TFF imemfungia Nyoso kwa miaka miwili kucheza mpira wa miguu

Kweli zifanyiwe kazi ili afungiwe miaka mitano na faini milioni kumi. . . .Na aliyefanyiwa kitendo hiko apewe uhuru wa kumpeleka mahakamani kwa mashtaka zaid ya udhalilishaji

Mkuu hiyo miwili inamtosha maana kwa umri alionao hawezi tena kurudi kucheza soka...
 
Marekani wakijua wataishinikiza TFF kuwa wanakandamiza haki za mchezaji! teh teh
 
Kumfungia miaka miwili si kumuua kabisa jamaa.Mi naona angefungiwa miezi kadhaa lakini apewe counselling ya nguvu katika muda huo.Maana jamaa inaonekana ni kawaida kwake kufanya vitendo vya kihuni.Jamaa inaonesha kapata malezi mabovu utotoni
 
Ni adhabu stahiki kwake.. Nyoso tukutane tena msimu wa 2017/2018.
Ila ni somo kwa timu zingine.. Kua makini na wachezaji waliotemwa kwa utovu wa nidhamu.. Poleni Mbeya City.
 
Na revise adhabu iwe miaka mitatu (3) pia fini milioni 5 (Tsh,5,000,000/=)
Hii itawafanya wale wenye vitendo kama hivi waheshimu kanuni na sheria!TFF naomba mrevise kanuni na sheria please.
 
mimi naona haitoshi,angefungiwa maisha kucheza soka.
Mpuuzi mkubwa huyo.

hupendezi na uzuri wako kuwa na roho ya kikatili kama hiyo...usisahau nyoso ana mke na watoto wanamtegemea acheze mpira wale wavae wasome...maisha ni adhabu kubwa sana...sawa na kuuwa familia yake.
 
Kufungiwa miaka miwili ni adhabu nzuri na inatosha kwa huyo Nyoso.
Ni sana na kufungiwa maisha.
atakaporudi, two years down the line, kiwango kimeshuka kama sio kuisha.
hakuna timu itakayomhitaji.
Keshajimaliza.
Wengine wajifunze, mpira ni ajira.
 
Kwani kuna official huu upande WA simba na huu WA yanga jamani huu si uchizi na sisi watu wa vila upande wetu upi
 
Mimi naona haitoshi,angefungiwa maisha kucheza soka.
Mpuuzi mkubwa huyo.

Naunga mkono hoja yako 100%.

Michezo ni furaha na si kudhalilishana wala uhasama.

Watu wanaoharibu jina la "mchezo" kama huyo mjinga wafungiwe maisha. Anashindwa kuelewa kuwa wanamichezo hususan mpira hapa kwetu wana influence kubwa sana kwa vitendo vyao kwa watoto.

Kuna siku mjukuu wangu alinambia "nataka kunyoa kama Baloteli", nilikuwa simjuwi ndiyo nani, akanambia ntakuonesha akioneshwa kwenye TV, mimi sikusubiri anioneshe nikaenda ku google, nikamuona Baloteli na alivyonyoa, kwanza nilicheka nikamwambia mjukuu wangu hapo utanisamehe sana, sikupeleki ukanyoe kiwazimu namna hiyo. Akanambia "mbona Baloteli kanyoa hivyo kwani yeye mwenda'zimu?". Nikakosa la kumjibu.

Nimeelezea hicho kisa kuonesha ni vipi hawa wachezaji wanaweza kuathiri jamii.

Kitendo alichokifanya si chema kabisa hafai kurudi uwanjani ukichukulia kuwa si mara yake kwanza kufanya hivyo, nimesoma sehemu kuwa alishawahi kufungiwa kwa kitendo kama hicho, hajakoma.
 
Safi sana. Nashauri hiyo faini apewe John Bocco kama kifuta jasho chake cha kudhalalishwa.

Iwe fundisho kwa wengine.

Hiyo faini hailipiki Mkuu. Jamaa kafungiwa miaka miwili kucheza soka, hakuna shaka faini hiyo inatakiwa ilipwe baada ya hiyo miaka miwili kutimia ili arudi uwanjani. Ukimwangalia Nyosso pale alipo baada ya miaka miwili atakuwaje? Huyu hatacheza tena hivyo hana sababu ya kulipa faini ya hiyo milioni mbili. Labda TFF imbane sasa hivi ailipe, lakini najiuliza tayari ameshafungiwa asipolipa atapewa adhabu gani?

Kwa maoni yangu adhabu pekee inayotekelezeka ni kufungiwa kucheza soka miaka 2 hiyo ya fedha haitekelezeki!
 
Na revise adhabu iwe miaka mitatu (3) pia fini milioni 5 (Tsh,5,000,000/=)
Hii itawafanya wale wenye vitendo kama hivi waheshimu kanuni na sheria!TFF naomba mrevise kanuni na sheria please.

Mkuu KakaKiiza revision yako ni nzuri sana lakini hebu tusaidie umeifanya chini ya Kanuni ipi ya Kanuni zipi?
 
Last edited by a moderator:
Hiyo faini hailipiki Mkuu. Jamaa kafungiwa miaka miwili kucheza soka, hakuna shaka faini hiyo inatakiwa ilipwe baada ya hiyo miaka miwili kutimia ili arudi uwanjani. Ukimwangalia Nyosso pale alipo baada ya miaka miwili atakuwaje? Huyu hatacheza tena hivyo hana sababu ya kulipa faini ya hiyo milioni mbili. Labda TFF imbane sasa hivi ailipe, lakini najiuliza tayari ameshafungiwa asipolipa atapewa adhabu gani?

Kwa maoni yangu adhabu pekee inayotekelezeka ni kufungiwa kucheza soka miaka 2 hiyo ya fedha haitekelezeki!

faini inalipwa na klabu kupitia nshahara wake na inalipwa kabla.
 
Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom