TFF hasara mil. 71/- | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TFF hasara mil. 71/-

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Congo, Aug 27, 2008.

 1. Congo

  Congo JF-Expert Member

  #1
  Aug 27, 2008
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,272
  Likes Received: 558
  Trophy Points: 280
  TFF hasara mil. 71/-
  MECHI YA STARS, GHANA  na Dina Ismail  MECHI ya kirafiki ya kimataifa kati ya timu ya Soka ya Tanzania, Taifa Stars, na Ghana, The Black Stars, iliyopigwa Agosti 20 kwenye Uwanja Mpya wa Taifa, Dar es Salaam, imeingiza hasara ya sh mil 71.

  Hasara hiyo imetokana na maandalizi ya mechi hiyo iliyotambuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), kugharimu sh mil 186.5 huku mechi ikiingiza sh mil 114. 9.

  Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Fredrick Mwakalebela, alisema kiasi hicho cha mapato ni kiingilio na haki za matangazo ya televisheni na fedha kutoka benki ya NMB.

  Akitoa mchanganuo wa gharama, Mwakalebela alisema sh 126,337,473 zilitumika kuileta Ghana huku maandalizi ya Stars zikiwa sh 16,714,600.

  Gharama za mechi zilikuwa sh 27,493,000 huku kukodi uwanja ikiwa ni sh 15, 981,800.

  “Kwa mantiki hiyo, jumla ya gharama hizo ni sh 186,526,873 huku mapato halisi ya mechi yakiwa ni sh mil 114, hivyo tumepata hasara ya sh mil 71.

  Mechi hiyo ilifanyika katika kuiimarisha Stars kwa mechi mbili za mwisho katika kukamilisha ratiba ya kusaka tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini na Mataifa ya Afrika, Angola, mwaka 2010.

  Katika kampeni hiyo, Stars imepoteza matumaini ingawa imesaliwa na mechi mbili mkononi dhidi ya Mauritius na Cape Verde.

  Mbali ya kampeni ya Afrika Kusini na Angola, Stars inakabiliwa na mechi mbili muhimu dhidi ya Sudan katika kutafuta tiketi ya fainali za Afrika kwa nyota wa Ligi ya Ndani, zitakazopigwa mwakani, nchini Ivory Coast.

  Mwakalebela alisema kwa kujiandaa na mechi dhidi ya Mauritius na Cape Verde, huenda wiki ijayo Stars itaingia kambini Bulyanhulu, Shinyanga.

  Hata hivyo, Mwakalebela alisema mazungumzo kuhusu kambi hiyo yanaendelea na uongozi wa mgodi wa Barrick huku akisema hakutakuwa na mabadiliko ya kikosi.

  Kamati ya TFF ya Mashindano inatarajia kukutana leo kupitia masuala mbalimbali ikiwamo usajili wa wachezaji na makocha wanaoshiriki Ligi Kuu iliyoanza Agosti 22.

  Katika hatua nyingine, mechi ya Ligi Kuu kati ya Simba dhidi ya Villa Squad iliingiza sh mil 21. 4 huku mechi ya Yanga na Prisons ya Mbeya ikiingiza sh mil 19.7.
   
 2. g

  gandil Member

  #2
  Aug 27, 2008
  Joined: Aug 1, 2008
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mh. Congo

  Kinachotatiza ni kwamba, ina maana cost za kuandaa mechi zilikuwa underestimated au mapato yalikuwa overestimated?
  Ninadhani TFF walipaswa kufanya analysis nzuri zaidi kuhusiana na hiyo mechi. Michezo ya namna hiyo sio endelevu kabisaa!

  Picha ninayopata ni kwamba, safu ya utendaji ya TFF ina walakini somewhere, na pengine kasoro hiyo isipoondolewa hasara kubwa zaidi zitatokea.

  Kama gharama za uandaaji zilibainika mapema kuwa ni kubwa kuliko mapato yaliyotarajiwa, basi hiyo mechi ingeahirishwa. Utabeba mechi za hasara ngapi??

  TFF ni ya watanzania na sio mtu binafsi. Viongozi waonyeshe kuwajibika kwa kutoa maelezo ya maana kwa wananchi.

  respect.
   
 3. Mtaalam

  Mtaalam JF-Expert Member

  #3
  Aug 27, 2008
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 1,276
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  wait a minute sijui kama nimeelewa vyema...tff wamekodi uwanja wetu wa taifa kwa ajili ya timu yetu ya taifa ya tanzania kutumia uwanja huo wetu wa taifa la tanzania kucheza mechi kwa bei ya milioni 16???hizo pesa zaenda wapiiii???
   
 4. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #4
  Aug 27, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  hapana kitu pale TFF wamezidi kubugia fedha za viingilio kila kukicha.
   
 5. C

  Chuma JF-Expert Member

  #5
  Aug 27, 2008
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  UFISADI kwenda Mbele....TFF waje safi...kinyume chake tutajua ni Timu ya MAFISADi tu...they didnt do anything tangible till now!!!
   
 6. C

  Chuma JF-Expert Member

  #6
  Aug 27, 2008
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  NMB walitaka kurudishiwa pesa zao? au?
   
 7. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #7
  Aug 27, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Kwasababu ni uwanja wa taifa basi utatumika bure? Hao wanaoutunza watalipwa nini? matengenezo atalipa nani?

  Hata kama ni uwanja wa taifa, ukitaka kuutumia inabidi kulipia.
   
 8. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #8
  Aug 27, 2008
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mtaalam,
  Hiyo nembo uliyoweka kama hapo ni kubwa sana katika medani za soka na hailingani na swali lako jinsi ulivyo uliza? Kukusaidia katika hilini hivi, hata ile timu ya Capello inapocheza pale Wembley hutengwa kiasi cha fedha ambacho hupelekwa kwenye huduma ya kiwanja. Kwahiyo basi, endapo uwanja kama umetumika na mapato yamepatikana ni vyema pesa ziende kwenye kuhudumia uwanja, vinginevyo uwanja hautakuweza kulipa gharama za kujiendesha
   
 9. Congo

  Congo JF-Expert Member

  #9
  Aug 27, 2008
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,272
  Likes Received: 558
  Trophy Points: 280
  Kimsingi ninachoshangaa ni gharama za kuileta timu, shs 126m/=. Yaani zimetumika zaidi ya shs 6m/= kwa mtu kwa hizo siku walizokuja. . Uwanja lazima ulipiwe ila formulae ya kulipia iwepo. Hebu tazama ghara za tiketi (9.91m/=). Hata kana tiketi hizo zingekuwa za aluminium au kutoka kiwanda kinachochapisha hundi za benki! Mtaalamu anisaidie
   
 10. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #10
  Aug 27, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Jamani ni kuunganisha tu dots, TFF ni mafisadi wa aina yake, Mwakalebela anakaribia kumzidi uzito Mh John Komba...ni pesa hizo hizo...mahesabu ya kijinga kabisa, Tkt zao huwa nifake sana hata hizo na mechi ya Ghana any serious stationery wanaweza zitengeneza sasa wenzetu wanatuambia gharama mil almost 10, please tumechoka
   
 11. Bonnie1974

  Bonnie1974 JF-Expert Member

  #11
  Aug 27, 2008
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 407
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  There is a problem there at TFF.
   
 12. M

  Mavanza Member

  #12
  Aug 27, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mnalipa gharama ya kuikosea Yanga. Lazima tukubali ukweli kuwa usipozitendea haki simba na yanga hapa nchini unaua kabisa morali ya soka. Mimi nahisi sababu mojawapo ya watu kutoingia mpirani kwa wingi sio jua isipokuwa wanazi wa Yanga wamesusa kuingia uwanjani, si kwa kupanga isipokuwa ile hamu ya kuanglia mpira inapotea tu kwa ajili ya kusononeka. Sasa kubalini tu uamuzi wa kamati ya Elmamri vinginevyo muamue ku-review budget yenu ya mwaka huu kwani mapato yatashuka tu. Haya msituulie unazi kwani huo ndio mtaji wenu.
   
Loading...