TFF MSIPOCHUKUA HATUA HARAKA KWA HILI KUNA SIKU YATATOKEA MAAFA.

Mohamed Mbelwa

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
507
272
Hakuna mahali popote duniani mshabiki wa soka aliyelipa kiingilo kuingia uwanjani anaruhusiwa kupigwa au kufanyiwa fujo.

Kuna wahuni wachache wasiojua mpira wanavamia soka letu. Na Kuna kila dalili wanataka kutuondolea utamaduni wetu wa soka letu.

Ikumbukwe kila mtu ana haki ya kushangilia timu yoyote aipendayo bila kubugudhiwa na mtu yeyote.
Kuwashangilia Zesco ni haki ya mshabiki wa Soka. Na kwa kufanya hivyo hajavunja Sheria yoyote ya nchi au ya soka.
Yanga wamekuwa wakishangilia wageni na wakati mwingine kupitiliza. Nani asiyejua Yanga msimu uliopita waliungana na Kocha wao Mwinyi Zahera kiasi Cha kusahau mechi yao na Lipuli kisa tu Simba inacheza na As Vita? Nani hakuwaona walivyojazana kuizomea Simba na Kuwashangilia Nkana? Ahly je? Walivaa jezi za wageni na hakuna aliyewabugudhi au kuwafanyia fujo kwa kuwa tuliamini ni haki yao. Kushangilia timu waipendayo.

Kichekesho ni kwamba wao wameonyesha hawajui mpira na sio wavumilivu katika mchezo huu. Yaani ni malimbukeni wa soka.

Wamepita kwenye vyombo vya habari wiki nzima wakihamasisha fuja na huu Tff inaona na haikuchukua hatua Wala kukemea. Kuna mjumbe mmoja wa kamati ya Yanga ya Hamasa alisikika waziwazi kila alipokuwa akipita kuhamasisha fujo. Mjumbe huyu ambaye haishi vituko vya kijinga kama kuweka mke rehani, kuzima kwa kuigiza wakati wa mechi, kuosha gari la Mabingwa wa nchi na mengine mengi ambayo na ya kujidhalilisha na kujishushia heshima. Kijana huyu mdogo ambaye nina wasisi hakupata malezi yetu ya kimaadili badala ya kuhamasisha watu wakajae uwanjani alitumia muda wake mwingi kuhamasisha mashabiki wa Yanga wakawapige mashabiki wa Simba. Tff ili iwe fundisho kwa wengine mnatakiwa muanze na huyu.
Fujo zilizotokea na mashabiki kuumizwa ni matokea ya ujinga wa watu wachache ambao wao wapo tayari kutafuta kiki hata kama njia watakayotumia inajenga uhasama na kuondoa amani uwanjani.

Wapo watu wenye heshima mbele ya jamii mliokuwa mkimpigia debe kijana huyu kwamba anaweza kufanya hamasa na mkafikia mahali mkamfananisha na Manara. Sasa ni kama amewavua nguo na kuwaacha uchi wale wote mliokuwa nyuma yake na kumpigia debe.

Tunaelewa athari za tabia hii ndio maana tunataka ikemewe na kukomeshwa mapema kabisa. Hatutaki ifike mahali tufungiwe uwanja wetu au tuamrishwe kucheza bila mashabiki kwa sababu ya wapuuzi wachache waliojivua ubinadamu na kujivika ujinga usio na faida yoyote kwa nchi Wala kwa klabu.

Nani asiyejua kinachoendelea katika viwanja vya Misri? Msidhani walianza siku moja wakafikia hapo walipo. Walianza taratibu Kama kilichotokea jana na baadae sumu ikakolea ndipo wakafika hapo walipo leo.

Tff ndio msimamizi wa soka na tuna imani mtachukua hatua haraka kuomesha huu upuuzi na Hawa watu wachache wanaovamia soka bila kujua misingi yake. Waswahili wanasemaa USIPOZIBA UFA UTAUJENGA UKUTA.
 
Yanga kuanzia kocha wao Mwinyi.
Hajawahi kuwapongeza timu pinzani wanapoishinda Yanga.
Yanga ni watu wa fujo kutokana kutostaraabika kwao.
Wanahitaji kufundwa Kama watoto wachanga.
 
Katufute Pesa acha kufuatilia mpira wa TZ utakuzeesha
 
Unalalamika Yanga msimu uliopita waliwashangilia wageni....umeshasahau kabla ya huo msimu uliopita simba walikua wanawashangilia kina nani?

Na nyie mkipata nafasi wapigeni.
 
Mkuu Nimefuatilia sana mabandiko yako ila nimegundua YANGA KWAKO NI KAMA ADUI Punguza munkari soka halipo hvyo mkuu utateseka sana usipobadilika soka s uadui pia tambua soka Lina utamaduni wake wa kipekee MM N MSIMBAZI DAMU ILA MWENZANGU UNA CHUKI
 
Kitendo Cha kutomtaja huyo kijana kimenifanya nikudharau ..
Hakika kwa majungu haya ya mleta Uzi, inabidi avalishwe vazi maalum akapige umbea wake huko na siyo hapa. Mod Uzi wa majungu, umbea na uchochezi kama huu unatakiwa kufutwa Mara moja. Halafu nyie mashabiki wa Bi Hindu fc kwa nini mnateseka hivi? Si mjipange kwa ajili ya muda mwingine yaani mwakani? Kwani aliyewaambia mashindano haya mwisho ni msimu huu nani? Kwa nini msikubali uwezo wenu umeishia hapo mlipofikia? Mnskuwa kama si watu wa mpira, mmejaa gubu tu na wivu, acheni hizo bwana, mnaboa.
 
Mkuu Nimefuatilia sana mabandiko yako ila nimegundua YANGA KWAKO NI KAMA ADUI Punguza munkari soka halipo hvyo mkuu utateseka sana usipobadilika soka s uadui pia tambua soka Lina utamaduni wake wa kipekee MM N MSIMBAZI DAMU ILA MWENZANGU UNA CHUKI
Mwambie aache swaga zake za uchochezi
 
Unalalamika Yanga msimu uliopita waliwashangilia wageni....umeshasahau kabla ya huo msimu uliopita simba walikua wanawashangilia kina nani?

Na nyie mkipata nafasi wapigeni.
Hajalalmika Yanga kuwashangilia wageni, hajapendezwa na kitendo cha Mashabiki wa Yanga kuwapiga mashabiki wa Simba wchache waliokuwepo uwanjani
 
Mkuu Nimefuatilia sana mabandiko yako ila nimegundua YANGA KWAKO NI KAMA ADUI Punguza munkari soka halipo hvyo mkuu utateseka sana usipobadilika soka s uadui pia tambua soka Lina utamaduni wake wa kipekee MM N MSIMBAZI DAMU ILA MWENZANGU UNA CHUKI
Ko kupigani Sio uadui, mana mtoa mada hoja yake ni kwamba kitendo cha mashabiki wa Yanga kuwapiga mashabiki wa Simba wachache waliokuwepo uwanjani Sio kizri.
Au we ulikua unachangia mada gani?
 
Hajalalmika Yanga kuwashangilia wageni, hajapendezwa na kitendo cha Mashabiki wa Yanga kuwapiga mashabiki wa Simba wchache waliokuwepo uwanjani

Wekeni video wanavyopigwa
Mara ngapi simba wanashabikia wageni na hamkupigwa?
 
Mashabiki wa yanga wengi ni maskini wa mali mpaka akili.
Tangu lini maskini akastaharabika?
 
Hakuna mahali popote duniani mshabiki wa soka aliyelipa kiingilo kuingia uwanjani anaruhusiwa kupigwa au kufanyiwa fujo.

Kuna wahuni wachache wasiojua mpira wanavamia soka letu. Na Kuna kila dalili wanataka kutuondolea utamaduni wetu wa soka letu.

Ikumbukwe kila mtu ana haki ya kushangilia timu yoyote aipendayo bila kubugudhiwa na mtu yeyote.
Kuwashangilia Zesco ni haki ya mshabiki wa Soka. Na kwa kufanya hivyo hajavunja Sheria yoyote ya nchi au ya soka.
Yanga wamekuwa wakishangilia wageni na wakati mwingine kupitiliza. Nani asiyejua Yanga msimu uliopita waliungana na Kocha wao Mwinyi Zahera kiasi Cha kusahau mechi yao na Lipuli kisa tu Simba inacheza na As Vita? Nani hakuwaona walivyojazana kuizomea Simba na Kuwashangilia Nkana? Ahly je? Walivaa jezi za wageni na hakuna aliyewabugudhi au kuwafanyia fujo kwa kuwa tuliamini ni haki yao. Kushangilia timu waipendayo.

Kichekesho ni kwamba wao wameonyesha hawajui mpira na sio wavumilivu katika mchezo huu. Yaani ni malimbukeni wa soka.

Wamepita kwenye vyombo vya habari wiki nzima wakihamasisha fuja na huu Tff inaona na haikuchukua hatua Wala kukemea. Kuna mjumbe mmoja wa kamati ya Yanga ya Hamasa alisikika waziwazi kila alipokuwa akipita kuhamasisha fujo. Mjumbe huyu ambaye haishi vituko vya kijinga kama kuweka mke rehani, kuzima kwa kuigiza wakati wa mechi, kuosha gari la Mabingwa wa nchi na mengine mengi ambayo na ya kujidhalilisha na kujishushia heshima. Kijana huyu mdogo ambaye nina wasisi hakupata malezi yetu ya kimaadili badala ya kuhamasisha watu wakajae uwanjani alitumia muda wake mwingi kuhamasisha mashabiki wa Yanga wakawapige mashabiki wa Simba. Tff ili iwe fundisho kwa wengine mnatakiwa muanze na huyu.
Fujo zilizotokea na mashabiki kuumizwa ni matokea ya ujinga wa watu wachache ambao wao wapo tayari kutafuta kiki hata kama njia watakayotumia inajenga uhasama na kuondoa amani uwanjani.

Wapo watu wenye heshima mbele ya jamii mliokuwa mkimpigia debe kijana huyu kwamba anaweza kufanya hamasa na mkafikia mahali mkamfananisha na Manara. Sasa ni kama amewavua nguo na kuwaacha uchi wale wote mliokuwa nyuma yake na kumpigia debe.

Tunaelewa athari za tabia hii ndio maana tunataka ikemewe na kukomeshwa mapema kabisa. Hatutaki ifike mahali tufungiwe uwanja wetu au tuamrishwe kucheza bila mashabiki kwa sababu ya wapuuzi wachache waliojivua ubinadamu na kujivika ujinga usio na faida yoyote kwa nchi Wala kwa klabu.

Nani asiyejua kinachoendelea katika viwanja vya Misri? Msidhani walianza siku moja wakafikia hapo walipo. Walianza taratibu Kama kilichotokea jana na baadae sumu ikakolea ndipo wakafika hapo walipo leo.

Tff ndio msimamizi wa soka na tuna imani mtachukua hatua haraka kuomesha huu upuuzi na Hawa watu wachache wanaovamia soka bila kujua misingi yake. Waswahili wanasemaa USIPOZIBA UFA UTAUJENGA UKUTA.
mashabiki wa simba mbumbumbu fc ndio wenye fujo waliharibu viti kwa kung'oa pale kwa mkapa hawana heshima wala ustaarabu,kweli mkuki kwa nguruwe tu binadamu mchungu, mtaje huyo kijana ni nani na aliepigwa
 
Back
Top Bottom