TEUZI: Rais Samia Suluhu ateua Majaji wa Mahakama ya Rufani, Majaji wa Mahakama Kuu. DPP Mganga ateuliwa kuwa Jaji

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Jan 27, 2018
648
1,000
Rais Samia amefanya teuzi za Majaji wa Mahakama wa Rufani, Mahakama Kuu na Kumwongezea muda Jaji Mahakama ya Rufani.

1.jpg

2.jpg

3.jpg
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
12,467
2,000
Naona nafasi ya DPP bado Mh. Rais Samia Suluhu Hassan anakuna kichwa kumtafuta mtu sahihi kwa matakwa ya Jamhuri ya Muungano.

MKURUGENZI WA MASHTAKA
Mkurugenzi wa Mashtaka ni mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka. Mkurugenzi wa Mashtaka ndiye msimamizi mkuu wa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka, Wakurugenzi, Wakurugenzi Wasaidizi, Mawakili wa serikali na Waendesha Mashtaka katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

Majukumu ya Mkurugenzi wa Mashtaka yatakuwa ni:

 • (i)Kuamua kushtaki au kutoshtaki kwenye makosa ya jinai;
 • (ii)Kuanzisha, kuendesha na kusimamia mashtaka ya makosa ya jinai katika mahakama zote isipokuwa mahakama za kijeshi;
 • (iii)Kutwaa na kuendelea na mashtaka ya kesi yoyote ya jinai iliyofunguliwa na mtu au taasisi nyingine;
 • (iv)Kufuta mahakamani mashtaka yoyote ya jinai yaliyofunguliwa na mtu au taasisi nyingine katika hatua yoyote kabla hukumu kutolewa;
 • (v)Kutoa maagizo kwa jeshi la polisi au vyombo chunguzi vyoyote kuchunguza taarifa yoyote ya kijinai na kutoa taarifa kwake haraka inavyowezekana;
 • (vi)Kuchukua hatua muhimu kwa jambo lolote lenyetija katika mashtaka ya jinai;
 • (vii)Kutoa miongozo inayohusu uratibu wa upelelezi na uendeshaji mashtaka;
 • (viii)Kuteua na kutenguamamlaka ya waendesha mashtaka wa umma;
 • (ix)Kumshauri waziri mwenye dhamana katika masualaya mashtaka yanayohitaji sera au hatua za kibunge;
 • (x)Kuteuwa maafisa maalum ndani ya taasisi za serikali kusimamia mali zilizozuiliwa au kutaifishwa na mahakama katika mazingira ambayo ni vigumu kuteua wasii;
 • (xi)Kufanya kazi nyingine ambayo zinahusiana na mashtaka ya umma;
 • (xii)Kuwasimamia maafisa sheria, mawakili wa serikali na watumishi wengine walioteuliwa au kuajiriwa na ofisi ya taifa ya mashtaka;
 • (xiii)Kusimamia shughuli zote zinazofanywa na maafisa sheria, mawakili wa serikali na watumishi wengine ndani ya ofisi ya taifa ya mashtaka;
 • (xiv)Kuita afisa yoyote wa umma kutoa maelezo au taarifa kuhusiana na jambo lolote ambalo linahusu mashtaka ya umma;
 • (xv)Kuandaa na kuwasilishakwa waziri taarifa ya nusu mwaka na nakala kwa mwanasheria mkuu wa serikali kuhusu utekelezaji wa majukumu ya ofisi ya taifa ya mashtaka; na
 • (xvi)Kuteua au kuajiri na kuwajibisha maafisa sheria, mawakili wa serikali na watumishi wengine ndani ya ofisi ya taifa ya mashtaka.
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
12,467
2,000
Awamu ya Sita ya Mh. Rais Samia Suluhu Hassan inazidi kujikita mizizi yake kwa kupanga safu za nafasi muhimu.

Nafasi ya DPP siku zote akitaka kuondolewa ni kumpandisha awe jaji ili umuondoe .

DPP cheo ni cheo kikubwa chenye kinga kikatiba na dawa ya kumuondoa ni kumpandisha cheo kama katika teuzi ya Leo

Soma zaidi kuhusu DPP Historia ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka |Ofisi ya Taifa ya Mashtaka

Mkurugenzi wa Mashtaka ambaye anatoa mchango mkubwa katika kusimamia haki jinai.Kwa mujibu wa Ibara ya 59B ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Mkurugenzi wa Mashtaka amepewa uwezo na mamlaka ya kusimamia uendeshaji wa mashtaka yote ya jinai katika Mahakama zote isipokuwa mahakama za kijeshi.Kwa msingi huo, Mkurugenzi wa Mashtaka ana uwezo wa kufungua, kuendesha na kusimamia mashtaka yote ya jinai nchini.Kutokana na Ibara hiyo ya Katiba, Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Mashtaka hayamhusu mtu mwingine yoyote au mamlaka nyingine na hawajibiki kusimamiwa na mtu mwingine yoyote au mamlaka nyingine.Katika kutekeleza majukumu yake, Mkurugenzi wa Mashtaka anatakiwa kufuata kanuni zifuatazo:Kutenda haki; Kuzuia ukiukaji wa taratibu za kisheria; na maslahi ya umma.Nafasi hii imewekwa chini ya kifungu cha 8 cha Sheria ya Taifa ya Mashtaka, Sura ya 430.
 

Jasmoni Tegga

JF-Expert Member
Oct 28, 2020
4,512
2,000
Hakuna pesa ya kupeleka kwenye miradi ndiyo anaitafuta, huyo alikuwa anazindua mpaka barabara ambazo zilizinduliwa na Mkapa asee

Una maana ileee safari ya kwa M7 na kwa Mr Freedom juzi, nyumba ya Jamaa wa Msoga na Benzi ya Mzee Ruksa vimekomba ^killer-key-2^ pale hazinani. Kumbe ndiyo maana waliharakisha sanaaa kumpandisha cheo Dkt Mpango ili atoke kule wafanye yao!??? Hii ni hatari na robo ^tar-two^¡¡¡ Nahisi kufikia mwisho wa mwaka Bi Mkubwa lazima atatembeza bakuli la michango huku mtaani, kama ndio mwendo huu.
 

Kambaku

JF-Expert Member
Nov 12, 2011
4,027
2,000
Bi Mkubwa ndiyo kazi pekee anaweza labda na kusafirisafiri -- ila kwenda kukagua miradi ya maendeleo anaona karaha. ^Ilikuwa Dkt Mwinyi ndiye awe Makamo wangu^ JPM
Kuteua na kutumbua nadhani 'mungu' wako bado anaongoza, usiseme kabisa hii ndio kazi mama anayoweza! Sasa ulitakaje, muda wa majaji umeisha akae tu asiteue majaji?

Acha chuki dogo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom