TFF imejipanga vipi kukabiliana na uwezekano wa kupanga matokeo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TFF imejipanga vipi kukabiliana na uwezekano wa kupanga matokeo?

Discussion in 'Sports' started by Zak Malang, Apr 10, 2011.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Apr 10, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wanajamvi, tujadili hili:

  Hivi TFF imejipanga vipi kukabiliana na uwezekano wa suala la kupanga matokea katika mechi mbili zihusuzo watani wa jadi -- Simba na Yanga leo? Nasema hivi kwani uko uwezekano mkubwa sana kupanga matokeo -- hasa kuzirubuni/kuzihonga timu pinzani -- yaani Majimaji na Toto Afrika ili zikubali kufungwa idadi kubwa ya magoli ili moja ya timu hizo -- yaani Simba au Yanga inyakuwe ubingwa mwaka huu. Nasema hivi iwapo timu zote mbili yaani Simba na Yanga zitashinda mechi zao za leo, kwani tofauti ni goal difference.

  TFF ni lazima iwe makini sana hapo. Ingawa bila shaka mechi zote mbili zitachezwa wakati mmoja, lakini kuna mawasiliano ya simu yanayoweza kutoa mwenendo wa mechi katika viwanja hivyo.

  Mimi nadhani TFF iangalie sana idadi ya magoli, yakiwa mengi, basi bila shaka kutakuwa kamchezi ka kupanga matokeo. Ningeshauri hilo likitokea, TFF isimtangaze bingwa hadi kwanza ifanye uchunguzi wa kina kuhusu matokeo ya kila uwanja.
   
 2. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #2
  Apr 10, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Ngumu kumesa...rushwa itatawala matokeo na maamuzi mkuu
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Apr 10, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Sasa TFF kazi yake nini? Ni lazima iwe makini kuhusu mchezo mchafu na isisite kufungia timu husika iwapo zitathibitka zilipanga matokeo. Ni lazima ifanye hivyo ili kuikoa soka kutoka disrepute.
   
Loading...