Tff! Ni Sawa Kuweka Kiingilio Kikubwa Namna Hii Au Ni Kutaka Kuvimbisha Matumbo Yenu?

Waga

JF-Expert Member
Feb 6, 2008
322
14
Jana afisa habari wa CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF) Frolian Kaijage, Alifanya press conference na kutangaza viingilio vya mechi ya TAIFA STARS NA CAMEROON, cha ajabu hawa jama wa TFF wametangaza viingilio vikubwa na vyenye kuwaumiza wavuja jasho wanaotaka kuja kuiangalia na kuishangilia Timu yao ya taifa bila kuangalia na kutathmin kuwa wanaoujaza uwanja wetu mpya wa Taifa ni hawa wenye uwezo wa kulipa si zaidi ya 15,000/= Nilifikiri kuwa somo wamelipata kwenye mechi mblizi zilizopita dhidi ya MALAWI ambayo ilikuwa ya kirafiki na dhidi ya Mauritius ambapo watu waliingia kwa wingi kwenye viti vya bei nafuu ambayo haikufikia 10,000/= lakini cha ajabu wamelifumbia macho somo hilo na kuendeleza ulafi wao.

ANGALIZO:-
Watanzania wanachoshwa na hali inayoendelea ya kutokuwa na mwelekeo wa timu yao ya Taifa na ipo siku maji yatawafika shingoni maana haituingii akilini kwa sababu Timu inapata udhamini mkubwa sana toka kwa wadhamini wawili ambao ni NMB na SERENGETI BREWERIES na pesa wanazotoa sinakuwa published lakini cha kushangaza timu inafanya uozo na kuwa na matokeo mabaya na mnazidi kuwakamua wapenda mpira wa nchi hii kwa kuwaekea kiingilio kikubwa namna hii ni nini haswa mnachokitaka kama si ufisadi?

Kwa kiingilio cha 50,000, 40,000, 20,000, 10,000, 7,000 kweli kabisa mnawaumiza watanzania ambao wana machungu ya kuliwa ka kodi zao na mafisadi.
Na katika pita pita yangu kwenye magazeti ni gazeti moja tu ndo nimeona wamelalamikia hili kwa kuandika kichwa cha habari STARS YAGEUZWA MTAJI VIINGILIO NA CAMERUNI VYATISHA!


Wana JF naomba tulipigie kelele hili swala maana hapa ndo pa kutoa malalamiko na dukuduku penye ufanisi na usawa na haki.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom