Kunguru Mjanja
JF-Expert Member
- Aug 22, 2012
- 2,036
- 3,929
Akizungumza leo Mubashara na kituo cha televisheni cha Azam Tv channeli ya Azam Sport 2, Kaimu Katibu Mkuu wa TFF akanusha tuhuma za kujilipa mamilioni na Kiernan unapoacha jambo la uongo lisambae mwisho litaonekana ni lakweli.
Rejea hapa; Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kujilipa posho mil. 438 kwa mwaka
Anaendelea Kaimu Katibu wa TFF kuwa
"Toka uongozi mpya uingie, tumejitahidi kuhakikisha tunaondoa makandokando hususan ya malipo na rushwa"
"Nataka niwahakikishieni suala la nyongeza ya posho halijawahi kuzungumziwa kabisa,"
"...Ndio kulikuwa na mjadala mkubwa juu ya posho ya kujikimu Rais na Makamu wake. Rais aligoma kupewa posho na kuandaa waraka wa kwanini hataki na amesisitiza mapato yote ya TFF yaende kwenye mpira moja kwa moja,"
"Posho pekee ambayo Rais amekubali iendelee ni Sh1.5 milioni kwa wajumbe wa kamati kuu kila baada ya miezi 3 na si milioni 1 kwa mwezi kama inavyodaiwa,"
"Hatukatai kukosolewa, lakini tukosolewe kwa haki. Siyo kutaka kuchafuliwa bila ya sababu. Tupo tayari kubaldilika. Ukipata habari kuhusu sisi njoo uthibitishe nasi,"
"Lazima tubadili utamaduni wetu wa kuongoza mpira ndani na nje ya TFF. Hivyo, baada ya kikao hiki mwanasheria wetu anaenda kuwaripoti kwenye vyombo husika watu wote waliokuwa wanasambaza taarifa hizi za uongo na kuchafua sura ya TFF,"
"Tayari tuna majina 10 ya watu ambao walikuwa wanasambaza taarifa hizi za uongo na kutuchafua kinyume kabisa na Sheria ya Mitandao. Tunataka wakathibitishe tuhuma hizi kwenye vyombo vya dola,"
"Naamini kuna watu watakaochukia kwa hizi hatua tunzochukua, lakini hatuwezi kurudi nyuma kwenye hili, hakuna aliye juu ya sheria. Lazima, kama mwanahabari uwe na uhakika na unachokiandika, hauwezi kukurupuka tu..."
"Tupo makini sana katika nidhamu ya kifedha, kwa mara ya kwanza TFF imeajiri mkaguzi wa ndani wa hesabu. Leo hii TFF hatulipani kwa 'cash' malipo yote yanafanyika kupitia benki, hii ni sehemu ya uwazi wa kifedha tunaopigania,"