Teuzi za kisiasa kwa wanahabari; Tutegemee nini katika tasnia ya habari?

Mtarban

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
3,818
5,007
Wimbi la kuwateua waandishi wa habari kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi ikiwemo ukuu wa wilaya, mkoa, ubunge, ukurugenzi n.k linazidi kushika kasi tokea awamu ya nne hadi awamu hii ya uongozi.

Tutegemee nini kwa waandishi waliopo au wanaotarajia kuingia katika tasnia hii muhimu ya habari hasa namna ya uandishi, utangazaji na namna ya uripotishaji wao wa habari kupitia vyombo vya habari km vile TV, radio, magazeti na mitandao ya kijamii?
 
Serikali ina akili maaana ukiona mtoto analia lia kila wakati mpe mtaji basi hapo zile kelele zoteee zinapotea Taraattiibuu...
 
Nadhani Rais wetu kafanya jambo la maana sana. Godwin Gondwe kateuliwa kwa vile yeye ni mwanasiasa japo ni mtangazaji. Aligombea Ubunge kwa tiketi ya CCM japo kura hazikutosha. Kwenye uteuzi huu wakuu wa wilaya walioteuliwa kutoka kwenye tasnia ya habari ni wawili tu wakati Kikwete aliteua 7. Ni uwakilishi mzuri
 
Hata uandishi wako leo unaonekana una kigugumizi tu
 
sioni ni kwa namna gani siasa zimeweza au zinaweza kuingilia majukumu ya watu ya kila siku, kwani bado tumeendelea kuona baadhi ya media zikiandika habari zinazoikosoa serikali despite political appointments zinazofanyika.
 
Nyie vijana wafia chama mitandaoni huu ndio mwisho wenu
Kukua kwa sayansi na teknolojia kunaifanya mitandao kua mojawapo ya jukwaa kama majukwaa mengine yalivyo hivyo...siasa za mitandaoni haziepukiki na zitaendelea kuwepo as long as mitandao bado ipo...
 
Kukua kwa sayansi na teknolojia kunaifanya mitandao kua mojawapo ya jukwaa kama majukwaa mengine yalivyo hivyo...siasa za mitandaoni haziepukiki na zitaendelea kuwepo as long as mitandao bado ipo...
Utashinda mtandaoni wakati huna uhakika wa mlo wako wa siku?magu kaamua kuwatupa
 
Kazi ya ukuu wa wilaya siyo ya kitaaalamu (non professional). Kwa hiyo wanateuliwa kutoka nyanja mbalimbali za uelewa!
 
wimbi la kuwateua waandishi Wa habari kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi ikiwemo ukuu Wa wilaya, mkoa, ubunge, ukurugenzi n.k linazidi kushika kasi tokea awamu ya nne had I awamu hii ya uongozi. tutegemee nini kwa waandishi waliopo au wanaotarajia kuingia katika tasnia hii mhimu ya habari hasa namna ya uandishi, utangazaji na namna ya uripotishaji wao Wa habari kupitia vyombo vya habari km vile TV, radio, magazeti na mitandao ya kijamii?
Kujikomba tu kutatamalaki in anticipation........????
 
wimbi la kuwateua waandishi Wa habari kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi ikiwemo ukuu Wa wilaya, mkoa, ubunge, ukurugenzi n.k linazidi kushika kasi tokea awamu ya nne had I awamu hii ya uongozi. tutegemee nini kwa waandishi waliopo au wanaotarajia kuingia katika tasnia hii mhimu ya habari hasa namna ya uandishi, utangazaji na namna ya uripotishaji wao Wa habari kupitia vyombo vya habari km vile TV, radio, magazeti na mitandao ya kijamii?
1. Kuegemea upande waobebwa
2. Kulipoti mazuri tu ya viongozi
3. Kuwachomea wengine wanaowapinga wanaowabeba
4. Kujipendekeza
5. Kutozingatia maadili ya utangazaji.
 
Back
Top Bottom