TFF na Karia wachunguzwe. Timu nyingi za ligi kuu masikini.Sababu kuipa haki ya kurusha ligi kuu TV moja tu

Kwo herufi ndogo tusingeona mpaka ukaamua utufokee kabisa kwa herufi kubwa...


KichWa bOx
 
Mnyonge mnyongenj ila Azam ametoa hela nyingi na anafanya kazi nzuri kwa nchi kama yetu mpira uliojaa figisu ni ngumu kupata mwekezaji wa nje kudumbukiza hela kama za Azam.
 
Kwenye muongozo wa kutumia jf, kipengele namba 3 kinaeleza kuhusu matumizi ya herufi kubwa! Sasa kinapokiukwa sijui ni kwa nini mods hawachukui hatua…
View attachment 2065762
Herufi kubwa ndogo kati mambo ya kizamani.wewe unaishi dunia hii au upo sayari nyingine?zamani wenye miandiko mizuri shuleni mnazawadiwa,siku hizi hata kalamu situmii.ualimu wako mpelekee mkeo au wanao.
 
Kwa ufupi tu naomba vyombo vinavyohusika na michezo na rushwa wachunguze mkataba katika ya TFF na TV moja kurusha live matangazo ya ligi kuu tena kwa miaka 10. Gharama walizolipa ni takriban billioni 200 na ushee. Duniani kote hakuna TV moja inayopewa haki bila ya kuzishindanishi tv zingine.Tunao star times, DSTV, ambao inasemekana waliomba lakini wakakataliwa. Ndio maana timu nyingi ni masikini kwani hawawezi kushindana na timu kubwa simba na yanga. Ilitakiwa iwe hivi, wote hawa 3 wanapewa haki kwa kila tv kutoa ofa halafu wanapewa michezo ya kuonyesha kutokana na malipo.

Ukiwajumlisha hawa 3, mfano azam atatoa bilioni 200, star times bilioni 200, DSTV billioni 300, jumla unapata haki za matangazo pekee bilioni 700. Bado kuna pesa za wadhamini wengine kama NBC N.K timu zenye mapato madogo yatafaidika sana. Angalia ligi kuu ya Uingereza ambayo ni ghali duniani timu zote 18 zinafaidika na matangazo ya tv pekee.Wameshindanishwa hivyo dau likapanda sana.Ligi hiyo almaarufu premier league matangazo pekee ya tv yanawaingizia dola bilioni 12.

Mchakato wao ni wa miaka 3 mitatu tu, sio kumi kama wa TFF, karia na azam. Skysports wana asilimia 60, BT sports 20 na amazon 20. Huu mkataba wa miaka 10 wa Karia, TFF na azam tena kwa miaka 10 unatia shaka sana. Daima yanga, simba, azam ndio watakaotawala.Isitoshe wan'gegawanya kwa TV hizi 3 ajira nyingi zingepatikana.Pia tuna DSTV ambao wanaonekana hadi ulaya, kodi zingeongezeka.Jamani waziri wa michezo amka twende na spidi ya dunia ya sasa. Naomba tena wahusika walichunguze hili suala. Football is top business earner duniani. Hata TRA amkeni. Naomba kuwasilisha.
We boya kweli aliyekwambia hawakushindanishwa ni nani? Ligi yetu haina viwango vya kutoa rights kwa tv zaidi ya moja, watakula hasara wote
 
Herufi kubwa ndogo kati mambo ya kizamani.wewe unaishi dunia hii au upo sayari nyingine?zamani wenye miandiko mizuri shuleni mnazawadiwa,siku hizi hata kalamu situmii.ualimu wako mpelekee mkeo au wanao.

Wee lofa kweli! Kwa hiyo jf wana mambo ya zamani siyo?
Hebu angalia andiko lako kama halijabadilishwa hizo herufi zako kubwa!
So waambie hayo mabadiliko waliyoyafanya wapeleke kwa watoto na wake zao!
Acha kuwa kumbafu…
 
Back
Top Bottom