SankaraBoukaka
JF-Expert Member
- Jul 2, 2019
- 910
- 1,394
Hili swala la wachezaji wa kigeni linaonekana kama zima moto lakini siyo mwarobaini wa Soka letu.
Hata tukiwa na mmoja wa kigeni soka letu bado lipo hapa hapa, tatizo letu kubwa ni ukuzaji wa vipaji tulivyonavyo. Kama tukiweza kusimamia hilo hata hao wa nje hakuna atakaosumbuka nao.
Cha muhimu ni kutafuta namna sahihi ya kuondokana na udumavu wa Elimu ya Soka.
Tengenezeni miongozo itakayoweza kusimamia FIFA CLUB LICENCING ambayo itafanya tubaki na timu ambazo zinauwezo wa kutengeneza vijana na kujiendesha. Ni bora muwe na ligi yenye timu chache hata 10 ambazo zitasaidia ukuaji wa soka letu.
Nafikiri kwa sasa swala muhimu ni vigezo vya ubora wa hao wachezaji wanaoletwa ambao hauna usimamizi unaoeleweka, hata kwenye ligi za Senegal, Ghana, Ivory Coast, Nigeria, Brazil, Argentina na Uruguay kuna wageni japo ni nchi ambazo zinazalisha wachezaji wengi duniani.
Kwa mtazamo wa haraka, ni kama tunatafuta visingizio ambavyo havitotutoa tulipo badala ya kuandaa msingi ambao utalitengeneza soka letu.
Halafu hii ligi yetu kiuhalisia inatakiwa kuwa na timu zisizidi 12. Maana kama vilabu hata kula ni shida ni vipi tupate Ligi Bora, na haya yote ndo yanatuporomosha. Timu nikiwa chache zitapata udhamini mnono that means zitaweza hata kuhudumia timu za vijana.
BMT na TFF kaeni chini mpange mipango ya kulisaidia SOKA acheni siasa.
Leo tunapigania wageni wakati hata ligi za vijana hakuna.