TFF mmewasikia Kanisa Katoliki?

MIGNON

JF-Expert Member
Nov 23, 2009
4,080
5,045
Leo nimepata wasaa wa kuangalia mechi ya Azam na Kagera Sugar. Waliovaa barakoa ni kama hakuna kabisa.

Tumewasikia Kanisa Katoliki na ni wajibu wa kila mtu 'kuchunga abiria wake". TFF himizeni wanaokwenda kuangalia mpira uwanjani wavae barakoa kwa kuanzia na ikiwezekana "social distancing'.

Kauli yenu moja inaweza kuokoa uhai wa watu wengi.
 
Leo nimepata wasaa wa kuangalia mechi ya Azam na Kagera Sugar.Waliovaa barakoa ni kama hakuna kabisa.Tumewasikia kanisa katoliki na ni wajibu wa kila mtu 'kuchunga abiria wake".TFF himizeni wanaokwenda kuangalia mpira uwanjani wavae barakoa kwa kuanzia na ikiwezekana "social distancing'

Kwani barakoa inazuia ugonjwa gani ili tuwashauli na wazungu?
 
Hivi kwanini unaloliona ni tatizo kwako mnataka liwe tatizo kwa kila mtu!?... Wewe waambie ndugu zako wavae barakoa,wakae ndani wasiende popote na humo ndani wazingatie social distance, wakapewe chanjo Kenya zimeshaletwa na wakirudi wakae ndani wakisubiri Corona iishe mwaka 2030. Watanzania wengine mtuache tuendelee na maisha yetu. Mnatuchosha na story za COVID.
 
Barakoa, chanjo wala vidonge havizuii ugonjwa wowote, ni maombi tu na nyungu.

Nashauri tufunge hospitali zote watu wapige maombi tu magonjwa yote yanapona kwa maombi na nyungu.

Hospitali za nini wakati Mungu yupo, tuzifunge zote hayo majengo tuyabadili yawe makanisa ili tutumie kufanyia maombi na kupiga nyungu.
 
Leo nimepata wasaa wa kuangalia mechi ya Azam na Kagera Sugar.Waliovaa barakoa ni kama hakuna kabisa.Tumewasikia kanisa katoliki na ni wajibu wa kila mtu 'kuchunga abiria wake".TFF himizeni wanaokwenda kuangalia mpira uwanjani wavae barakoa kwa kuanzia na ikiwezekana "social distancing'
Kauli yenu moja inaweza kuokoa uhai wa watu wengi.
Mtoa tarifa wa katoliki naye hakuwa hata na Barakoa
 
Leo nimepata wasaa wa kuangalia mechi ya Azam na Kagera Sugar.Waliovaa barakoa ni kama hakuna kabisa.Tumewasikia kanisa katoliki na ni wajibu wa kila mtu 'kuchunga abiria wake".TFF himizeni wanaokwenda kuangalia mpira uwanjani wavae barakoa kwa kuanzia na ikiwezekana "social distancing'
Kauli yenu moja inaweza kuokoa uhai wa watu wengi.
Hao wanafikiria kupiga PESA tu hawana utu huo niWALAFI
 
Leo nimepata wasaa wa kuangalia mechi ya Azam na Kagera Sugar.Waliovaa barakoa ni kama hakuna kabisa.Tumewasikia kanisa katoliki na ni wajibu wa kila mtu 'kuchunga abiria wake".TFF himizeni wanaokwenda kuangalia mpira uwanjani wavae barakoa kwa kuanzia na ikiwezekana "social distancing'
Kauli yenu moja inaweza kuokoa uhai wa watu wengi.
Hapa unataka kuleta vita dhidi ya TFF na Catholic
 
Leo nimepata wasaa wa kuangalia mechi ya Azam na Kagera Sugar.Waliovaa barakoa ni kama hakuna kabisa.Tumewasikia kanisa katoliki na ni wajibu wa kila mtu 'kuchunga abiria wake"...
Sidhani kama barakoa inasaidia kwenye msongamano kama huo. Watu wamebanana wanagusana na kutoka jasho.

Watu wajuliongeze waepuke mikusanyiko.
 
Hivi kwanini unaloliona ni tatizo kwako mnataka liwe tatizo kwa kila mtu!?... Wewe waambie ndugu zako wavae barakoa,wakae ndani wasiende popote na humo ndani wazingatie social distance, wakapewe chanjo Kenya zimeshaletwa na wakirudi wakae ndani wakisubiri Corona iishe mwaka 2030. Watanzania wengine mtuache tuendelee na maisha yetu. Mnatuchosha na story za COVID.
Ujinga wa mwafrika!!! Kama tatizo kwako halijafika huna haja ya kuwa concerned.Kwa upumbavu huu kama wa kwako ndio uliosababisha HIV ikasambaa kwa haraka.

Wazungu walichukua hatua mapema sisi marehemu aRemmy akaimba wimbo "Mambo kwa soksi" na wimbo ukafungiwa.Tulipogutuka tukawa tunagawa condom bure.

La pili sikutaja ugonjwa kwa hiyo usinilishe maneno.
 
Barakoa, chanjo wala vidonge havizuii ugonjwa wowote, ni maombi tu na nyungu...
Umeulizwa barakoa inazuia ugonjwa gani? Ili kama unafahamu ugonjwa unaozuiwa na barakoa basi, tuwapelekee na wazungu wapone. Sasa wewe unaanza kusema hospitali eti zifungwe ilitumwombe Mungu, kwani unafikiri Mungu hawezi kiituu?? Were jibu swali, uliloulizwa.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom