TFF Ishaanza Kuwasetia Simba SC Viporo Kwenye NBC Premier League

Hawa si waliingia mkataba na ATCL kwa safari za ndege za Air Tanzania.

Wakimaliza game Tar 17 jioni hiyo hiyo wanapanda dege lao wenyewe mpk Tz hata kabla siku haijapinduka, na Tar 20 wanakichafua ligi kuu, halafu tar 24 wanamalizana hao waswana

Hio kwanza inakupa faida ya game fitness, rejea game ya simba na Kaizer chipsi kule South, kumbuka simba alikuwa hajacheza mechi yoyote kwa muda wa siku takribani 12 na akafika kule akala mkono kasoro moya
 
Kama TFF itakuwa imebadilisha ratiba kutokana na ratiba za ndege ni sawa na haipaswi kulaumiwa kwani ratiba za ndege sio kama za mabasi ya mikoani ambapo likijaa tu dereva anawasha gari safari inaanza. Lakini kama ratiba za ndege zipo vizuri basi TFF wanapaswa kulaumiwa kwa kubadilisha ratiba.

Kwa upande mwingine kwenye hili suala naona mashabiki wa hizi timu kubwa mbili kila mmoja anavutia upande wake. Lakini wanapaswa wakumbuke kuwa viporo vinaweza kuwa faida au hasara kutokana na matokeo ya hivyo viporo.

Masahabiki wengi wa Simba wanafurahia sana ratiba kusogezwa mbele lakini wanasahau kuwa mwaka huu timu zipo vizuri sana na hasa mtani wao Yanga kwa hiyo iwapo Yanga atakuwa kashinda mechi zake hapo ndipo balaa litakapoanza kwa mashabiki, benchi la ufundi na hasa kwa wachezaji wa Simba. Kwani watakuwa wanacheza kwa presha kubwa ili kufukia pengo la pointi matokeo yake ndio wanaweza kujikuta wanaharibu. Na Simba wanapaswa wawe makini sana kwani mwaka huu Yanga wana timu imara sana na hawana mashindano ya mengine zaidi ya ligi kwa hiyo "concentration" yao itakuwa kubwa sana kwenye ligi. Na Simba ikifanya vibaya kwenye viporo basi mashabiki hawa hawa wa Simba wanaofurahia leo kubadilishwa ratiba ndio hao hao watakuwa wa kwanza kuilaumu timu yao kwa kukubali kubadilishiwa ratiba na wataenda mbali zaidi kuilaumu TFF kwa nini imebadilisha ratiba

Mashabiki wengi wa Yanga wanalalamika sana kuhusu kubadilishwa ratiba kwa kusogezwa mechi za Simba mbele. Lakini iwapo Yanga watafanya vizuri kwenye mechi zake za ligi halafu Simba akavurunda kwenye viporo basi ni mashabikii hawa hawa wataisifu timu yao na hutosikia kelele tena kwa TFF kubadilisha ratiba. Kinachotakiwa kwa Yanga sasa hivi wao wasilalamikie viporo wala nini bali wao wapambane wapate pointi tatu kwenye kila mechi ya ligi inayokuja mbele yao halafu wakae watulie wamwangalie Simba atakavyohangaika na viporo vyake kwani mwaka huu kila timu kwenye ligi ipo vizuri.

Kwa Yanga kama wanataka ubingwa kweli pambaneni chukueni pointi tatu kila mechi halafu tulieni juu ya msimamo wa ligi hapo hata mpinzani akiwa na viporo kumi vitakuwa havina shida sana sana ni matatizo tu kwake kwani atakuwa na presha ya kufanya vizuri na hapo ndio kuvurunda kunaanzia. Kwa Simba wao wasifurahie hivi viporo kwani mwaka huu timu zipo vizuri kwenye ligi kwani hakuna tena timu za kujichukulia pointi kirahisi zote zinakaza hasa. Na pia Simba wanapaswa kujifunza kilichowakuta kwa Kaizer walipokaa muda mrefu bila kucheza mechi ya ligi wakaenda kukutana na dhahama kule Afrika Kusini.
 
Masahabiki wengi wa Simba wanafurahia sana ratiba kusogezwa mbele lakini wanasahau kuwa mwaka huu timu zipo vizuri sana na hasa mtani wao Yanga kwa hiyo iwapo Yanga atakuwa kashinda mechi zake hapo ndipo balaa litakapoanza kwa mashabiki,
Kwa hiyo Yanga ikishinda mechi ilizotangulia, inaathiri vipi uchezaji wa Simba kwenye viporo? Kila mtu ashinde mechi zake, halafu hesabu zipigwe
 
Mimi nadhani issue sio kulalamika, ila simba wanahitaji Game fitness kabla ya hizo game za CAF champions league coz inaweza ikawa advantage kwao

Rejea game na wale Kaizer chiefs kule South, timu ilikaa bila game kwa siku takribani 12 na ilipokuwa inacheza inaonekana kabisa hawana game fitness
 
Ni mizunguko ya mechi mbili tu ambazo zimepita tangu ligi kuu Tanzania bara ya msimu wa 2021/22 ianze.

Tayari TFF (Wallace Karia) imekwishaanza kuweka mazingira ya kuzalisha viporo kwenye ligi. Yaani ndio kama hivyo, mapeeeeeemaaaaa!

Hebu fikiria. Ratiba ya mechi ya inapelekwa mbele siku saba (7) zaidi ili kufidia changamoto ya usafiri wa kurudi nchini ambayo itawafanya wakawie siku moja (1) tu.

Ikumbukwe. Simba SC wanacheza tarehe 17 huko Botswana na mechi ya ligi kuu ni tarehe 20. Hivyo basi hayo masaa 72 za hapo katikati hayawatoshi Simba SC kufika Dar kwa wakati na kucheza na Police Tanzania FC kwa Mkapa?

View attachment 1972314
Simba si ni timu Kubwa, wanashindwaje kukodi Ndege?
 
Mimi nadhani issue sio kulalamika, ila simba wanahitaji Game fitness kabla ya hizo game za CAF champions league coz inaweza ikawa advantage kwao
Sasa kama Simba hawahitaji hiyo game fitness, iweje wewe mshabiki mtopolo uionee huruma Simba eti unataka iwe na game fitness? Hilo ni suala la kiufundi, waachie wenyewe, wewe tafuta game fitness na JKU
 
Sasa kama Simba hawahitaji hiyo game fitness, iweje wewe mshabiki mtopolo uionee huruma Simba eti unataka iwe na game fitness? Hilo ni suala la kiufundi, waachie wenyewe, wewe tafuta game fitness na JKU
Sawa mashikolo mageni
 
Sijui kwanini kila time wenzako wanapo jaribu kutumia nguvu kubwa kuwaaminisha watu kua sio kweli kwa kauli ya manara aliyodai mashabiki wa yanga wenye utimamu ni baba yake na kikwete peke yao, wewe umekua mstari wa mbele kuwakatisha tamaa wenzako?
Kwa hiyo hata boss wake wasasa hayumo
 
Back
Top Bottom