TFDA: Ufafanuzi kuhusu usalama wa mafuta ya alizeti

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,253
Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) imefanya uchambuzi wa awali wa matokeo ya utafiti uliofanywa mwaka 2014/15 na wataalamu kutoka Michigan State University Marekani wakishirikiana na SUA kuhusu mbegu za alizeti na mashudu kuchafuliwa na Aflatoxins.Sumu iletayo kansa yagundulika katika mbegu za Alizeti(sunflower seeds)

Uchambuzi huo umebaini kuwa utafiti huo ulihusu mbegu za alizeti na mashudu pekee hivyo hautoshelezi kuthibitisha kuwa mafuta ya Alizeti yanachafuliwa na Aflatoxins kwa kiwango hatarishi.

Hivyo wamesema wananchi waendelee kuyatumia mafuta ya Alizeti hasa yaliyothibitishwa na TFDA.

Hata hivyo TFDA itafanya uchambuzi wa kina wa matokeo ya utafiti huo na kufanya ufatiliaji na uchunguzi zaidi wa mbegu, mashudu na mafuta ya alizeti yanayozalishwa nchini.

Soma: Hivi vidonge ndani ya chupa za chai nini kipo nyuma yake? TFDA, TBS zatoa ufafanuzi

Rai inatolewa kwa vyombo vya habari kuwasilisha tafiti za kisayansi zinazohusu usalama na ubora wa chakula, dawa, vipodozi kabla ya kuchapisha ili kuondoa uwezekano wa kuleta hofu kwa jamii.

WhatsApp Image 2017-04-24 at 13.36.40.jpeg
 
Hapo namba 3 huu utetezi wa TFDA siuelewi, na nadhani umetolewa na mtu ambae hana weledi wa maswala haya.
Wanadai Mafuta yatakua hayana hiyo sumu sababu waliotafiti au waliopima walipima kwenye Mbegu na Mashudu, hawakupima Mafuta yenyewe.

Ni sawa na mtu aseme kua alilipima dafu (nazi changa/mbegu) akalikuta na sumu, akaja akapima machicha ya nazi (mashudu) nayo akayakuta na sumu, lakini tui lenyewe (ambalo halijapimwa) halitakua na sumu, sasa hayo machicha yamekuaje na sumu kisha isiwepo kwenye nazi??

Kwanini wao TFDA badala ya kupinga kua Mafuta ya Alizeti (ambayo hayajapimwa) hayana sumu basi wasichukue jukumu wao kuyapima ili tupate uhakika?? Kwanin wao wategemee utafiti wa wengine kisha wajiridhishe hapo na wasifanye utafiti wao wenyewe?
 
Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) imefanya uchambuzi wa awali wa matokeo ya utafiti uliofanywa mwaka 2014/15 na wataalamu kutoka Michigan State University Marekani wakishirikiana na SUA kuhusu mbegu za alizeti na mashudu kuchafuliwa na Aflatoxins.

Uchambuzi huo umebaini kuwa utafiti huo ulihusu mbegu za alizeti na mashudu pekee hivyo hautoshelezi kuthibitisha kuwa mafuta ya Alizeti yanachafuliwa na Aflatoxins kwa kiwango hatarishi.

Hivyo wamesema wananchi waendelee kuyatumia mafuta ya Alizeti hasa yaliyothibitishwa na TFDA.

Hata hivyo TFDA itafanya uchambuzi wa kina wa matokeo ya utafiti huo na kufanya ufatiliaji na uchunguzi zaidi wa mbegu, mashudu na mafuta ya alizeti yanayozalishwa nchini.

Rai inatolewa kwa vyombo vya habari kuwasilisha tafiti za kisayansi zinazohusu usalama na ubora wa chakula, dawa, vipodozi kabla ya kuchapisha ili kuondoa uwezekano wa kuleta hofu kwa jamii.

View attachment 500436
sasa yale ya barabarani singida na dodoma tuyaache:eek::eek:
kila tugusacho kina madhara wakati Mungu karuhusu tutumie, mara nyama mara mafuta ya wanyama mara alizeti, duuh
 
Hapo namba 3 huu utetezi wa TFDA siuelewi, na nadhani umetolewa na mtu ambae hana weledi wa maswala haya.
Wanadai Mafuta yatakua hayana hiyo sumu sababu waliotafiti au waliopima walipima kwenye Mbegu na Mashudu, hawakupima Mafuta yenyewe.

Ni sawa na mtu aseme kua alilipima dafu (nazi changa/mbegu) akalikuta na sumu, akaja akapima machicha ya nazi (mashudu) nayo akayakuta na sumu, lakini tui lenyewe (ambalo halijapimwa) halitakua na sumu, sasa hayo machicha yamekuaje na sumu kisha isiwepo kwenye nazi??

Kwanini wao TFDA badala ya kupinga kua Mafuta ya Alizeti (ambayo hayajapimwa) hayana sumu basi wasichukue jukumu wao kuyapima ili tup;ate uhakika?? Kwanin wao wategemee utafiti wa wengine kisha wajiridhishe hapo na wasifanye utafiti wao wenyewe?
Hapo nilipo natetemeka ,ukikwepa cholestor unakumbana na misumu cancer!
Ndugu, ni hatari!
Nenda TBS, TFDA na hizi taasisi nyinginezo mipakani kudhibiti bidhaa, wana vitengo vya valuation kuzidi hata TRA na wanachokusanya ni faini! Suala la viwango lina utata maana unaweza ukakuta bidhaa imetengenezwa Ujerumani au EU lakini wanasema iko chini ya viwango kwa sababu haina vibali vyao hata kama ina Certificate of Origin halali.
 
Kwakweli mmefanya jambo la maana sana kwa maana hayo ndio mafuta ambayo wengi waliamini ni salama kwa afya zao. vile vile tungependa matokeo ya tafiti yenu kuhusiana na content ya Aflatoxins, kwenye mafuta yawe published haraka ili kuondoa sintofahamu hii.
 
Hapo namba 3 huu utetezi wa TFDA siuelewi, na nadhani umetolewa na mtu ambae hana weledi wa maswala haya.
Wanadai Mafuta yatakua hayana hiyo sumu sababu waliotafiti au waliopima walipima kwenye Mbegu na Mashudu, hawakupima Mafuta yenyewe.

Ni sawa na mtu aseme kua alilipima dafu (nazi changa/mbegu) akalikuta na sumu, akaja akapima machicha ya nazi (mashudu) nayo akayakuta na sumu, lakini tui lenyewe (ambalo halijapimwa) halitakua na sumu, sasa hayo machicha yamekuaje na sumu kisha isiwepo kwenye nazi??

Kwanini wao TFDA badala ya kupinga kua Mafuta ya Alizeti (ambayo hayajapimwa) hayana sumu basi wasichukue jukumu wao kuyapima ili tup;ate uhakika?? Kwanin wao wategemee utafiti wa wengine kisha wajiridhishe hapo na wasifanye utafiti wao wenyewe?
Washakwambia utumie mafuta yaliyothibitishwa ubora. Matokeo ya wanasayansi husika hayakuhusisha mafuta kwa hiyo kisayansi wako sahihi kukanusha mpaka nao watakapofanya utafiti wao.
 
Tafiti hupingwa kwa tafiti sijui hawa wataalamu wetu huwa wamesomea wapi?
Mtu hajapima chochote hata hiyo mbegu ya alizeti hajui inaanzaje kupimwa hiyo sumu ila anasimama kupinga!

Yale Yale ya dr.Mwele na zika
 
HAYO NDIYO YATABAKI KUWA MAFUTA YANGU BORA KABISA.
Unsaturated fats ndio salama kwa afya ya mwanadamu.
 
Wasije wakawa wamekurupuka!
Maana utafiti wa vitu kama hivyo unahitaji muda wa kutosha, sio siku mbili au wiki moja.
 
kazi ipo, sijui tule nini ambacho hakina madhara!!!!!
Nimesikitishwa sana na majibu ya taasisi hii ambayo msingi wake ni wa kisayansi na inashughurika na sayansi. Majibu ya kisayansi hayajibiwi kisiasa hivyo, na upo utaratibu wa kisayansi wa kupinga hoja ya utafitiwa mtu aliyetoa matokea ya awali.

TFDA mlitakiwa kuja na utafiti wenu mkifuatia paramita za aliye watangulia na kukubaliana au kukataa matokeo ya utafiti wake kwa mujibu wa hoja zinazojibiwa na facts zenu mpya. Mnapingeje utafiti kwa maneno?, kiutafiti mbegu na mashudu zinautofauti gani na mafuta? kiasi kwamba uone kuwa kulichokuwemo kwenye mbegu na mashudu hakizi kuwemo kwenye mafuta.

sidhani kama ni sahihi kujibu hivyo mlivyojibu, fanyeni utafiti mje na majibu yenye fact na sio siasa na kuwalidhisha wafanya biashara na wakulima bila msingi wowote kwani mtu haishi mara mbili.
 
Daaah!
Hii ni njama ya kuudhoofisha kiuchumi mkoa wa singida.
 
Back
Top Bottom