TFDA hakuna dawa iliyosajiliwa kwa ajili ya kutibu Dengue

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imesema hadi sasa hakuna dawa waliyoisajili kwa ajili ya kutibu ugonjwa wa dengue.

Taarifa ya mamlaka hiyo iliyotolewa jana Jumatatu Mei 20, 2019 katika mtandao wake na kuthibitishwa na msemaji wa mamlaka hiyo, Gaudensia Semwanza leo Jumanne Mei 21, 2019, imewataka watu kupuuza dawa zinazoonyeshwa mitandaoni zikielezwa kuwa zinatibu ugonjwa huo.

Amezitaja dawa hizo kuwa ni Capria (carica papaya leaf extract tablets) na Papaya platelet booster tablet zinazodhaniwa kutengenezwa nchini India.

"Picha za dawa hizo zinasambazwa katika mitandao ya kijamii. TFDA inapenda kufafanua kuwa dawa tajwa hapo hazijasajiliwa na mamlaka yetu hivyo taarifa zinazosambazwa ni za kupotosha kuhusu kutibu dengue.”

"Kwa mantiki hiyo usalama, ubora na ufanisi wake haufai kwa matumizi hapa nchini na ieleweke kuwa TFDA haijasajili wala kutoa idhini ya dawa kwa ajili ya kutibu homa ya dengue,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Hata hivyo, mamlaka hiyo imesema kutokana na upotoshaji huo na kwa kuzingatia mfumo wa ukaguzi na ufuatiliaji wa dawa nchini, Mei 16, 2019 ilikamata vidonge 105 vya aina ya Carpill kutoka katika moja ya maduka ya dawa yanayouza dawa hizo jijini Dar es Salaam.

"TFDA inatoa wito kwa wananchi kuzingatia maelekezo yanayotolewa mara kwa mara na Serikali kupitia Wizara ya Afya kuhusu namna ya kujikinga na ugonjwa huo ikiwemo wale wanaopata dalili kufika katika vituo vya kutolea huduma za afya ili kufanyiwa vipimo na kupewa huduma," inasema taarifa hiyo.
 
Maji na parasol tu plus mijuisi ya kutosha na matunda. Unakunywa 5 t 6 litres za maji per day plus other fluids.
 
Back
Top Bottom