinyaa,haiwezi kuheshimu kanuni na taratibu zake,period.
   
 10. adakiss23

  adakiss23 JF-Expert Member

  #10
  Aug 11, 2012
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 3,346
  Likes Received: 655
  Trophy Points: 280
  Twite alisaini kaka. Sisemi kwa kuwa Rage amesema nilipata hiyo kwa mtu wa ndani kabisa ya klabu. Na ndio maana Yanga wamerudisha dola 30elfu ingawa simba wametakaa.

  Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
   
 11. m

  mzalendoasilia Member

  #11
  Aug 12, 2012
  Joined: Aug 10, 2012
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna tatizo la kimsingi kabisa ktk soka la TZ kama zilivyo siasa zetu. Kimsingi tatizo la TFF kuwa genge la kufanikisha mambo ya wenye fedha si siri tena. They are there to save their interests and the interest za hao WAKUBWA wao! TFF Yanga, wakubwa wa nchi Yanga dont expect any fairness kwenye maamuzi, na hili nazilaumu timu nyingine hasa SIMBA kwa kushindwa kulikemea kwa nguvu zote. Its high time now kwa wanasimba na wanamichezo kwa ujumla kutokubali kupelekwapelekwa na siasa za maagizo ya watoto wa wakubwa na wenye fedha ambazo hatuna hakika na wanakozipata na wanarudishaje pesa zao. Imefikia mahali Yanga wanajeuri ya kufanya chochote nchi hii, hata kupindisha sheria za wazi but there is no body analiona na kulikemea. Nitatoa mifano michache kuthibitisha hoja yangu; issue ya usajili wa CHUJI kutoka simba kwenda yanga mara ya kwanza, adhabu ya kinazi na kipuuzi ya wachezaji waliompiga refa mechi ya zanga na Azam,
  usajili wa Yondani , na hata hili saga jipya. Hauhitaji kuwa na PhD kujua kwamaba kuna upuuzi wa kufikiri kwamba wao yanga ndio Tanzania simply because they get support from the so called BIG GUNS. Wanasimba tupo wengi tusikubali kupelekwapelekwa na wahuni wachache kwa kuogopa kwamba kuna mkono wa WAKUBWA:
  Rage anaweza kuwa na matatizo yake, lakini kubwa zaidi si rage ni hili la TFF kutumika kufurahisha WAKUBWA kwa kila maamuzi double standardwanayofanya.
   
 12. m

  mzalendoasilia Member

  #12
  Aug 12, 2012
  Joined: Aug 10, 2012
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I dont care kama simba na yanga zote zikifa na kupotea kabisa . Tatizo hapa siusimba bali ni ulimbukeni wa kukubali watu wachache wafanye upuuzi wowote na yet
  wawe na jeuri kwamba hakuna wakuwafanya lolote. Why always issue inayohusu Yanga na Simba au timu nyingine lazima vitafutizwe vipengele vya ku justfy Yanga kuwa na haki? Ni wapi yanga wanapata details za mikataba ya wachezaji ambayo inawasaidia kufanya wanayofanya kama issue ya Yondani? inasemakana yondani alisajiliwa kutokea kamabi ya Stars, alitokajetokaje kambini kama si kwa jeuri ya yanga kwamba TFF ni yanga? If not so mbona yondani hakuchukuliwa hatua kwa kutoroka kambini kwenda kusaini? hivi huu upuuzi wote TFF mnadhani bado mnaweza jenga hoja nyinyi si yanga na watu wakawasikia na kuwaamini? TATIZO LANGU SI TFF; NIWANASIMBA KUKUBALI KUONEWA KWA KUOGOPA KUTETEA HAKI ZAO ZA KIMSINGI: Upuuzi huu ndani ya vyombo vya michezo ndio huohuo tunauona ndani ya siasa zetu. Pesa watoe wahindi , sisi na kimbelembele chetu tunajisifia sisi matajiri! utajiri upi walionao yanga? timu ambayo Tajiri akikasirika watu wanampigia magoti?
  Hivi watz tutaacha lini utegemezi na kupenda vya bure hata kufikia kutamba kwa fedha zisizo zetu? hivi simba na yanga kunawakumcheka mwenzake kwamba sisi ni matajiri? ndio maana umasikini hauwezi kwisha TZ sababu hao Matajiri washajua wapi na nini wafanye ili wazidi kutengeneza fedha toka shamba la bibi. Tutaendelea kudanganywa kwa pilau na vihela kidogo ili wao wazidi kuchota mali zetu na vizazi vyetu. Yanga na simba zinahazina kubwa ya wapenzi , lakini kuchwa hawaachi kuwapigia magoti na kuwaabudu BINADAMU wenzao huku wakitamba sisi ni MATAJIRI!
   
 13. m

  mzalendoasilia Member

  #13
  Aug 12, 2012
  Joined: Aug 10, 2012
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani wewe na yanga wenzako ndio maboya , coz wanaume kamili hawawezi kupita barabarani ukitamba mimi ninapesa wakati unajua pesa ni za mdosi. Ndio maana akijitoa kwenye timu hamuwezi fanya chochote mpaka mumpigie magoti tena! Ni aibu kubwa hata huwanashangaa inakuwaje mwanaume mzima ujitape kwa pesa binafsi za mtu mwingine! yanga ina mradi gani zaidi ya Manji? To me and many reasonable people, yanga inafaa kubadili jina na kuitwa Manji sports club, coz kila kitu anafanya yeye na wengine mlichobaki kufanya ni kujisifu! Think twice kati yako na hao unaowaita maboya , who is the real boya!
   
 14. naumbu

  naumbu JF-Expert Member

  #14
  Aug 12, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 3,305
  Likes Received: 3,790
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo simba ndo ina mradi?washabik wa Tanzania na timu zao wanachekesha sana
   
 15. M

  Maswalala Senior Member

  #15
  Aug 12, 2012
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sasa huo ni umaskin wa mawazo hakuna point uliyoongea hapo zote ni pumba kinacho kusumbua ni unazi wa kifala acha wivu usio na maana
   
 16. Bwana Mapesa

  Bwana Mapesa JF-Expert Member

  #16
  Aug 12, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,924
  Likes Received: 660
  Trophy Points: 280
  safi..muulize huyo Mbwa wamefanya biashara gan mpaka kuwa na uwezo wa kulipa mishahara wakati miez 2 iliyopita hata posho ilishindikana kuwepo..wachezaj nauli wanalipiwa na Chuji...ndomana jamaa wakigoma kinanuka..kuwen makin mtaachwa kwenye mataa.
   
 17. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #17
  Aug 13, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mtaita majina yote lkn Yanga itabaki kuwa Yanga "daima mbele,nyuma mwiko"
   
 18. Bwana Mapesa

  Bwana Mapesa JF-Expert Member

  #18
  Aug 13, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,924
  Likes Received: 660
  Trophy Points: 280
  hili jitu la wapi?...DAIMA MBELE Wakati daily NYI WAHAPAHAPA.......hata mkishiriki mashindano ya kimataifa mwisho Round ya Kwanza
   
 19. M

  Masuke JF-Expert Member

  #19
  Aug 13, 2012
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Mkuu achane naye huyo atakusababishia upigwe ban bure, wametukopesha nje ya uwanja sisi tutawalipa ndani ya uwanja subiri ligi ianze.
   
 20. Jaslaws

  Jaslaws JF-Expert Member

  #20
  Aug 13, 2012
  Joined: May 31, 2011
  Messages: 5,129
  Likes Received: 2,186
  Trophy Points: 280
  kumbe we ***** unapenda kutukana ukitukanwa unamaid,nasisitiza yanga nyote ni"MBWA"manji sports club.bado kidogo manji atatangaza ndoa kwa wanachama wote wa yanga endeleni kumchekea ,mwaka huu mtaolewa tena ndo ya kiislam...nakuombea uwe mkemkubwa.
   
Loading...