TFDA inangoja watoto wangapi wafe ili wazifute cough syrup kwa watoto? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TFDA inangoja watoto wangapi wafe ili wazifute cough syrup kwa watoto?

Discussion in 'JF Doctor' started by Nduka, Mar 17, 2009.

 1. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 763
  Trophy Points: 280
  Hivi karibuni kumekuwa na taarifa za kufutwa kwa matumizi ya dawa za kikohozi na mafua kwa watoto chini ya miaka 12 na mamlaka nchini Kenya. Hali hii imetokana na madhara yanayosababishwa na dawa hizi. Kwa mujibu wa gazeti la Sunday News la tarehe 15 March 2009 tarifa za dawa hizi kuwa na madhara kwa watoto zipo tangu Julai mwaka 2007 ambapo kituo cha kuzuia na kudhibiti magonjwa cha Marekani(CDC) kilionya juu ya matumizi ya dawa hizi kufuatia vifo vya watoto watatu. Uchunguzi wa kituo hiki ulibaini zaidi ya watoto wengine 1,500 walifikishwa hospitali kwa matibabu ya dharura kutoka na matumizi ya dawa hizi. CHA KUSHANGAZA hapa Tanzania watendaji wa mamlaka ya udhibiti wa dawa na chakula wanadai wanaendele kuchunguza madhara ya dawa hizi.JE WANASUBIRI WATOTO WANGAPI WAFE ILI UCHUNGUZI WAO UWE UMEKAMILIKA?
   
 2. M

  Mzawa Halisi JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 500
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  May be wanataka kuthibitisha kuwa TDFA ni better than CDC in area of uchunguzi. Tatizo kubwa la wataalamu wazalendo ni kutumia taaluma zao kwa maslahi ya ama kisiasa au maslahi binafsi. Imechukua muda gani kupiga vita vipodozi vyenye madhara pamoja na kujulikana kwa muda mrefu.

  Leo hii ukitembelea maduka ya madawa hasa mbali na mijini yanaendeshwa na watu wasio na utalaamu kama fani ya ufamasia, hii inaonyesha jinsi gani hatuko serious na masuala ya afya ya raia wa Tanzania.
   
 3. DMussa

  DMussa JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2009
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 1,301
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Wakuu mimi ningependa kupata data halisi za huo uchunguzi wa CDC na pia ule wa Aghakhan Hospital maana wao ndio walikuwa wa kwanza kutangaza kuondoa madawa kadhaa katika list ya recommended pediatric Cough Syrups.
  I think we should know the contents maana tunaweza sema tuachane na hizo syrups then tukapewa alternative ya tablets/capsules with the same effect but different contect.
  Mimi ni mmoja wa wazazi na ningependa kulijua hili.... Any Doctor/pharmacist with these datas please assist! Sihitaji kusubiri mpaka TFDA wapige marufuku if these drugs aren't effective....
   
 4. k

  kakamiye Member

  #4
  Mar 17, 2009
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakuu!

  Kuna kitwa inaitwa EVIDENCE BASED MEDICINE,kwa ufupi recently hapa UK wameanounce officially kutotumika kwa hizo Paediatric Cough Syrups kwa watoto below six years of age, trend ni kuongeza age limit up to 12 years of age in the nearest future.Before it was below two years of age.

  Hii inatokana na kwamba hakuna ushahidi wowote kuwa madawa haya yana ponyesha watoto.

  Hii ni Historia ndefu kwa ufupi, most of drug discoveries huwa hazi wahusishi watoto of these ages kwa sababu za ki-ethical na Liability issues.

  Pamoja na hayo yote hili halizuii health proffessionals to use their common sense and duty of care to decide on prescribing these medicines.

  Kwa hiyo kinachotokea huko ni copy and paste results za clinical researches na decisions zilizofanyika hapa Europe na marekani na soon utasikia bongo nao wanaamua hivyo hivyo.

  Ahsanteni.
   
Loading...