TFF hasara mil. 71/-

Congo

JF-Expert Member
Mar 13, 2008
2,062
2,288
TFF hasara mil. 71/-
MECHI YA STARS, GHANA



na Dina Ismail



MECHI ya kirafiki ya kimataifa kati ya timu ya Soka ya Tanzania, Taifa Stars, na Ghana, The Black Stars, iliyopigwa Agosti 20 kwenye Uwanja Mpya wa Taifa, Dar es Salaam, imeingiza hasara ya sh mil 71.

Hasara hiyo imetokana na maandalizi ya mechi hiyo iliyotambuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), kugharimu sh mil 186.5 huku mechi ikiingiza sh mil 114. 9.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Fredrick Mwakalebela, alisema kiasi hicho cha mapato ni kiingilio na haki za matangazo ya televisheni na fedha kutoka benki ya NMB.

Akitoa mchanganuo wa gharama, Mwakalebela alisema sh 126,337,473 zilitumika kuileta Ghana huku maandalizi ya Stars zikiwa sh 16,714,600.

Gharama za mechi zilikuwa sh 27,493,000 huku kukodi uwanja ikiwa ni sh 15, 981,800.

“Kwa mantiki hiyo, jumla ya gharama hizo ni sh 186,526,873 huku mapato halisi ya mechi yakiwa ni sh mil 114, hivyo tumepata hasara ya sh mil 71.

Mechi hiyo ilifanyika katika kuiimarisha Stars kwa mechi mbili za mwisho katika kukamilisha ratiba ya kusaka tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini na Mataifa ya Afrika, Angola, mwaka 2010.

Katika kampeni hiyo, Stars imepoteza matumaini ingawa imesaliwa na mechi mbili mkononi dhidi ya Mauritius na Cape Verde.

Mbali ya kampeni ya Afrika Kusini na Angola, Stars inakabiliwa na mechi mbili muhimu dhidi ya Sudan katika kutafuta tiketi ya fainali za Afrika kwa nyota wa Ligi ya Ndani, zitakazopigwa mwakani, nchini Ivory Coast.

Mwakalebela alisema kwa kujiandaa na mechi dhidi ya Mauritius na Cape Verde, huenda wiki ijayo Stars itaingia kambini Bulyanhulu, Shinyanga.

Hata hivyo, Mwakalebela alisema mazungumzo kuhusu kambi hiyo yanaendelea na uongozi wa mgodi wa Barrick huku akisema hakutakuwa na mabadiliko ya kikosi.

Kamati ya TFF ya Mashindano inatarajia kukutana leo kupitia masuala mbalimbali ikiwamo usajili wa wachezaji na makocha wanaoshiriki Ligi Kuu iliyoanza Agosti 22.

Katika hatua nyingine, mechi ya Ligi Kuu kati ya Simba dhidi ya Villa Squad iliingiza sh mil 21. 4 huku mechi ya Yanga na Prisons ya Mbeya ikiingiza sh mil 19.7.
 
Naombeni kuuliza. Kila mechi ya kimataifa ikichezwa TFF huwa inatangaza kuwa imepata hasara. Kwa vipi? Hawapangi budget kabla? TFF watusaidi kuchanganu hizo 126m/= zilivyotumika kuleta hiyo timu. Naona ni zaidi ya shs 5m/= kwa mtu!!!!!
 
.. Hivi faida ya uzoefu na exposure ambao timu inapata zinaweza kuwa-quantified? binafsi naona "investment in the future of the team" ndiyo gharama ya hiyo pesa. hakuna haja ya kulalamika.

...liwa ule ...(JK, Aug 08)
 
Wana JF, wakati nikiwa kwenye pitapita zangu mitaa ya maelezo nilikutana na uvumi kwamba Rais wa sasa wa TFF Ndugu L. C. Tenga hatogombea tena nafasi yake ya Urais mara ifikapo December, kipindi cha uchaguzi mkuu wa TFF. Je kwa mtazamo wako nani atafaa kumrithi huyu Mheshimiwa Tenga iwapo uvumi huo ni kweli?
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom