Teuzi za vijana zizingatie busara, hekima, uadilifu na umri, sio ukada tu

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
3,086
4,881
Hakika aliyoyafanya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya hai ni ushahidi tosha kuwa uteuzi wa viongozi mbalimbali bado una kasoro nyingi sana. Pamoja na kuwa vijana wapewe nafasi lakini sio vijana wa aina ya Sabaya, Makonda, Murro, Mnyeti hapi n.k

Vijana hawa wamedhihirisha kuwa uongozi kwa vijana ni kuwapa umungu mtu na kuwatendea mabaya wanao waongoza.Vijana walio wengi wakipewa madaraka wanajisahau kuwa wanatakiwa kuwatendea haki wananchi na kuwaheshimu na sio wananchi wawaogope wao viongozi. Wakati umefika wa kuteua vijana wenye busara, hekima, umri wa kuanzia miaka 40 na kigezo isiwe ukada.

Wakati wa utawala wa awamu ya kwanza nafasi za UDC, RC hata ubunge zilizingatia busara hekima na umri na walioteuliwa walipewa mafunzo ya uongozi.

Awamu ya 5 tumeshuhudiwa watu wa ajabu ajabu wanapewa nafasi za UDC, RC, Ubunge kwa kuwa ni wasemaji wazuri kuwatukana wapinzani na wengine mahusiano lakini sifa za uongozi hawana.
 
Matokeo ya YaTeuzi za Ukada ndio haya
JamiiForums2073931459.jpg
 
Sio VIJANA TEUZI MBAYA NI ZA UVCCM mbona KAFULILA HANA UJINGA MKOSAMALI MTATIRO HAWA HAWAKULELEWA NA UVCCM ILA KINA ALLY HAPPI MAKONDA SABAYA HERRY JAMES KASESERA SIJUI UVCCM INAWALEAJE VIJANA WAKE HAWANA ETHICS ZA UONGOZI KABISAA
 
Back
Top Bottom