TFF kuweni wakali dhidi ya vitendo vya Ushirikina michezoni

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,323
4,667
Nadiriki kusema kuwa vitendo/imani za kishirikina ni kati ya vitu vinavyochangia mpira wetu kurudi nyuma baadhi ya wachezaji wetu wamekua wakiamini sana kuhusu imani hizo potofu katika mpira

Pia hata baadhi ya timu kuanzia zile za mchangani mpaka za ligi kuu nazo zimejikuta zikiingia kwenye huo mkumbo wa kuamini Ulozi ndo chanzo za kushinda uwanjani na hivyo kushindwa kufanya mazoezi na kujiandaa vizuri.

Ukijaribu hata kuwasikia wachezaji wa zamani wakihojiwa watakwambia vitendo ivyo vilikuwepo tangu enzi zao wengne waliishia kuviamini na matokeo yake bado walikula goli nyingi tu

Wanasema kwamba Ushirikina ungekuwa na nafasi nchi kama Nigeria leo ingekua na makombe yote ya dunia hii.

Mfano hapo kesho kuna mchezo mkubwa unaenda kuchezwa pale uwanja wa taifa nimepita katika mitandao mbalimbali nimeona baadhi ya picha zimetumwa zikiashiria vitendo vya ushirikina baadhi yake ni nazi zikiwa zimeandikwa maandishi nisiyoyajua,huku upande mmoja ukishutumu upande mwingine kuhusika.

Pia tumeshaona hata baadhi ya wachezaji wakikamatwa na baadhi ya vitu vinavyoashiria ushirikina uwanjani.

Siku zote tunaamin mazoezi,bidii,kujituma ndo chanzo cha ushindi uwanjani.

Hivyo TFF Inabidi wawe wakali sana kwa vitendo vyovyote vile vinavyoashiria ushirikina viwanjani ikiwepo kufanya uchunguzi makini na Timu husika ikibainika adhabu yake iwe hata Kupokwa pointi au hata kushushwa daraja.

KARIBUNI.
 
Back
Top Bottom