TFF na Taifa Stars yenu nini tatizo?

Ng'wanamangilingili

JF-Expert Member
Aug 22, 2015
5,704
4,737
Wasalamu in the name of football.

Kuna haja ya kuwa na mjadala wa kitaifa wa kwanini hatufanikiwi katika mpira wa miguu hasa timu yetu ya Taifa yaani Taifa Stars.

Ni aibu sana, watanzania wanaupenda sana mpira lakini mpira hauwapendi kivile, machungu na mapenzi yamebaki kwa timu za Simba na Yanga tu ambazo kwa namna moja au nyingine nazo zinchangia kudhoofisha mpira kimataifa hasa Taifa Stars na TFF kiujumla huku zikiimarisha mpira wa ndani.

Ni aibu iliyoje, tuna kila kitu katika miundombinu ya football ikiwemo moja ya viwanja bora na vikubwa barani Afrika, fanbase ya kutosha ila mafanikio kiduchu au hakuna kabisaaa tofauti na siasa tupu na serikali kuingilia mpira kupitia siasa inapoona tu Taifa Starz inajitutumua.

Sioni kama tuna program angalau ya miaka angalau kumi tu, hakuna. Ni kuunga unga tu.tunajivunia amani ila wasio nazo ndio wanchanja Mbuga, mfano SieraLeon,Burkina Faso, Ethiopia and the likes.

Mataifa mapya kabisa yaliyoingia mara ya kwanza AFCON hizi yanafanya maajabu the likes of Gambia, Comoros (tunaliitaaga koloni letu na wanategemea Kariakoo yetu kwa biashara )Cape Verde na hata Mauritius, Mauritania na Malawi hapa yaani zinadunda tu. Sijataja Zambia,Congo na hata Burundi.

Tujadiliane.
 
Makolo na Utoo...ndo tatizo.

Akili zenu ndo zimeishia hapo, alafu kila siku mbona tunawaambia. Hiyo ndo shida.
 
Hapo kwenye miundombinu umechemsha. Ligi inachezwa kwenye viwanja kama majaruba ya mpunga wewe unasema tuna kila kitu kisa ka uwanja kamoja.
 
Hapo kwenye miundombinu umechemsha. Ligi inachezwa kwenye viwanja kama majaruba ya mpunga wewe unasema tuna kila kitu kisa ka uwanja kamoja.
 
Matatizo ni kwa kila mtu.

Wachezaji wetu tunawapa vichwa kwa kucheza rafu na kuwasifu kama wachezaji wazuri.

Tunawatambua kwa kung'ara wanapocheza viwanja vibovu na tunawapa sifa lukuki kama vile ni wachezaji bora sana.Siku wakienda kwenye viwanja vizuri,wanaboronga.Wakikutana na waamuzi wasio na mahaba na upande mmoja,wanashindwa kucheza vizuri.


Ushauri wangu
Wanaoteua wachezaji timu ya taifa watangaze wazi kuwa,watachagua wachezaji waliofanya vizuri kwenye viwanja bora tu na sio kwenye majaruba.

Wachezaji wajitume sana wanapocheza vuwanja vizuri tuone uwezo wao.Na si kurukia rukia tu wachezaji wenzao maana michezo hii inaweza kulindwa hapa kwetu kwa ushabiki wa waamuzi,wakichexa mechi za nje wanaogopa kurukia hovyo wachezaji wenzao kwa kuogopa kadi
 
Back
Top Bottom