Tff Waendekeza Njaa

Nungwi

Senior Member
Sep 9, 2006
196
12
Shirikisho la soka Tanzania(TFF) Limekuwa likiwanyang'anya jezi wachezaji wa Timu ya Taifa kila baada ya mechi. na kitendo cha beki wa timu ya Taifa Canavarro kubadilishana jezi na mshambuliaji wa kimataifa wa Cameroon-Etoo amelazimika kutozwa faini na TFF.

hivi hawajui kuwa Etoo kuchukua jezi ya Timu yetu ni kuitangaza nchi yetu?
Tff wana pata pesa nyingi sana kama kiingilio na hawana gharama zozote kwa timu kwani NMB na Serengeti wanaidhamini timu yetu, huu ni unyama unaofanywa na TFF hasa katibu mkuu Mwakalebela. habari zaidi iko gazeti la mwananchi.co.tz la leo.
 
Shirikisho la soka Tanzania(TFF) Limekuwa likiwanyang'anya jezi wachezaji wa Timu ya Taifa kila baada ya mechi. na kitendo cha beki wa timu ya Taifa Canavarro kubadilishana jezi na mshambuliaji wa kimataifa wa Cameroon-Etoo amelazimika kutozwa faini na TFF.
Hii hatari!Hata ukata si kihivyo jamani!
 
Jezi wanazotumia wachezaji wa timu ya taifa zinatakiwa zibakiawe kwa wachezaji hao kama sehemu ya kumbukumbu zao; kwanza nadhani kila jezi huwa ina jina la mchezaji mwenyewe aliyeitumia. Wachezaji wana tabia ya kubadilishana jezi baada ya mcehzo kama njia moja ya sportsmanship.

TFF vipi nyie? Nilikuwa na matumaini sana na uongozi bwa Leodgar Tenga lakini basi tena.
 
Back
Top Bottom