Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,635
- 29,509
Wadau za Sikukuu,
Bila shaka mnaendelea vizuri na mapumziko ya Sikukuu. Mi langu ni moja tu, jana nimenunua nyama buchani huku Kijitonyama kilo moja kwa Tshs 15,000/=. Hii bei ni 250% (mara mbili na nusu) ya bei ya Tshs 6,000/= iliyokuwepo juzi. Huu ni wizi wa wazi, hakuna sababu ya msingi iliyofanya bei kupanda kwa kiasi hiki zaidi ya ulafi na uroho wa wafanyabiashara.
Kawaida inapofikia mwishoni mwaka kunakuaga na sikukuu, mamlaka ya usafiri wa nchi kavu na majini hua inakuaga makini kuhakikisha wafanyabiashara wenye vyombo vya usafiri hawawaibii wasafiri kwa kuwaongezea nauli. Lakini cha ajabu hili halifanyiki kwa Mamlaka ya chakula na madawa (TFDA). Hata kabla ya sikuu hii ya Eid, bado kipindi cha mfungo watu walikua wakinunua nafaka mbalimbaliu kwa bei ya juu kuliko kawaida na mamlaka hii ilikua imekaa kimya tu.
Waache na wao kukaa majumbani wakati wa sikukuu sababu tu sio siku ya kazi, bali waingie mitaani kuona jinsi wananchi tunavyoibiwa. Wahusika wa TFDA zingatieni haya, otherwise itabidi mtuambie kama mumeshindwa kazi ili tuwe tunanunua Nyama siku chache kabla ya sikukuu na kuzihifadhi tukisubiria siku ifike ili tule viporo.